< Isaya 48 >

1 “Sikilizeni hili, ee nyumba ya Yakobo, ninyi mnaoitwa kwa jina la Israeli, na mnaotoka katika ukoo wa Yuda, ninyi mnaoapa kwa jina la Bwana, mnaomwomba Mungu wa Israeli, lakini si katika kweli au kwa haki;
Sikiliza hili, nyumba ya Jakobo, mlioitwa kwa jina la Israeli, na mmetoka katika mbegu ya Yuda; yeye akirie kwa jina la Yahwe na kumuhusisha Mungu wa Israeli, lakini sio kweli wala kwa namna ya haki.
2 ninyi mnaojiita raiya wa mji mtakatifu, na kumtegemea Mungu wa Israeli, Bwana Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake:
Maana wanajiita wenyewewatu wa mji mtakatifu na kumuamini Mungu wa Israeli; Yahwe wa majeshi ndilo jina lake.
3 Nilitoa unabii mambo ya kwanza tangu zamani, kinywa changu kiliyatangaza na kuyafanya yajulikane; kisha ghafula nikayatenda, nayo yakatokea.
''Nimetangaza vitu kutoka siku nyingi; Wamekuja nje kutoka mdomoni mwangu, na nimewafanya wajulikane; halafu gafla nimewafanyia, na yakatimia.
4 Kwa kuwa nalijua jinsi ulivyokuwa mkaidi; mishipa ya shingo yako ilikuwa chuma, kipaji chako cha uso kilikuwa shaba.
Kwa sababu nilijua kwamba wewe ni mkaiidi, misuli ya shingo yako ni kama ya chuma, na paji la uso ni kama shaba,
5 Kwa hiyo nilikuambia mambo haya tangu zamani, kabla hayajatokea nilikutangazia ili usije ukasema, ‘Sanamu zangu zilifanya hayo; kinyago changu cha mti na mungu wangu wa chuma aliyaamuru.’
Hivyo basi nilitangaza vitu hivi kabla havijatokeo hivyo, nilikujulisha wewe, 'Sanamu yangu imefanya haya au sanamu yangu ya kuchonga na sanamu yangu ya kuyeyusha, yamekwishisha vitu.
6 Umesikia mambo haya; yaangalie hayo yote. Je, hutayakubali? “Kuanzia sasa na kuendelea nitakueleza mambo mapya, juu ya mambo yaliyofichika usiyoyajua.
Umesikia kuhusu mambo haya; angalia ushahidi wote; na wewe, Je hautakubali kwamba ninacho kisema ni cha kweli? Kuanzia sasa na kuendelea Nitawaonyesha vitu vipya, mambo yaliyofichika ambayo hamkuyajua.
7 Yameumbwa sasa, wala si tangu zamani; hukupata kuyasikia kabla ya siku ya leo. Hivyo huwezi kusema, ‘Naam, niliyajua hayo.’
Sasa, na sio yaliyopita, yamekuwa sasa, na kabla ya leo hamkusikia kuhusu wao, hivyo hautaweza kusema, 'Ndio, nilijua kuhusu wao.'
8 Hujayasikia wala kuyaelewa, tangu zamani sikio lako halikufunguka. Ninafahamu vyema jinsi ulivyo mdanganyifu, uliitwa mwasi tangu kuzaliwa kwako.
Haukusikia; haukuelewa; haya mambo hayakufuniliwa katika masikio kabla ya. Maana nilijua kwamba umekuwa mdanganyifu, na kwamba umekuwa muasi kutoka kuzaliwa.
9 Kwa ajili ya Jina langu mwenyewe ninaichelewesha ghadhabu yangu, kwa ajili ya sifa zangu nimeizuia isikupate, ili nisije nikakukatilia mbali.
Kwa niaba ya jina langu nitahairisha asira yangu, na kwa heshima yangu nitajizuia kutokumuharibu yeye.
10 Tazama, nimekusafisha, ingawa si kama fedha, nimekujaribu katika tanuru ya mateso.
Tazama, Mimi niliwaandaa ninyi, lakini sio kama fedha; Nimekusafisha wewe katika tanuru la mateso.
11 Kwa ajili yangu mwenyewe, kwa ajili yangu mwenyewe, nafanya hili. Jinsi gani niliache Jina langu lichafuliwe? Sitautoa utukufu wangu kwa mwingine.
Kwa niaba yangu, kwa niaba yangu nitafanya; maana ni kwa jinsi gani niruhusu jina langu lisiheshimike? Sitampa utukufu wangu mtu yeyote.
12 “Ee Yakobo, nisikilize mimi, Israeli, ambaye nimekuita: Mimi ndiye; mimi ndimi mwanzo na mwisho.
Nisikilize mimi, Yakobo, na Israeli niliyekuita: Mimi ndiye; Mimi ni wa kwanza, na pia wa mwisho.
13 Mkono wangu mwenyewe uliweka misingi ya dunia, nao mkono wangu wa kuume umezitanda mbingu; niziitapo, zote husimama pamoja.
Ndio, mkono wangu umeweka msingi wa nchi, na mkono wangu wa kuume ulizitawanya mbingu, zimesimama juu kwa pamoja.
14 “Kusanyikeni, ninyi nyote, msikilize: Ni ipi miongoni mwa hizo sanamu ambayo imetabiri vitu hivi? Watu wa Bwana waliochaguliwa na kuungana watatimiza kusudi lake dhidi ya Babeli; mkono wa Mungu utakuwa dhidi ya Wakaldayo.
Jikusanyeni wenyewe, nyinyi nyote, na sikilizeni; ni nani miongoni mwenu atangazaye mambo haya? Yahwe atakamilisha lengo lake dhidi ya Babeli. Atachukua mapenzi ya Yahwe dhidi ya wa Wakaldayo.
15 Mimi, naam, Mimi, nimenena; naam, nimemwita yeye. Nitamleta, naye atafanikiwa katika lile nililomtuma.
Mimi, nimezungumza, ndio, nimemchagua yeye, nimemleta yeye, na yeye atafanikiwa.
16 “Nikaribieni na msikilize hili: “Tangu tangazo la kwanza sikusema kwa siri; wakati litokeapo, nitakuwako hapo.” Sasa Bwana Mwenyezi amenituma, kwa Roho wake.
Sogea karibu na mimi, sikiliza hili; kutoka mwanzo sikuzungumza katika siri; lakini ilipotokea, Mimi niko hapa; na sasa Bwana Mungu amenituma mimi, na Roho wake.''
17 Hili ndilo asemalo Bwana, Mkombozi wako, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli: “Mimi ni Bwana, Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye katika njia ikupasayo kuiendea.
Yahwe asema hivi, Mkombozi wenu, Mtakatifu wa Israeli anasema, ''Mimi ni Yahwe Mungu wenu, ninayewafundisha juu ya kufanikiwa, ninayewaonyesha njia mtakayoiptia.
18 Laiti ungesikiliza kwa makini maagizo yangu, amani yako ingekuwa kama mto, haki yako kama mawimbi ya bahari.
Ikiwa kama mtaheshimu amri zangu! Hivyo amani na maendeleo yatatiririka kama mto, na wokovu wenu ni kama mawimbi kwenye bahari.
19 Wazao wako wangekuwa kama mchanga, watoto wako kama chembe zake zisizohesabika; kamwe jina lao lisingefutiliwa mbali, wala kuangamizwa kutoka mbele zangu.”
Watoto wako watakuwa wengi kama mchanga, na watoto kutoka kwenye tombo zenu watakuwa wengi kama nafaka kwenye mchanga; majina yao hayataondolewa wala kufutwa mbele yangu.
20 Tokeni huko Babeli, kimbieni kutoka kwa Wakaldayo! Tangazeni hili kwa kelele za shangwe na kulihubiri. Lipelekeni mpaka miisho ya dunia; semeni, “Bwana amemkomboa mtumishi wake Yakobo.”
Tokeni nje ya Babeli! wakimbieni Wakaldayo! kwa sauti ya kupiga kelele tangaza kwamba! hakikisha hili linajulikana, hakikisha hili linafika mpaka miisho ya nchi! sema 'Yahwe amemkomboa Yakobo mtumishi wake.
21 Hawakuona kiu alipowaongoza kupita jangwani; alifanya maji yatiririke kutoka kwenye mwamba kwa ajili yao; akapasua mwamba na maji yakatoka kwa nguvu.
Hawakupatwa na kiu alipowaongoza katika jangwa, alifanya maji kutokea kwenye mwamba kwa ajili yao; aliugawa na kufungua mwamba, na maji yakatoka nje.
22 “Hakuna amani kwa waovu,” asema Bwana.
Hakuna amani kwa watenda makosa- amesema Yahwe.''

< Isaya 48 >