< Isaya 46 >

1 Beli anasujudu hadi nchi, Nebo anainama; sanamu zao zabebwa na wanyama wa mizigo. Vinyago hivi mnavyobeba kila mahali ni mzigo wa kulemea, mzigo kwa waliochoka.
Beli huaguka chini, Nebo husujudu; miungu yao imebebwa na wanyama na mzigo wa mnyama. Sanamu hizi mlizobeba ni mzigo mzito kwa wanyama kuchoka.
2 Vinyago pamoja na wale wanaovibeba wanainama chini; hiyo miungu haiwezi kuwaokoa watu, wote wanakwenda utumwani pamoja.
Kwa pamoja wanashuka chini; hawawezi kuziokoa sanamu zao, na wao wenyewe wameenda uhamishoni.
3 “Nisikilizeni mimi, ee nyumba ya Yakobo, ninyi nyote mliobaki wa nyumba ya Israeli, ninyi ambao nimewategemeza tangu mlipotungwa mimba, nami nimewabeba tangu kuzaliwa kwenu.
Nisikilizeni mimi, nyumba ya Yakobo, wote mliobaki kwenye nyumba ya Israeli mliochukuliwa na mimi kutoka kabla amjazaliwa, mlichukuliwa mkiwa tumboni.
4 Hata mpaka wakati wa uzee wenu na mvi, Mimi ndiye, Mimi ndiye nitakayewasaidia ninyi. Nimewahuluku, nami nitawabeba, nitawasaidia ninyi na kuwaokoa.
Hata kwa njie wazee Mimi ndiye, mpaka mmeshapata mvi nitawachukua. Nimewaumba ninyi na nitawabeba ninyi; Nitwachukua nyie na nitawakomboa nyie.
5 “Mtanilinganisha na nani, au mtanihesabu kuwa sawa na nani? Ni nani mtakayenifananisha naye ili tuweze kulinganishwa?
Je utanifananisha mimi na nani? na mimi nimefanana na nani, ili utulinganishe?
6 Wengine humwaga dhahabu kutoka kwenye mifuko yao, na kupima fedha kwenye mizani; huajiri mfua dhahabu kutengeneza mungu, kisha huisujudia na kuiabudu.
Watu humwaga dhahabu kutoka kwenye mabegi yao na uzito wa fedha kwenye uzani. Humuajiri mfua dhahabu, na hutengeneza kuwa dhahabu; na huinama chini na kuzisuju.
7 Huiinua mabegani na kuichukua; huiweka mahali pake, papo hapo ndipo isimamapo. Wala haiwezi kusogea kutoka mahali pale. Ingawa mtu huililia, haimjibu; haiwezi kumwokoa kwenye taabu zake.
Wanazinyanyua juu ya mabega yao na kuzibeba; wanaziweka katika sehemu yake, na itasimama katika eneo lake na alitasogea kutoka pale, hulilia, lakini haiwezi kujibu wala kumuokoa yeyote kwenye matatizo.
8 “Kumbukeni hili, litieni akilini, liwekeni moyoni, enyi waasi.
Tafakari kuhusu hivi vitu; katu usivipuuzie, enyi waasi!
9 Kumbukeni mambo yaliyopita, yale ya zamani za kale; mimi ndimi Mungu, wala hakuna mwingine; mimi ndimi Mungu, wala hakuna mwingine aliye kama mimi.
Tafakari kuhusu vitu vya awali, nyakati zile zilizopita, Maana mimi ni Mungu, na hakuna mwingine, Mimi ni Mungu na hakuna kama mimi.
10 Ni mimi nitangazaye mwisho tangu mwanzo, naam, tangu zamani za kale, mambo ambayo hayajatendeka. Ninasema: Kusudi langu ndilo litakalosimama, nami nitatenda mapenzi yangu yote.
Mimi ninatangaza mwisho kutoka mwanzo, na kabla ya kitu ambacho hakijatokea; Ninasema, ''Mpango wangu utatokea na nitafanya kama ninavyotamani.''
11 Kutoka mashariki ninaita ndege awindaye; kutoka nchi ya mbali, mtu atakayetimiza kusudi langu. Lile ambalo nimelisema, ndilo nitakalolitimiza; lile nililolipanga, ndilo nitakalolitenda.
Nitamuita ndege wa mawindo kutoka mashariki, Mtu ambaye ni chaguo langu kutoka nchi ya mbali; Ndio nimesema; na pia nitayatimiza haya, nimekusudia, na pia nitafanya hivyo.
12 Nisikilizeni, ninyi wenye mioyo migumu, ninyi mlio mbali na haki.
Nisikilize mimi, enyi watu makaidi, ambao mko mbali na kutenda mema.
13 Ninaleta haki yangu karibu, haiko mbali; wala wokovu wangu hautachelewa. Nitawapa Sayuni wokovu, Israeli utukufu wangu.
Ninaileta haki yangu karibu; na wala sio mbali, na wokovu wangu hausubiri; na nitatoa wokovu wangu kwa Sayuni na uzuri wangu kwa Israeli.

< Isaya 46 >