< Isaya 45 >
1 “Hili ndilo asemalo Bwana kwa mpakwa mafuta wake, Koreshi, ambaye nimemshika mkono wake wa kuume kutiisha mataifa mbele yake na kuwavua wafalme silaha zao, kufungua milango mbele yake ili malango yasije yakafungwa:
Yahwe asema hivi kwa mapakwa mafuta, kwa Koreshi, niliyemshika kwa mkono wa kuume, illi niweze kuangamiza mataifa mbele yake, kuwalinda wafalme, kufunguo milango mbele yao, ili lango liwe wazi:
2 Nitakwenda mbele yako na kusawazisha milima; nitavunjavunja malango ya shaba na kukatakata mapingo ya chuma.
''Nitakwenda mbele yako na kusawazisha milima; nitavunjavunja vipandevivande milango ya shaba na kukuta vipandevipande nguzo za chuma,
3 Nitakupa hazina za gizani, mali zilizofichwa mahali pa siri, ili upate kujua ya kwamba Mimi ndimi Bwana, Mungu wa Israeli, akuitaye kwa jina lako.
Nitakupa hazina iliyo gizani na utajiri uliofichwa mbali, ili ujue kwamba ni mimi Yahwe, niliyekuita kwa jina lako, Mimi, Mungu wa Israeli.
4 Kwa ajili ya Yakobo mtumishi wangu, Israeli niliyemchagua, nimekuita wewe kwa jina lako, na kukupa jina la heshima, ingawa wewe hunitambui.
Kwa niaba ya Jakobo mtumishi wangu, na Israeli chaguo langu, Nimekuita wewe kwa jina lako: nimekupa heshima iliyotukuka, jabo hakunijua mimi.
5 Mimi ndimi Bwana, wala hakuna mwingine, zaidi yangu hakuna Mungu. Nitakutia nguvu, ingawa wewe hujanitambua,
Mimi ni Yahwe na hapana mwingine; hakuna Mungu ila mimi. Nitakuimarisha katika vita, japo hamkunifamu mimi;
6 ili kutoka mawio ya jua mpaka machweo yake, watu wapate kujua kwamba hakuna Mungu mwingine ila Mimi. Mimi ndimi Bwana wala hakuna mwingine.
kwamba watu wajue kutoka mapambazuko ya jua, na kutoka magharibi, kwamba hakuna mungu mwngine ila mimi: Mimi ni Yahwe, na hakuna mwingine.
7 Mimi ninaumba nuru na kuhuluku giza, ninaleta mafanikio na kusababisha maafa. Mimi, Bwana, huyatenda haya yote.
Nimefanya mwanga na nimeumba giza; Ninanateta amani na ninaumba majanga; Mimi Yahwe, nifanyae haya yote.
8 “Enyi mbingu juu, nyesheni haki, mawingu na yaidondoshe. Dunia na ifunguke sana, wokovu na uchipuke, haki na ikue pamoja nao. Mimi, Bwana, ndiye niliyeiumba.
Enyi mbingu, nyesha kutoka juu! Acha anga lishushe chini haki, na acha nchi inyonje haki, ili wokovu uweze kuchipukia juu, na haki kutawanyika kwa pamoja. Mimi Yahwe nimewumba wote kwa pamoja.
9 “Ole wake yeye ashindanaye na Muumba wake, yeye ambaye ni kigae tu kati ya vigae juu ya ardhi. Je, udongo wa kufinyangia humwambia mfinyanzi, ‘Unatengeneza nini wewe?’ Je, kazi yako husema, ‘Hana mikono’?
Ole kwa yeyote anayesema kwa yule aliyemfanya yeye, kwake yeye ni kama chungu cha udongo miongoni mwa vyingu vya udongo katika aridhi! Je udongo umwambia mfinyanzi, 'Unatengeneza nini? au ' Kazi yako haina kitu cha kushika?
10 Ole wake amwambiaye baba yake, ‘Umezaa nini?’ Au kumwambia mama yake, ‘Umezaa kitu gani?’
Ole wake asemae kwa baba, 'Unanizaa nini? au kwa mwanamke, 'unanizaa mimi nin?'
11 “Hili ndilo asemalo Bwana, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli na Muumba wake: Kuhusu mambo yatakayokuja, je, unaniuliza habari za watoto wangu, au kunipa amri kuhusu kazi za mikono yangu?
Yahwe asema hivi, yeye aliye Mtakatifu wa Israeli, muumbaji wake: 'Kwa nini unauliza swali kuhusu nini nitakacho kifanya kwa watoto wangu? Je unaweza kuniambia kuuhusiana na kazi ya mikono yangu?
12 Mimi ndiye niliyeumba dunia na kumuumba mwanadamu juu yake. Mikono yangu mwenyewe ndiyo iliyozitanda mbingu, nikayapanga majeshi yake yote ya angani.
Nimeifanya nchi na kuumba mtu juu yake. Ni mkono yangu mimi nilioinyoosha ju ya mbingu, na nikazimuru nyota zote kutokea.
13 Mimi nitamwinua Koreshi katika haki yangu: nitazinyoosha njia zake zote. Yeye atajenga mji wangu upya, na kuwaweka huru watu wangu walio uhamishoni, lakini si kwa kulipiwa fedha wala kupewa zawadi, asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.”
Nimemuinua Keroshi juu katika haki yangu, na nitalainisha njia zake zote. Ataujenga mji wangu kwa upya; atawachia walioko uhamishoni kurudi nyumbani kwao, na so kwa pesa wala kwa rushwa,'' asema Yahwe wa majeshi.
14 Hili ndilo asemalo Bwana: “Mazao ya Misri na bidhaa za Kushi, nao wale Waseba warefu, watakujia na kuwa wako, watakujia wakijikokota nyuma yako, watakujia wamefungwa minyororo. Watasujudu mbele yako wakikusihi na kusema, ‘Hakika Mungu yu pamoja nawe, wala hakuna mwingine; hakuna Mungu mwingine.’”
Yahwe asema hivi, mapato ya Misri na bidhaa ya Ethiopia pamoja na Waseba jamii ya watu werefu, tatawaleta kwenu. Watakuwa wa kwenu. Watafuata baada yenu, watakuja na minyororo. Watakuinamia chini na kukuomba huku wakisema, 'Hakika Mungu yuko pamoja na wewe na hakuna mwingine ila yeye.''
15 Hakika wewe u Mungu unayejificha, Ee Mungu na Mwokozi wa Israeli.
Hakika mna Mungu aliyejifisha ndani yenu, Mungu wa Israeli, Mkombozi.
16 Wote watengenezao sanamu wataaibika na kutahayarika; wataenda kutahayarika pamoja.
Wote wataabishwa na kuzaraliwa kwa pamoja; wale wachongao sanamu watatembea katika udhalilishaji.
17 Lakini Israeli ataokolewa na Bwana kwa wokovu wa milele; kamwe hutaaibika wala kutatahayarika, milele yote.
Lakini Israeli itakombolewa na Yahwe kawa wokovu wa milele; na wala hautaabika tena au kudhalilishwa.
18 Kwa kuwa hili ndilo asemalo Bwana, yeye aliyeumba mbingu, ndiye Mungu; yeye aliyeifanya dunia na kuiumba, yeye ndiye aliiwekea misingi imara, hakuiumba ili iwe tupu, bali aliiumba ikaliwe na viumbe vyake. Anasema: “Mimi ndimi Bwana, wala hakuna mwingine.
Yahwe asem hivi, nani aliyeziumba mbingu, Mungu wa kweli ndiye aliyeiumbwa nchi na kuifaya, ndiye aliyeianzisha nchi. Aliiumba yeye, sio kama taka, aliimba ili pawe na wenyeji: ''mimi ni Yahwe, na hakuna mwingine.
19 Sijasema sirini, kutoka mahali fulani katika nchi ya giza; sijawaambia wazao wa Yakobo, ‘Nitafuteni bure.’ Mimi, Bwana, nasema kweli; ninatangaza lililo sahihi.
Sijaongea katika siri, katika maeneo ya siri; Sijauambia ukoo wa Daudi, 'Nitafute bure! Mimi ni Yahwe ninayezungumza ukweli; Ninatangaza vitu vilivyo vya kweli.
20 “Kusanyikeni pamoja mje, enyi wakimbizi kutoka mataifa. Wale wabebao sanamu za mti ni watu wasio na akili, wale waombao miungu isiyoweza kuokoa.
Jikusanjeni wenyewe na mje! kusanyikeni kwa pamoja, enyi wakimbizi kutoka miongoni mwa mataifa! Hawana maarifa, wale wanaobeba sanamu ya kuchonga na kuiomba miungu asiyewasidia.
21 Tangazeni litakalokuwepo, lisemeni hilo, wao na wafanye shauri pamoja. Ni nani aliyetangulia kusema hili tangu zamani, aliyetangaza tangu zamani za kale? Je, haikuwa Mimi, Bwana? Wala hapana Mungu mwingine zaidi yangu mimi, Mungu mwenye haki na Mwokozi; hapana mwingine ila mimi.
Sogeeni karibu na mnitangazie mimi, leteni ushahidi! waache walete mashauri kwa pamoja. Ni nani aliyewaonyesha haya kutoka zamani? Ni nani aliyetangaza? Je sikuwa mimi, Yahwe? na hakuna Mungu mwingine ila mimi, Mungu mwenye haki; na mkombozi; hakuna mwingine zaidi yake.
22 “Nigeukieni mimi, nanyi mkaokolewe, enyi miisho yote ya dunia; kwa maana mimi ndimi Mungu, wala hapana mwingine.
Nijeukieni mimi, na mkaokolewe, miisho yote ya nchi; Maana mimi ni Mungu, na hakuna mwingine. Mimi mwenyewe ninaapa, ninaongea katika haki yangu, na sitarudi nyuma:
23 Nimeapa kwa nafsi yangu, kinywa changu kimenena katika uadilifu wote neno ambalo halitatanguka: Kila goti litapigwa mbele zangu, kwangu mimi kila ulimi utaapa.
'kwangu kila goti litapigwa, na kila ulimi utakiri.
24 Watasema kuhusu mimi, ‘Katika Bwana peke yake ndiko kuna haki na nguvu.’” Wote ambao wamemkasirikia Mungu watamjia yeye, nao watatahayarika.
Wataniambia mimi, Ni katika Yahwe peke yake kuna wokovu na nguvu.'' wataaibika wale wote wenye hasira na Mungu.
25 Lakini katika Bwana wazao wote wa Israeli wataonekana wenye haki na watashangilia.
Katika Yahwe makabila yote ya Israeli yataalalishwa; watachukua kiburi katika yeye.