< Isaya 44 >

1 “Lakini sasa sikiliza, ee Yakobo, mtumishi wangu, Israeli, niliyemchagua.
Sasa, sikiliza, Yakobo mtumishi wangu, na Isreli, Niliyekuchagua:
2 Hili ndilo asemalo Bwana, yeye aliyekuhuluku, aliyekuumba tumboni, yeye atakayekusaidia: Usiogope, ee Yakobo, mtumishi wangu, Yeshuruni, niliyekuchagua.
Yahwe asema hivi, yeye aliyekufanya na kukuumba wewe katika tumbo na yeye aliye kusadia wewe: Usiogope, Yakobo mtumishi wangu; na wewe Yeshuruni, niliyekuchagua.
3 Kwa maana nitamimina maji juu ya nchi yenye kiu, na vijito vya maji juu ya ardhi iliyokauka; nitamimina Roho wangu juu ya watoto wako, nayo baraka yangu juu ya wazao wako.
Maana nitashusha mvua kwenye aridhi yenye kiu, na mikondo ya maji kwenye ardhi kavu; Nitashusha roho yangu kwa watoto wako, na baraka zangu kwa watoto wako.
4 Nao watachipua kama manyasi katika shamba la majani, kama mierezi kando ya vijito vya maji yatiririkayo.
Watakuwa miongoni mwa nyasi, kama mti pembeni ya mkondo wa maji.
5 Mmoja atasema, ‘Mimi ni wa Bwana’; mwingine atajiita kwa jina la Yakobo; vilevile mwingine ataandika juu ya mkono wake, ‘Wa Bwana,’ na kujiita kwa jina la Israeli.
Mmoja atasema, 'Mimi ni wa Yahwe; na mwingine ataita jina la Yakobo, na mwingine ataandika kwenye mkono wake 'Mimi ni wa Yahwe, na kujiita mwenyewe kwa jina la Israeli.''
6 “Hili ndilo asemalo Bwana, Mfalme wa Israeli na Mkombozi, Bwana Mwenye Nguvu Zote: Mimi ni wa kwanza na Mimi ni wa mwisho; zaidi yangu hakuna Mungu.
Yahwe asema hivi—Mfalme wa Israeli na Mkombozi wake, Yahwe wa majeshi: ''Mimi ni mwanzo na ni mwisho; na hakuna mungu ila mimi.
7 Ni nani basi aliye kama mimi? Yeye na atangaze. Yeye atangaze na kuweka mbele yangu ni kitu gani kilichotokea tangu nilipoumba watu wangu wa kale, tena ni nini kitakachotokea: naam, yeye na atoe unabii ni nini kitakachokuja.
Ni nani aliye kama mimi? Na atangaze na anielezee matukio yaliyotokea tangu nilipoanzisha watu wangu wa kale, na waache watangaze matukio yajayo.
8 Msitetemeke, msiogope. Je, sikutangaza hili, na kutoa unabii tangu zamani? Ninyi ni mashahidi wangu. Je, yuko Mungu zaidi yangu mimi? Hasha, hakuna Mwamba mwingine; mimi simjui mwingine.”
Usiogope wala usifadhaike. Je si mimi niliyekutangazia toka zamani, na nikatangaza? ninyi ni mashaidi wangu: Je kuna Mungu mwingine zaidi yangu? Hakuna Mwamba mwingine zaidi yangu; Ninajua hakuna.''
9 Wote wachongao sanamu ni ubatili, navyo vitu wanavyovithamini havifai kitu. Wale ambao wanazitetea ni vipofu, ni wajinga, nao waaibika.
Mitindo yote ya sanamu si kitu; vitu wanavyo vifurahia ndani havina maana; mashahidi wake hawawezi kuona au kujua chochote, na watapatwa katika aibu.
10 Ni nani atengenezaye mungu na kusubu sanamu, ambayo haiwezi kumfaidia kitu chochote?
Ni nani atengenezae miungu au sanamu zisizo na maana?
11 Yeye pamoja na wenziwe wa aina yake wataaibishwa, mafundi wao si kitu ila ni wanadamu tu. Wote wakusanyike pamoja na kuwa na msimamo wao, watashushwa chini kwa hofu na kwa fedheha.
Tazama, washirika wote watapatwa na aibu; mafundi ni watu tu. waache washikilie msimamao wao kwa pamoja; wataogopa na kuhaibishwa.
12 Muhunzi huchukua kifaa na kukifanyia kazi kwenye makaa ya moto, hutengeneza sanamu kwa nyundo, huifanyiza kwa nguvu za mkono wake. Huona njaa na kupoteza nguvu zake, asipokunywa maji huzimia.
Mhunzi anafanya kazi kwa vyombo vyake, kutengeneza, kufanya kazi kwenye makaa ya mawe. Hurekebisha kwa kutumia nyundo na hufanya kazi kwa mkono wake wenye nguvu. Hupata njaa, na nguvu zake humuishia; Hajanywa maji na huzimia.
13 Seremala hupima kwa kutumia kamba na huuchora mstari kwa kalamu; huchonga kwa patasi na kutia alama kwa bikari. Huifanyiza katika umbo la binadamu, la mwanadamu katika utukufu wake wote, ili iweze kukaa katika sehemu yake ya ibada ya miungu.
Seremala hupima mbao kwa kamba na kuiweka alama kwa kitu kikali. Huichonga kwa vyombo vyake na kuweka alama kwa kutumia dira. Huichonga baada ya sanamu ya mtu, kama mtu anyevutia, ili iweze kukaa ndani ya nyumba.
14 Hukata miti ya mierezi, huchukua mtiriza au mwaloni. Huuacha ukue miongoni mwa miti ya msituni, au hupanda msunobari, nayo mvua huufanya ukue.
Huikata chini mierezi, huchagua miti ya miseprasi au miti ya mialoni. Huchukua mti yeye mwenyewe katika msitu. huotesha mvinje na mvua huifanya ikue.
15 Ni kuni ya binadamu: yeye huchukua baadhi yake na kuota moto, huwasha moto na kuoka mkate. Lakini pia huutumia kumtengeneza mungu na akamwabudu, huitengeneza sanamu na kuisujudia.
Basi mtu hutumia kwa moto na kujipatia joto. Ndio, huwasha moto kuwooka mkate. Halafu hutengeneza miungu ili ausujudie;
16 Sehemu ya kuni huziweka motoni, akapikia chakula chake, hubanika nyama na kula hadi ashibe. Huota moto na kusema, “Aha! Ninahisi joto, ninaona moto.”
Huchoma sehemu ya kuni kwa moto, na huchoma nyama yake juu yake. hula na kushiba. huota moto na kusema, ''Ah, Nimepata joto, nimeouna moto.''
17 Mabaki yake hutengeneza mungu, sanamu yake; yeye huisujudia na kuiabudu. Huiomba na kusema, “Niokoe; wewe ni mungu wangu.”
Kwa kutumia mbao hutengeneza miungu, sanamu yake; huisujudu na kuhieshimu, huipa sifa na kusema, ''Niokoe mimi, maana wewe ni mungu wangu.''
18 Hawajui chochote, hawaelewi chochote, macho yao yamefungwa hata hawawezi kuona, akili zao zimefungwa hata hawawezi kufahamu.
Hawajui, wala hawaelewi, maana macho yao yamepofuka na hawaoni, na mioyo yao haiwezi kufahamu.
19 Hakuna anayefikiri, hakuna mwenye maarifa wala ufahamu wa kusema, “Sehemu yake nilitumia kwa kuni; hata pia nilioka mkate juu ya makaa yake, nikabanika nyama na kuila. Je, nifanye machukizo kwa kile kilichobaki? Je, nisujudie gogo la mti?”
Hakuna anayefikiria, wala kuelewa na kusema, ''Nimechoma sehemu ya mbao kwenye moto; na pia nimewooka mkate kwa kutumia makaa yake. Nimechoma nyama kwa makaa yake nikala. Sasa Je ninaweza kutengeneza kitu kinachochukiza kwa ajili ya kuabudia kwa sehemu ya mbao iliyobakia? Je ninaweza kusujudia sanamu ya mbao?''
20 Hujilisha kwa majivu, moyo uliodanganyika humpotosha; hawezi kujiokoa mwenyewe, au kusema, “Je, kitu hiki kilichoko katika mkono wangu wa kuume si ni uongo?”
Ni kama anayejilisha majivu; moyo wke mdanganyifu unampoteza yeye. Huwezi kujiokoa mwenyewe, wala hawezi kusema, ''Hiki kitu katika mkono wangu wa kulia sio mungu wa kweli.''
21 “Ee Yakobo, kumbuka mambo haya, ee Israeli, kwa kuwa wewe ni mtumishi wangu. Nimekuumba wewe, wewe ni mtumishi wangu. Ee Israeli, sitakusahau.
Fikiria kuhusu vitu hivi, Yakobo na Israeli, maana wewe ni mtumishi wangu: Nimekuumba wewe; wewe ni mtumishi wangu:
22 Nimeyafuta makosa yako kama wingu, dhambi zako kama ukungu wa asubuhi. Nirudie mimi, kwa kuwa nimekukomboa wewe.”
Nimeyafuta makosa yako, kama wingu zito, matendo yako mabaya, na wingu, ni kama dhambi zako; maana nimekukomboa wewe.
23 Enyi mbingu, imbeni kwa furaha, kwa maana Bwana amefanya jambo hili. Ee vilindi vya dunia, piga kelele. Enyi milima, pazeni sauti kwa nyimbo, enyi misitu na miti yenu yote, kwa maana Bwana amemkomboa Yakobo, ameuonyesha utukufu wake katika Israeli.
Imba, enyi mbingu, maana Yahwe ameyafanya haya; piga kelele enyi mkaao katika nchi. Pazeni sauti enyi mlima milima, enyi misitu yenye miti ndani yake, ewe mlima, ewe msitu wenye kila aina ya mti ndani yak; Maana Yahwe amemkomboa Yakobo, na nitakuonyesha utukufu wake katika Israeli.
24 “Hili ndilo asemalo Bwana, Mkombozi wako, aliyekuumba tumboni: “Mimi ni Bwana, niliyeumba vitu vyote, niliyezitanda mbingu peke yangu, niliyeitandaza nchi mwenyewe,
Yahwe asema hivi, Mkombozi wako, yeye aliyekuumba wewe kutoka tumboni: ''Mimi ni Yahwe, niliyefanya kila kitu, mimi mwenyewe nizinyooshae mbigu, mimi peke niitngenezae nchi.
25 “mimi huzipinga ishara za manabii wa uongo, na kuwatia upumbavu waaguzi, niyapinduaye maarifa ya wenye hekima, na kuyafanya kuwa upuzi,
Mimi niliyezikata dalili za waongo na kuwaabisha wanaosoma dalili zake; Mimi niliyezigeuza busara za wenye hekima na kujeuza ushauri wao kuwa ujinga.
26 niyathibitishaye maneno ya watumishi wake, na kutimiza utabiri wa wajumbe wake, “niambiaye Yerusalemu, ‘Itakaliwa na watu,’ niambiaye miji ya Yuda kuwa, ‘Itajengwa,’ na kuhusu magofu yake, ‘Mimi nitayatengeneza,’
Mimi, Yahwe, niliyethibitisha maneno ya mtumishi wake na kuutimiza utabiri wa mjumbe wake. Aliyezungumza kuhusu Yerusalemu, 'Atakuwa mwenyeji; na katika mji wa Yuda, 'Watatengeneza tena, na nitapatengeneza palipoharibika;
27 niambiaye kilindi cha maji, ‘Kauka, nami nitakausha vijito vyako,’
awezae kusema kwa bahari kubwa, 'Kauka,' na yanakauka mda huo.'
28 nisemaye kuhusu Koreshi, ‘Yeye ni mchungaji wangu, naye atatimiza yote yanipendezayo; atauambia Yerusalemu, “Ukajengwe tena,” na kuhusu Hekalu, “Misingi yake na iwekwe.”’
Yahwe ndiye amwambiye Koreshi, 'Ni mchungaji wangu, atafanya kila nilitakalo; atatoa amri kuhusu Yerusalemu, 'Utajengwa kwa upya, 'na kuhusu Hekalu, 'Basi na msingi wake uanzwe kuwekwa.''

< Isaya 44 >