< Isaya 4 >

1 Katika siku ile wanawake saba watamshika mwanaume mmoja wakisema, “Tutakula chakula chetu wenyewe na kuvaa nguo zetu wenyewe, ila wewe uturuhusu tu tuitwe kwa jina lako. Utuondolee aibu yetu!”
Siku hiyo wanawake saba watamchukua mwanaume mmoja na kusema, ''Tutakula chakula chetu wenyewe, tutavaa nguo zetu wenyewe. lakini tunahitaji kuchukua jina lako ili tuondoe haibu zetu.''
2 Katika siku ile Tawi la Bwana litakuwa zuri na lenye utukufu, nalo tunda la nchi litakuwa fahari na utukufu wa wale Waisraeli watakaonusurika.
Na siku hiyo tawi zuri la Yahwe na utukufu, na matunda yatakuwa na ladha nzuri na kupendeza kwa wale wanaoishi Israeli.
3 Wale watakaoachwa Sayuni, watakaobaki Yerusalemu, wataitwa watakatifu, wale wote ambao wameorodheshwa miongoni mwa walio hai huko Yerusalemu.
Itatokea kwa yule aliyeachwa Sayuni na wale waliobakia Yerusalemu wataitwa watakatifu, yeyeto aliyeandikwa chini anaishi Yerusalemu.
4 Bwana atausafisha uchafu wa wanawake wa Sayuni, atatakasa madoa ya damu kutoka Yerusalemu kwa Roho ya hukumu na Roho ya moto.
Hii itatokea pale ambapo Bwana atasafisha uchafu wa mabinti wa Sayuni, na atasafisha madoa ya damu kutoka kati ya Yerusalemu, kwa namna ya roho ya hukumu na roho ya kuungua na moto.
5 Kisha Bwana ataumba juu ya Mlima wote wa Sayuni, na juu ya wale wote wanaokusanyika hapo, wingu la moshi wakati wa mchana, na kungʼaa kwa miali ya moto wakati wa usiku, nako juu ya huo utukufu wote kutatanda kifuniko cha ulinzi.
Tena juu ya mlima wote wa Sayuni na mahali pakuksanyikia, Yahwe atafanya wingu na moshi kwa wakati wa mchana na moto unaong'a wakati wa usiku; na itakuwa dari juu ya utukufu wote.
6 Utakuwa sitara na kivuli kutokana na joto la mchana, na kuwa mahali pa kujificha kutokana na dhoruba na mvua.
kutakuwa na kivuli kwenye makazi wakati mchana kuzuia jua, na kimbilio na mfuniko kutoka kwenye mawimbi na mvua.

< Isaya 4 >