< Isaya 32 >

1 Tazama, mfalme atatawala kwa uadilifu na watawala watatawala kwa haki.
הן לצדק ימלך מלך ולשרים למשפט ישרו
2 Kila mtu atakuwa kama kivuli cha kujificha kutokana na upepo na kimbilio kutokana na dhoruba, kama vijito vya maji jangwani na kivuli cha mwamba mkubwa katika ardhi yenye kiu.
והיה איש כמחבא רוח וסתר זרם כפלגי מים בציון כצל סלע כבד בארץ עיפה
3 Ndipo macho ya wale wanaoona hayatafumbwa tena, nayo masikio ya wale wanaosikia yatasikiliza.
ולא תשעינה עיני ראים ואזני שמעים תקשבנה
4 Moyo wa mtu mwenye hamaki utafahamu na kuelewa, nao ulimi wenye kigugumizi utanena kwa ufasaha.
ולבב נמהרים יבין לדעת ולשון עלגים תמהר לדבר צחות
5 Mpumbavu hataitwa tena muungwana, wala mtu mbaya kabisa kupewa heshima ya juu.
לא יקרא עוד לנבל נדיב ולכילי לא יאמר שוע
6 Kwa kuwa mpumbavu hunena upumbavu, moyo wake hushughulika na uovu: Hutenda mambo yasiyo ya kumcha Mungu, na hueneza habari za makosa kuhusu Bwana; yeye huwaacha wenye njaa bila kitu, na wenye kiu huwanyima maji.
כי נבל נבלה ידבר ולבו יעשה און--לעשות חנף ולדבר אל יהוה תועה להריק נפש רעב ומשקה צמא יחסיר
7 Taratibu za mtu mbaya kabisa ni ovu, hufanya mipango miovu ili kumwangamiza maskini kwa uongo, hata wakati ambapo hoja za mhitaji ni za haki.
וכלי כליו רעים הוא זמות יעץ לחבל ענוים (עניים) באמרי שקר ובדבר אביון משפט
8 Lakini mtu muungwana hufanya mipango ya kiungwana, na kwa matendo ya kiungwana yeye hufanikiwa.
ונדיב נדיבות יעץ והוא על נדיבות יקום
9 Enyi wanawake wenye kuridhika sana, amkeni na mnisikilize. Enyi binti mnaojisikia kuwa salama, sikieni lile ninalotaka kuwaambia!
נשים שאננות--קמנה שמענה קולי בנות בטחות--האזנה אמרתי
10 Muda zaidi kidogo ya mwaka mmoja, ninyi mnaojisikia salama mtatetemeka, mavuno ya zabibu yatakoma na mavuno ya matunda hayatakuwepo.
ימים על שנה תרגזנה בטחות כי כלה בציר אסף בלי יבוא
11 Tetemekeni, enyi wanawake wenye kuridhika, tetemekeni kwa hofu, enyi binti mnaojisikia salama! Vueni nguo zenu, vaeni nguo ya gunia viunoni mwenu.
חרדו שאננות רגזה בטחות פשטה וערה וחגורה על חלצים
12 Pigeni matiti yenu kwa ajili ya mashamba mazuri, kwa ajili ya mizabibu iliyozaa vizuri
על שדים ספדים על שדי חמד על גפן פריה
13 na kwa ajili ya nchi ya watu wangu, nchi ambayo miiba na michongoma imemea: naam, ombolezeni kwa ajili ya nyumba zote za furaha na kwa ajili ya mji huu wenye kufanya sherehe.
על אדמת עמי קוץ שמיר תעלה כי על כל בתי משוש קריה עליזה
14 Ngome itaachwa, mji wenye kelele nyingi utahamwa, ngome ndani ya mji na mnara wa ulinzi vitakuwa ukiwa milele, mahali pazuri pa punda na malisho ya makundi ya kondoo,
כי ארמון נטש המון עיר עזב עפל ובחן היה בעד מערות עד עולם--משוש פראים מרעה עדרים
15 mpaka Roho amwagwe juu yetu kutoka juu, nalo jangwa kuwa shamba lenye rutuba, na shamba lenye rutuba kuwa kama msitu.
עד יערה עלינו רוח ממרום והיה מדבר לכרמל וכרמל (והכרמל) ליער יחשב
16 Haki itakaa katika jangwa, na uadilifu utakaa katika shamba lenye rutuba.
ושכן במדבר משפט וצדקה בכרמל תשב
17 Matunda ya haki yatakuwa amani, matokeo ya haki yatakuwa utulivu na matumaini milele.
והיה מעשה הצדקה שלום ועבדת הצדקה--השקט ובטח עד עולם
18 Watu wangu wataishi katika makao ya mahali pa amani, katika nyumba zilizo salama, katika mahali pa kupumzika pasipo na usumbufu.
וישב עמי בנוה שלום ובמשכנות מבטחים ובמנוחת שאננות
19 Hata kama mvua ya mawe iangushe msitu na mji ubomolewe kabisa,
וברד ברדת היער ובשפלה תשפל העיר
20 tazama jinsi utakavyobarikiwa, ukipanda mbegu yako katika kila kijito, na kuwaacha ngʼombe wako na punda wajilishe kwa uhuru.
אשריכם זרעי על כל מים משלחי רגל השור והחמור

< Isaya 32 >