< Isaya 31 >

1 Ole wao wale washukao Misri kwa ajili ya msaada, wale wategemeao farasi, wanaoweka tumaini katika wingi wa magari yao ya vita, na katika nguvu nyingi za wapanda farasi, lakini hawamwangalii yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli, wala hawatafuti msaada kwa Bwana.
Ole wao washukao Misri kuomba msaada na kutegemea farasi, kuweka imani katika magari (maana wako wengi) na ( maana faras haziesabiki). Lakini hawausiani na Mtakatifu wa Israeli, wala hawamtafuti Yahwe!
2 Hata hivyo yeye pia ana hekima na anaweza kuleta maafa, wala hayatangui maneno yake. Yeye atainuka dhidi ya nyumba ya mwovu, dhidi ya wale ambao huwasaidia watenda mabaya.
Lakini ni mwenye busara, na ataleta maafa na atakanusha maneno yake. Na atakuja juu ya nyumba zitendazo maovu, na dhidi ya wale wanaowasaidia kuteda dhambi.
3 Lakini Wamisri ni wanadamu, wala si Mungu, farasi wao ni nyama, wala si roho. Wakati Bwana atakaponyoosha Mkono wake, yeye anayesaidia atajikwaa, naye anayesaidiwa ataanguka, wote wawili wataangamia pamoja.
Misri ni mtu na sio Mungu, ni farasi wa mwili na sio wa roho. Yahwe atakapota nje kwa mkono wake, wote waliowasaidia watakuwa na mashaka, na yeyote atakayesidia atanguka; wote kwa pamoja watatoweka.
4 Hili ndilo Bwana analoniambia: “Kama vile simba angurumavyo, simba mkubwa juu ya mawindo yake: hata ingawa kundi lote la wachunga mifugo huitwa pamoja dhidi yake, hatiwi hofu na kelele zao wala kusumbuliwa na ghasia zao; ndivyo Bwana Mwenye Nguvu Zote atakavyoshuka kufanya vita juu ya Mlima Sayuni na juu ya vilele vyake.
Hivi ndivyo Yahwe alivyosema na mimi, '' kama simba, na hata mtoto wa simba, hunguruma juu ya mawindo yake, pale makundi ya wachungaji yanapoita dhidi yake, lakini hatatemeka kwa sauti zao, wala hatakwenda kwa sababu ya kelele zao, hivyo Yahwe wa majeshi atashuka kupigana kwenye mlima Sayuni, katika kilima hicho.
5 Kama ndege warukao, Bwana Mwenye Nguvu Zote ataukinga Yerusalemu; ataukinga na kuuokoa, atapita juu yake na kuufanya salama.”
Kama ndege apaavyo, hivyo Yahwe wa majeshi atailinda Yerusalemu; atailinda na kuiokoa kama apitavyo juu na kuilinda.
6 Mrudieni yeye ambaye nyumba ya Israeli imemwasi sana.
Mrudieni yeye kutoka huyo mliyemgeukia, watu wa Israeli.
7 Kwa kuwa katika siku ile kila mmoja wenu atazikataa sanamu za fedha na za dhahabu zilizotengenezwa kwa mikono yenu yenye dhambi.
Maana katika siku hiyo kila mmoja ataondoa miungu ya fedha na miungu ya dhahabu iliyotegenezwa kwa mikono yenu yenye dhambi.
8 “Ashuru itaanguka kwa upanga ambao si wa mwanadamu; upanga usio wa kibinadamu utawaangamiza. Watakimbia mbele ya upanga na vijana wao wa kiume watafanyizwa kazi kwa lazima.
Asiria atangamizwa kwa upanga; na upanga usioshikiwa na mtu utumaliza yeye. Ataukimbia upanga, na vijana wake wadogo watafanyishwa kazi ngumu.
9 Ngome zao zitaanguka kwa sababu ya hofu; kwa kuona bendera ya vita, majemadari wao watashikwa na hofu ya ghafula,” asema Bwana, ambaye moto wake uko Sayuni, nayo tanuru yake iko Yerusalemu.
Na watashindwa kujiani kwa sababu ya hofu, na mkuu wao ataogopa mbele ya bendera ya jeshi la Yahwe.''- Hili ni tamko la Yahwe, ambao moto uko Sayuni na ambayo sufuria ya moto iko Yerusalemu.

< Isaya 31 >