< Isaya 29 >

1 Ole wako, wewe Arieli, Arieli, mji alimokaa Daudi! Ongezeni mwaka kwa mwaka, na mzunguko wa sikukuu zenu uendelee.
Woe to Ariel, to Ariel, The city where David dwelt! Add year to year, Let the festivals go round,
2 Hata hivyo nitauzunguka Arieli kwa jeshi, utalia na kuomboleza, utakuwa kwangu kama mahali pa kuwashia moto madhabahuni.
Then will I distress Ariel; Mourning and sorrow shall be there; Yet shall she be to me as Ariel [[the lion of God]].
3 Nitapiga kambi pande zote dhidi yako, nitakuzunguka kwa minara na kupanga mazingirwa yangu dhidi yako.
I will encamp against thee round about, And I will lay siege against thee with a mound, And I will raise towers against thee.
4 Utakaposhushwa, utanena kutoka ardhini, utamumunya maneno yako kutoka mavumbini. Sauti yako itatoka katika nchi kama vile ya mzimu, utanongʼona maneno yako toka mavumbini.
Thou shalt be brought down, and speak from the ground, And thy speech shall be low from the dust; Thy voice shall be like that of a spirit under ground, And thy speech shall chirp as from the dust.
5 Lakini adui zako wengi watakuwa kama vumbi laini, kundi la wakatili watakuwa kama makapi yapeperushwayo. Naam, ghafula, mara moja,
Yet shall the multitude of thine enemies be like fine dust; The multitude of the terrible like flying chaff; It shall take place suddenly, in a moment.
6 Bwana Mwenye Nguvu Zote atakuja na ngurumo, tetemeko la ardhi, na kwa sauti kuu, atakuja na dhoruba, tufani na miali ya moto iteketezayo.
From Jehovah of hosts cometh the visitation With thunder, and earthquake, and great noise, With storm and tempest, And flames of devouring fire.
7 Kisha makundi ya mataifa yote yale yapiganayo dhidi ya Arieli, yale yanayomshambulia yeye na ngome zake, na kumzunguka kwa jeshi, watakuwa kama ilivyo ndoto, kama maono wakati wa usiku:
As a dream, a vision of the night, Shall be the multitude of all the nations That fight against Ariel, That fight against her and her fortress, And distress her.
8 kama vile mtu aliye na njaa aotavyo kuwa anakula, lakini huamka, bado njaa yake ingalipo, kama vile mtu mwenye kiu aotavyo kuwa anakunywa maji, lakini huamka akiwa anazimia, akiwa bado angali ana kiu. Hivyo ndivyo itakavyokuwa kwa makundi yote ya mataifa yanayopigana dhidi ya Mlima Sayuni.
As a hungry man dreameth, and lo! he eateth, But awaketh and is still hungry; And as a thirsty man dreameth, and lo! he drinketh, But awaketh, and lo! he is faint and thirsty; So shall it be with the multitude of all the nations That fight against mount Zion.
9 Duwaeni na kushangaa, jifanyeni vipofu wenyewe na msione, leweni, lakini si kwa mvinyo, pepesukeni lakini si kwa kileo.
Be in amazement and be amazed! Be blinded and be blind! They are drunk, but not with wine; They stagger, but not with strong drink!
10 Bwana amewaleteeni usingizi mzito: Ameziba macho yenu (ninyi manabii); amefunika vichwa vyenu (ninyi waonaji).
For Jehovah hath poured upon you a spirit of slumber; He hath closed your eyes, the prophets, And covered your heads, the seers;
11 Kwa maana kwenu ninyi, maono haya yote si kitu ila maneno yaliyotiwa lakiri katika kitabu. Kama mkimpa mtu yeyote awezaye kusoma kitabu hiki, nanyi mkamwambia, “Tafadhali kisome,” yeye atajibu, “Mimi siwezi, kwa kuwa kimetiwa lakiri.”
And so every vision is to you as the words of a sealed book, Which is given to a man that is skilled in writing, Saying, “Read this, I pray thee”; But he answereth, “I cannot, for it is sealed.”
12 Au kama mkimpa mtu yeyote kitabu hiki asiyeweza kusoma na kumwambia, “Tafadhali kisome,” atajibu, “Mimi sijui kusoma.”
Or, if he give it to one that is not skilled in writing, Saying, “Read this, I pray thee,” He answereth, “I am not skilled in writing.”
13 Bwana anasema: “Watu hawa hunikaribia kwa vinywa vyao na kuniheshimu kwa midomo yao, lakini mioyo yao iko mbali nami. Ibada yao kwangu inatokana na maagizo waliyofundishwa na wanadamu.
Therefore saith the Lord, Since this people draweth near to me with their mouth, And honoreth me with their lips, While their heart is far from me, And their worship of me is according to the commandments of men,
14 Kwa hiyo mara nyingine tena nitawashangaza watu hawa, kwa ajabu juu ya ajabu. Hekima ya wenye hekima itapotea, nayo akili ya wenye akili itatoweka.”
Therefore, behold, I will proceed to deal marvellously with this people; Marvellously and wonderfully, For the wisdom of their wise men shall perish, And the prudence of the prudent shall be hid.
15 Ole kwa wale wanaokwenda kwenye vilindi virefu kumficha Bwana mipango yao, wafanyao kazi zao gizani na kufikiri, “Ni nani anayetuona? Ni nani atakayejua?”
Woe to them that hide deep their purposes from Jehovah, Whose work is in darkness; That say, Who seeth us? Who knoweth us?
16 Mnapindua mambo juu chini, kana kwamba mfinyanzi aweza kufikiriwa kuwa kama udongo wa mfinyanzi! Je, kile kilichofinyangwa chaweza kumwambia yule aliyekifinyanga, “Wewe hukunifinyanga mimi?” Je, chungu kinaweza kumwambia mfinyanzi, “Wewe hujui chochote?”
Alas, your perverseness! Is the potter to be esteemed as the clay, That the work should say of its maker, He made me not? And the thing formed say of him that formed it, He hath no understanding?
17 Kwa muda mfupi sana, je, Lebanoni haitageuzwa kuwa shamba lenye rutuba, na shamba lenye rutuba liwe kama msitu?
Is it not yet a very little while, And Lebanon shall be changed to a fruitful field, And the fruitful field be esteemed a forest.
18 Katika siku ile viziwi watasikia maneno ya kitabu, na katika utusitusi na giza macho ya kipofu yataona.
And in that day shall the deaf hear the words of the book, And out of mist and darkness shall the eyes of the blind see.
19 Mara nyingine tena wanyenyekevu watafurahi katika Bwana, wahitaji watafurahi katika yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli.
The afflicted shall exceedingly rejoice in Jehovah, And the poor shall exult in the Holy One of Israel.
20 Wakatili watatoweka na wenye kudhihaki watatokomea, nao wote wenye jicho la uovu watakatiliwa mbali,
For the oppressor hath come to naught; the scoffer is destroyed; And all that watched for iniquity are cut off;
21 wale ambao kwa neno humfanya mtu kuwa mwenye hatia, wamtegeao mtego mtetezi katika mahakama, na kwa ushuhuda wa uongo humnyima haki yeye asiye na hatia.
Who condemned a man in his cause, And laid snares for him who defended himself in the gate, And with falsehood caused the righteous to fail.
22 Kwa hiyo hili ndilo Bwana, aliyemkomboa Abrahamu, analosema kwa nyumba ya Yakobo: “Yakobo hataaibishwa tena, wala nyuso zao hazitabadilika sura tena.
Therefore concerning the house of Jacob thus saith Jehovah, He that redeemed Abraham: No more shall Jacob be ashamed, And no more shall his face grow pale.
23 Wakati watakapoona watoto wao miongoni mwao, kazi ya mikono yangu, watalitakasa Jina langu takatifu; wataukubali utakatifu wa yeye Aliye Mtakatifu wa Yakobo, nao watamcha Mungu wa Israeli.
For when his children behold the work of my hands in the midst of them, They shall honor my name. They shall honor the Holy One of Jacob, And reverence the God of Israel.
24 Wale wanaopotoka rohoni watapata ufahamu, nao wale wanaolalamika watayakubali mafundisho.”
They that erred in spirit shall come to understanding, And the obstinate shall receive instruction.

< Isaya 29 >