< Isaya 25 >
1 Ee Bwana, wewe ni Mungu wangu, nitakutukuza na kulisifu jina lako, kwa maana katika ukamilifu wa uaminifu umetenda mambo ya ajabu, mambo yaliyokusudiwa tangu zamani.
Yahwe wewe ni Mungu wangu; nitakutukuza wewe, nitalisifu jina lako; maana umetenda matendo ya ajabu, mambo uliyoyapanga toka zamaini, kwa uaminifu na ukamilifu.
2 Umeufanya mji kuwa lundo la kifusi, mji wenye ngome kuwa magofu, ngome imara ya wageni kuwa si mji tena, wala hautajengwa tena kamwe.
Maana umeufanya mji kuwa chungu, ngome ya mji, uharibifu na ngome ya wageni kuwa si mji.
3 Kwa hiyo mataifa yenye nguvu yatakuheshimu, miji ya mataifa katili itakuheshimu wewe.
Hivyo basi watu wenye nguvu watakutukuza wewe; na mji waishio watu wasio na ukatili watakuogopa wewe.
4 Umekuwa kimbilio la watu maskini, kimbilio la mhitaji katika taabu yake, hifadhi wakati wa dhoruba na kivuli wakati wa hari. Kwa maana pumzi ya wakatili ni kama dhoruba ipigayo ukuta
Maana umekuwa katika eneo salama kwa aliye masikni, makazi kwa mhitaji ambaye yuko kwenye dhiki- makazi kwa aliyeko kwenye dhoruba na kivuli kwa aliyeko kwenye jua. Pale punzi ya watu wakatili imekuwa kama dhoruba dhidi ya ukuta,
5 na kama joto la jangwani. Wewe wanyamazisha makelele ya wageni; kama vile hari ipunguzwavyo na kivuli cha wingu, ndivyo wimbo wa wakatili unyamazishwavyo.
na jua kwenye aridhi kavu, na watazuia kelele za wageni, kama vile jua linavyozuiliwa na kivuli cha mawingu, hivyo basi nyimbo wasio na makosa zimejibiwa.
6 Juu ya mlima huu Bwana Mwenye Nguvu Zote ataandaa karamu ya vinono kwa mataifa yote, karamu ya mvinyo wa zamani, nyama nzuri sana na divai zilizo bora sana.
Katika mlima huu Yahwe wa majeshi atafanya kwa watu sikukuu ya ya vitu vilivyonona, na mvinyo uliochaguliwa, zabuni ya nyama na sikuku juu ya sira.
7 Juu ya mlima huu ataharibu sitara ihifadhiyo mataifa yote, kile kifuniko kifunikacho mataifa yote,
Na katika mlima huu atauharibu mfuniko uliowekwa juu watu wote, na mtandao wa kusuka juu ya mataifa.
8 yeye atameza mauti milele. Bwana Mwenyezi atafuta machozi katika nyuso zote; ataondoa aibu ya watu wake duniani kote. Bwana amesema hili.
Atameza kifo daima, na Bwana Yahwe atayafuta machozi katika nyuso zetu; na aibu ya watu wake itatupwa mbali kutoka duniani kote, maana Yahwe amesema hivyo.
9 Katika siku ile watasema, “Hakika huyu ndiye Mungu wetu; tulimtumaini, naye akatuokoa. Huyu ndiye Bwana, tuliyemtumaini; sisi tushangilie na kufurahia katika wokovu wake.”
Yatazungumzwa katika siku hiyo, ''Huyu ni Mungu wetu; na tunayemngoja, na atatuokoa. Huyu ni Yahwe; tuliyemngoja, tutafurahia na kushangilia wokovu wake.''
10 Mkono wa Bwana utatulia juu ya mlima huu, bali Moabu atakanyagwa chini kama majani makavu yakanyagwavyo kwenye shimo la mbolea.
Maana katika mlima huu mkono wa Bwana utashuka; na Moabu itakanyagwakangwa chini kwenye eneo lake, na hata majani yatakanyagwakanyagwa chini katika shimo lililojaa mbolea.
11 Watakunjua mikono yao katikati yake, kama vile mwogeleaji akunjuavyo mikono yake ili aogelee. Mungu atashusha kiburi chao licha ya ujanja wa mikono yao.
Wataitawnya mikono yao katikati yao, kama vile mpiga mbizi atawanyavyo mikono yake wakati akipiga mbizi. Lakini Bwana atashusha kiburi chao chini japo kuwa na ujuzi katika mikono yao.
12 Atabomoa kuta ndefu za maboma yako na kuziangusha chini, atazishusha chini ardhini, mpaka mavumbini kabisa.
Na ataiangusha chini kwenye aridhi kuta za ngome, kwenye mavumbi.