< Isaya 24 >

1 Tazama, Bwana ataifanya dunia kuwa ukiwa na kuiharibu, naye atauharibu uso wake na kutawanya wakaao ndani yake:
Angalia Yahwe anakaribia kuifanya dunia kuwa utupu, kuhiharibu, kuharibu uso wake, na kuwatawanya wenyeji wake.
2 ndivyo itakavyokuwa kwa makuhani na kwa watu, kwa bwana na kwa mtumishi, kwa bibi na kwa mtumishi wake wa kike, kwa muuzaji na kwa mnunuzi, kwa mkopaji na kwa mkopeshaji, kwa mdaiwa na kwa mdai.
Itakuwa kama ilivyo kwa watu itakuwa hivyo hivyo kwa kuhani; na kwa watumishi na kwa bwana wake, na kwa mfanyakazi wa ndani itakuwa hivyo na kwa tajiri yake, ndivyo itakavyokuwa kwa anayeuza na anayenunua; ndivyo itakavyokwa kwa wenye kupata faida na wenye madeni, na wale wennye kupokea faida itakuwa hivyo hivyo kwa wale wenye kutoa faida.
3 Dunia itaharibiwa kabisa na kutekwa nyara kabisa. Bwana amesema neno hili.
Dunia itaharibiwa kabisa na kufanjwa ukiwa; maana Yahwe amenena maneno hayo. Dunia imekauka kabisa na kunyauka,
4 Dunia inakauka na kunyauka, dunia inanyongʼonyea na kunyauka, waliotukuzwa wa dunia wananyongʼonyea.
Dunia inazimia n kudhohofika. Watu maarufu wa duniani watapotezwa.
5 Dunia imetiwa unajisi na watu wake; wameacha kutii sheria, wamevunja amri na kuvunja agano la milele.
Dunia inavutwa na watu wakao ndani yake kwa sababu wamepindisha sheria, wameibadili amri na wamevunja agano la milele.
6 Kwa hiyo laana inaiteketeza dunia, watu wake lazima waichukue hatia yao. Kwa hiyo wakazi wa dunia wameteketezwa, nao waliosalia ni wachache sana.
Hivyo basi laana inaitafuna nchi, na wenyeji wake wamekutwa na makosa. Wakaao duniani wanateketea, na watu wachache wameachwa.
7 Divai mpya inakauka na mzabibu unanyauka, watu wote wafurahishao wanalia kwa huzuni.
Divai mpya imekauka, mizabibu imenyauka, na mioyo yote iliyochangamka inaugua.
8 Furaha ya matoazi imekoma, kelele za wenye furaha zimekoma, shangwe za kinubi zimenyamaza.
Sauti ya furha ya kigoma inasimama, na kelele za wenye furaha zimekwisha, na furaha ya kinubi imesitishwa.
9 Hawanywi tena mvinyo pamoja na wimbo, kileo ni kichungu kwa wanywaji wake.
Hawatakunjwa mvinyo tena na kuimba, bia chungu kwa wale wanokunywa.
10 Mji ulioharibiwa umekuwa ukiwa, mlango wa kila nyumba umefungwa.
Mji uliochafuka umeangushwa chini; kila nyumba imefungwa na hakuna kitu.
11 Barabarani wanalilia kupata mvinyo, furaha yote imegeuka kuwa majonzi, furaha yote imefukuziwa mbali na dunia.
Kuna kilio mtaani kwa sababu ya mvinyo; furaha yote imetiwa giza, furaha ya nchi imetoweka.
12 Mji umeachwa katika uharibifu, lango lake limevunjwa vipande.
Ndani ya mji kumebaki ukiwa, na lango limebolewa kwa uharibifu.
13 Ndivyo itakavyokuwa duniani na miongoni mwa mataifa, kama vile wakati mzeituni upigwavyo, au kama vile wakati masazo yabakiavyo baada ya zabibu kuvunwa.
Hivi ndivyo itakavyofanyika kwa dunia yote mwiongoni mwa mataifa, pale mti wa mzabibu utakapopigwa, na waokotapo zabibu baada mavuno yake kuwa tayari.
14 Wanainua sauti zao, wanapiga kelele kwa furaha, kutoka magharibi wanasifu kwa ukelele utukufu wa Bwana.
Watanyanyua saut zao na kupiga keleleYahwe mwenye enzi, na utapaza sauti kutoka kwenye bahari.
15 Kwa hiyo upande wa mashariki mpeni Bwana utukufu, liadhimisheni jina la Bwana, Mungu wa Israeli, katika visiwa vya bahari.
Hivyo basi mashariki mtukuze Yahwe, na katika kisiwa cha bahari tukuzeni jina la Yahwe, Mungu wa Israeli.
16 Kutoka miisho ya dunia tunasikia uimbaji: “Utukufu kwa Yule Mwenye Haki.” Lakini nilisema, “Ninadhoofika, ninadhoofika! Ole wangu! Watenda hila wanasaliti! Kwa hila watenda hila wanasaliti!”
Kutoka umbali wa sehemu ya dunia tumesika nyimbo, ''Utukufu kwa watu wenye haki! Lakini nikasema, ''Nimepita mbali, Ole juu wangu! Wasaliti walshulika na wenye hila; ndio, wasaliti walishuhulika na wenye hila.''
17 Hofu, shimo na mtego vinakungojea, ewe mtu ukaaye duniani.
Hofu, shimo, na mtego yako juu yako, wenyeji wa dunia.
18 Kila akimbiaye asikiapo sauti ya hofu atatumbukia shimoni, naye yeyote apandaye kutoka shimoni, atanaswa kwenye mtego. Malango ya gharika ya mbinguni yamefunguliwa, misingi ya dunia inatikisika.
Amekimbia maana sauti ya hofu itaanguka kwenye shimo, na anayekuja juu katikati ya shimo atanaswa na mtego. Madirisha ya mbinguni yatafunguliwa, na misingi ya dunia itatikisika.
19 Dunia imepasuka, dunia imechanika, dunia imetikiswa kabisa.
Dunia itangamizwa kabisa, dunia itapasukia mbali; dunia itatatikisika vikali.
20 Dunia inapepesuka kama mlevi, inayumbayumba kama kibanda kwenye upepo; imelemewa sana na mzigo wa hatia ya uasi wake na ikianguka kamwe haitainuka tena.
Dunia itajikongoja kama mlevi na itachezacheza kurudi nyuma na mbele kama kibanda. Dhambi zao zitakuwa nzito juu yao na zitaanguka na hazitasimama tena.
21 Katika siku ile Bwana ataadhibu nguvu zilizoko mbinguni juu, na wafalme walioko duniani chini.
Itakuwa siku hiyo ambayo Yahwe ataliadhibu jeshi la aliye juu mahali pa juu, na falme za dunia katika dunia.
22 Watakusanywa pamoja kama wafungwa waliofungwa gerezani, watafungiwa gerezani na kuadhibiwa baada ya siku nyingi.
Watakusanyika pamoja, wafungwa katika shimo, na watafungw gerezani; na baada ya siku nying watadhibiwa.
23 Mwezi utatiwa haya, nalo jua litaaibishwa; kwa maana Bwana Mwenye Nguvu Zote atawala juu ya Mlima Sayuni na katika Yerusalemu, tena mbele ya wazee wake kwa utukufu.
Halafu Mwenzi utatiwa aibu na jua pia litatwa aibu, maana Yahwe wa majeshi atatawala katika mlima Sayuni na Yerusalemu, kabla ya wazee wake katika utukufu.

< Isaya 24 >