< Isaya 22 >

1 Neno kuhusu Bonde la Maono: Nini kinachokutaabisha sasa, kwamba ninyi nyote mmepanda juu ya mapaa?
משא גיא חזיון מה לך אפוא כי עלית כלך לגגות
2 Ewe mji uliojaa ghasia, ewe mji wa makelele na sherehe! Watu wenu waliokufa hawakuuawa kwa upanga, wala hawakufa vitani.
תשאות מלאה עיר הומיה--קריה עליזה חלליך לא חללי חרב ולא מתי מלחמה
3 Viongozi wako wote wamekimbia pamoja, wamekamatwa bila kutumia upinde. Ninyi nyote mliokamatwa mlichukuliwa wafungwa pamoja, mlikimbia wakati adui alipokuwa bado mbali.
כל קציניך נדדו יחד מקשת אסרו כל נמצאיך אסרו יחדו מרחוק ברחו
4 Kwa hiyo nilisema, “Geukia mbali nami, niache nilie kwa uchungu. Usijaribu kunifariji juu ya maangamizi ya watu wangu.”
על כן אמרתי שעו מני אמרר בבכי אל תאיצו לנחמני על שד בת עמי
5 Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, anayo siku ya ghasia, ya kukanyaga, na ya kuogofya katika Bonde la Maono, siku ya kuangusha kuta na ya kupiga kelele mpaka milimani.
כי יום מהומה ומבוסה ומבוכה לאדני יהוה צבאות--בגי חזיון מקרקר קר ושוע אל ההר
6 Elamu analichukua podo, pamoja na waendesha magari ya vita na farasi. Kiri anaifungua ngao.
ועילם נשא אשפה ברכב אדם פרשים וקיר ערה מגן
7 Mabonde yako yaliyo mazuri sana yamejaa magari ya vita, nao wapanda farasi wamewekwa kwenye malango ya mji;
ויהי מבחר עמקיך מלאו רכב והפרשים שת שתו השערה
8 ulinzi wa Yuda umeondolewa. Nawe ulitazama siku ile silaha katika Jumba la Kifalme la Mwituni,
ויגל את מסך יהודה ותבט ביום ההוא אל נשק בית היער
9 mkaona kuwa Mji wa Daudi una matundu mengi katika ulinzi wake, mkaweka akiba ya maji kwenye Bwawa la Chini.
ואת בקיעי עיר דוד ראיתם כי רבו ותקבצו את מי הברכה התחתונה
10 Mlihesabu majengo katika Yerusalemu nanyi mkabomoa nyumba ili kuimarisha ukuta.
ואת בתי ירושלם ספרתם ותתצו הבתים לבצר החומה
11 Mlijenga bwawa la maji katikati ya kuta mbili kwa ajili ya maji ya Bwawa la Zamani, lakini hamkumtazama Yule aliyelitengeneza, au kuwa na heshima kwa Yule aliyeubuni tangu zamani za kale.
ומקוה עשיתם בין החמתים למי הברכה הישנה ולא הבטתם אל עשיה ויצרה מרחוק לא ראיתם
12 Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, aliwaita siku ile ili kulia na kuomboleza, kungʼoa nywele zenu na kuvaa nguo ya gunia.
ויקרא אדני יהוה צבאות--ביום ההוא לבכי ולמספד ולקרחה ולחגר שק
13 Lakini tazama, kuna furaha na sherehe, kuchinja ngʼombe na kuchinja kondoo, kula nyama na kunywa mvinyo! Mnasema, “Tuleni na kunywa, kwa kuwa kesho tutakufa!”
והנה ששון ושמחה הרג בקר ושחט צאן אכל בשר ושתות יין אכול ושתו כי מחר נמות
14 Bwana Mwenye Nguvu Zote amelifunua hili nikiwa ninasikia: Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, asema: “Mpaka siku ya kufa kwenu, dhambi hii haitafanyiwa upatanisho.”
ונגלה באזני יהוה צבאות אם יכפר העון הזה לכם עד תמתון אמר אדני יהוה צבאות
15 Hili ndilo Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, asemalo: “Nenda ukamwambie huyu wakili Shebna, ambaye ni msimamizi wa jumba la kifalme:
כה אמר אדני יהוה צבאות לך בא אל הסכן הזה על שבנא אשר על הבית
16 Unafanya nini hapa, na ni nani aliyekupa ruhusa kujikatia kaburi lako mwenyewe, ukichonga kaburi lako mahali palipo juu, na kutoboa kwa patasi mahali pako pa kupumzikia katika mwamba?
מה לך פה ומי לך פה כי חצבת לך פה קבר חצבי מרום קברו חקקי בסלע משכן לו
17 “Jihadhari, Bwana yu karibu kukukamata thabiti, na kukutupa mbali, ewe mtu mwenye nguvu.
הנה יהוה מטלטלך טלטלה גבר ועטך עטה
18 Atakuvingirisha uwe kama mpira na kukutupa katika nchi kubwa. Huko ndiko utakakofia, na huko ndiko magari yako ya vita ya fahari yatabakia, wewe unayeifedhehesha nyumba ya bwana wako!
צנוף יצנפך צנפה כדור אל ארץ רחבת ידים שמה תמות ושמה מרכבות כבודך--קלון בית אדניך
19 Nitakuondoa kutoka kazi yako, nawe utaondoshwa kutoka nafasi yako.
והדפתיך ממצבך וממעמדך יהרסך
20 “Katika siku ile, nitamwita mtumishi wangu, Eliakimu mwana wa Hilkia.
והיה ביום ההוא וקראתי לעבדי לאליקים בן חלקיהו
21 Nitamvika joho lako, nami nitamfunga mshipi wako kiunoni mwake, na kumkabidhi mamlaka yako. Yeye atakuwa baba kwa wale wanaoishi Yerusalemu na kwa nyumba ya Yuda.
והלבשתיו כתנתך ואבנטך אחזקנו וממשלתך אתן בידו והיה לאב ליושב ירושלם ולבית יהודה
22 Nitaweka mabegani mwake ufunguo wa nyumba ya Daudi. Kile afunguacho hakuna awezaye kufunga, na kile afungacho hakuna awezaye kufungua.
ונתתי מפתח בית דוד על שכמו ופתח ואין סגר וסגר ואין פתח
23 Nitamgongomea kama kigingi kilicho mahali palipo imara, naye atakuwa kiti cha enzi cha heshima kwa ajili ya nyumba ya baba yake.
ותקעתיו יתד במקום נאמן והיה לכסא כבוד לבית אביו
24 Utukufu wote wa jamaa yake utakuwa juu yake: Watoto wa jamaa hiyo na machipukizi yake, vyombo vyake vyote vidogo, tangu bakuli hadi magudulia yote.”
ותלו עליו כל כבוד בית אביו הצאצאים והצפעות כל כלי הקטן--מכלי האגנות ועד כל כלי הנבלים
25 Bwana Mwenye Nguvu Zote asema, “Katika siku ile, kigingi kilichogongomewa mahali imara kitaachia njia. Kitakatwa, nacho kitaanguka na mzigo ulioningʼinia juu yake utaanguka chini.” Bwana amesema.
ביום ההוא נאם יהוה צבאות תמוש היתד התקועה במקום נאמן ונגדעה ונפלה ונכרת המשא אשר עליה--כי יהוה דבר

< Isaya 22 >