< Isaya 2 >

1 Hili ndilo aliloliona Isaya mwana wa Amozi kuhusu Yuda na Yerusalemu:
הדבר אשר חזה ישעיהו בן אמוץ על יהודה וירושלם
2 Katika siku za mwisho mlima wa Hekalu la Bwana utaimarishwa kama mlima mkuu miongoni mwa milima yote, utainuliwa juu ya vilima, na mataifa yote yatamiminika huko.
והיה באחרית הימים נכון יהיה הר בית יהוה בראש ההרים ונשא מגבעות ונהרו אליו כל הגוים
3 Mataifa mengi yatakuja na kusema, “Njooni, twendeni mlimani mwa Bwana, kwenye nyumba ya Mungu wa Yakobo. Atatufundisha njia zake, ili tuweze kuenenda katika mapito yake.” Sheria itatoka Sayuni, neno la Bwana litatoka Yerusalemu.
והלכו עמים רבים ואמרו לכו ונעלה אל הר יהוה אל בית אלהי יעקב וירנו מדרכיו ונלכה בארחתיו כי מציון תצא תורה ודבר יהוה מירושלם
4 Atahukumu kati ya mataifa na ataamua migogoro ya mataifa mengi. Watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao kuwa miundu ya kukata matawi. Taifa halitainua upanga dhidi ya taifa jingine, wala hawatajifunza vita tena.
ושפט בין הגוים והוכיח לעמים רבים וכתתו חרבותם לאתים וחניתותיהם למזמרות--לא ישא גוי אל גוי חרב ולא ילמדו עוד מלחמה
5 Njooni, enyi nyumba ya Yakobo, tutembeeni katika nuru ya Bwana.
בית יעקב--לכו ונלכה באור יהוה
6 Umewatelekeza watu wako, nyumba ya Yakobo. Wamejaa ushirikina utokao Mashariki, wanapiga ramli kama Wafilisti na wanashikana mikono na wapagani.
כי נטשתה עמך בית יעקב--כי מלאו מקדם ועננים כפלשתים ובילדי נכרים ישפיקו
7 Nchi yao imejaa fedha na dhahabu, hakuna mwisho wa hazina zao. Nchi yao imejaa farasi, hakuna mwisho wa magari yao.
ותמלא ארצו כסף וזהב ואין קצה לאצרתיו ותמלא ארצו סוסים ואין קצה למרכבתיו
8 Nchi yao imejaa sanamu, wanasujudia kazi za mikono yao, vitu vile vidole vyao vimevitengeneza.
ותמלא ארצו אלילים למעשה ידיו ישתחוו לאשר עשו אצבעתיו
9 Kwa hiyo mwanadamu atashushwa na binadamu atanyenyekezwa: usiwasamehe.
וישח אדם וישפל איש ואל תשא להם
10 Ingieni kwenye miamba, jificheni ardhini kutokana na utisho wa Bwana na utukufu wa enzi yake!
בוא בצור והטמן בעפר מפני פחד יהוה ומהדר גאנו
11 Macho ya mtu mwenye majivuno yatanyenyekezwa na kiburi cha wanadamu kitashushwa, Bwana peke yake ndiye atakayetukuzwa siku hiyo.
עיני גבהות אדם שפל ושח רום אנשים ונשגב יהוה לבדו ביום ההוא
12 Bwana Mwenye Nguvu Zote anayo siku aliyoiweka akiba kwa wote wenye kujivuna na wenye kiburi, kwa wote wanaojikweza (nao watanyenyekezwa),
כי יום ליהוה צבאות על כל גאה--ורם ועל כל נשא ושפל
13 kwa mierezi yote ya Lebanoni iliyo mirefu sana, na mialoni yote ya Bashani,
ועל כל ארזי הלבנון הרמים והנשאים ועל כל אלוני הבשן
14 kwa milima yote mirefu na vilima vyote vilivyoinuka,
ועל כל ההרים הרמים ועל כל הגבעות הנשאות
15 kwa kila mnara ulio mrefu sana na kila ukuta wenye ngome,
ועל כל מגדל גבה ועל כל חומה בצורה
16 kwa kila meli ya biashara, na kila chombo cha baharini cha fahari.
ועל כל אניות תרשיש ועל כל שכיות החמדה
17 Majivuno ya mwanadamu yatashushwa, na kiburi cha wanadamu kitanyenyekezwa, Bwana peke yake ndiye atatukuzwa siku hiyo,
ושח גבהות האדם ושפל רום אנשים ונשגב יהוה לבדו ביום ההוא
18 nazo sanamu zitatoweka kabisa.
והאלילים כליל יחלף
19 Watu watakimbilia kwenye mapango ndani ya miamba, na kwenye mahandaki ardhini kutokana na utisho wa Bwana na utukufu wa enzi yake, ainukapo kuitikisa dunia.
ובאו במערות צרים ובמחלות עפר--מפני פחד יהוה ומהדר גאונו בקומו לערץ הארץ
20 Siku ile, watu watawatupia panya na popo sanamu zao za fedha na za dhahabu, walizozitengeneza ili waziabudu.
ביום ההוא ישליך האדם את אלילי כספו ואת אלילי זהבו--אשר עשו לו להשתחות לחפר פרות ולעטלפים
21 Watakimbilia kwenye mapango miambani na kwenye nyufa za miamba kutokana na utisho wa Bwana na utukufu wa enzi yake, ainukapo kuitikisa dunia.
לבוא בנקרות הצרים ובסעפי הסלעים--מפני פחד יהוה ומהדר גאונו בקומו לערץ הארץ
22 Acheni kumtumainia mwanadamu, ambaye hana kitu ila pumzi katika pua zake. Yeye ana thamani gani?
חדלו לכם מן האדם אשר נשמה באפו כי במה נחשב הוא

< Isaya 2 >