< Isaya 16 >
1 Pelekeni wana-kondoo kama ushuru kwa mtawala wa nchi, Kutoka Sela, kupitia jangwani, hadi mlima wa Binti Sayuni.
你们当将羊羔奉给那地掌权的, 从西拉往旷野,送到锡安城的山。
2 Kama ndege wanaopapatika waliofukuzwa kutoka kwenye kiota, ndivyo walivyo wanawake wa Moabu kwenye vivuko vya Arnoni.
摩押的居民在亚嫩渡口, 必像游飞的鸟,如拆窝的雏。
3 “Tupeni shauri, toeni uamuzi. Wakati wa adhuhuri, fanyeni kivuli chenu kama usiku. Waficheni watoro, msisaliti wakimbizi.
求你献谋略,行公平, 使你的影子在午间如黑夜, 隐藏被赶散的人,不可显露逃民。
4 Waacheni watoro wa Moabu wakae pamoja nanyi; kuweni mahali pao pa salama ili kuepuka mharabu.” Mtesi atafikia mwisho na maangamizi yatakoma, aletaye vita atatoweka kutoka nchi.
求你容我这被赶散的人和你同居。 至于摩押,求你作他的隐密处, 脱离灭命者的面。 勒索人的归于无有, 毁灭的事止息了, 欺压人的从国中除灭了,
5 Kwa upendo kiti cha enzi kitaimarishwa, kwa uaminifu mtu ataketi juu yake, yeye atokaye nyumba ya Daudi: yeye ambaye katika kuhukumu hutafuta haki, na huhimiza njia ya haki.
必有宝座因慈爱坚立; 必有一位诚诚实实坐在其上, 在大卫帐幕中施行审判, 寻求公平,速行公义。
6 Tumesikia juu ya kiburi cha Moabu: kiburi chake cha kujivuna na udanganyifu, kiburi chake na ufidhuli wake, lakini majivuno yake si kitu.
我们听说摩押人骄傲, 是极其骄傲; 听说他狂妄、骄傲、忿怒; 他夸大的话是虚空的。
7 Kwa hiyo Wamoabu wanaomboleza, wanaiombolezea Moabu kwa pamoja. Wanaomboleza na kuhuzunika kwa ajili ya watu wa Kir-Haresethi.
因此,摩押人必为摩押哀号; 人人都要哀号。 你们摩押人要为吉珥·哈列设的葡萄饼哀叹, 极其忧伤。
8 Mashamba ya Heshboni yananyauka, pia na mizabibu ya Sibma. Watawala wa mataifa wamekanyaga mizabibu iliyo mizuri sana, ambayo ilipata kufika Yazeri na kuenea kuelekea jangwani. Machipukizi yake yalienea yakafika hadi baharini.
因为希实本的田地 和西比玛的葡萄树都衰残了。 列国的君主折断其上美好的枝子; 这枝子长到雅谢延到旷野, 嫩枝向外探出,直探过盐海。
9 Hivyo ninalia kama Yazeri aliavyo, kwa ajili ya mizabibu ya Sibma. Ee Heshboni, ee Eleale, ninakulowesha kwa machozi! Kelele za furaha kwa ajili ya tunda lako lililoiva na kwa ajili ya mavuno zimekomeshwa.
因此,我要为西比玛的葡萄树哀哭, 与雅谢人哀哭一样。 希实本、以利亚利啊, 我要以眼泪浇灌你; 因为有交战呐喊的声音 临到你夏天的果子, 并你收割的庄稼。
10 Furaha na shangwe zimeondolewa kutoka mashamba ya matunda; hakuna yeyote aimbaye wala apazaye sauti katika mashamba ya mizabibu; hakuna yeyote akanyagaye zabibu shinikizoni, kwa kuwa nimekomesha makelele.
从肥美的田中夺去了欢喜快乐; 在葡萄园里必无歌唱,也无欢呼的声音。 踹酒的在酒榨中不得踹出酒来; 我使他欢呼的声音止息。
11 Moyo wangu unaomboleza kwa ajili ya Moabu kama kinubi, nafsi yangu yote kwa ajili ya Kir-Haresethi.
因此,我心腹为摩押哀鸣如琴; 我心肠为吉珥·哈列设也是如此。
12 Wakati Moabu anapojitokeza mahali pake pa juu, anajichosha mwenyewe tu; anapokwenda mahali pake pa kuabudia miungu ili kuomba, haitamfaidi lolote.
摩押人朝见的时候,在高处疲乏,又到他圣所祈祷,也不蒙应允。
13 Hili ndilo neno ambalo Bwana ameshasema kuhusu Moabu.
这是耶和华从前论摩押的话。
14 Lakini sasa Bwana anasema: “Katika miaka mitatu, kama vile mtumishi aliyefungwa na mkataba angeihesabu, fahari ya Moabu na watu wake wengi watadharauliwa, nao walionusurika watakuwa wachache sana, tena wanyonge.”
但现在耶和华说:“三年之内,照雇工的年数,摩押的荣耀与他的群众必被藐视,余剩的人甚少无几。”