< Isaya 15 >

1 Neno kuhusu Moabu: Ari iliyo Moabu imeangamizwa: imeharibiwa kwa usiku mmoja! Kiri iliyo Moabu imeangamizwa, imeharibiwa kwa usiku mmoja!
משא מואב כי בליל שדד ער מואב נדמה--כי בליל שדד קיר מואב נדמה
2 Diboni anakwea hadi kwenye hekalu lake, mpaka mahali pake pa juu ili walie, Moabu anaombolezea Nebo na Medeba. Kila kichwa kimenyolewa na kila ndevu limeondolewa.
עלה הבית ודיבן הבמות לבכי על נבו ועל מידבא מואב ייליל--בכל ראשיו קרחה כל זקן גרועה
3 Wamevaa nguo za magunia barabarani, juu ya mapaa na kwenye viwanja wote wanaomboleza, wamelala kifudifudi kwa kulia.
בחוצתיו חגרו שק על גגותיה וברחבתיה כלה ייליל ירד בבכי
4 Heshboni na Eleale wanalia, sauti zao zinasikika hadi Yahazi. Kwa hiyo watu wenye silaha wa Moabu wanapiga kelele, nayo mioyo yao imezimia.
ותזעק חשבון ואלעלה עד יהץ נשמע קולם על כן חלצי מואב יריעו--נפשו ירעה לו
5 Moyo wangu unamlilia Moabu; wakimbizi wake wanakimbilia Soari, hadi Eglath-Shelishiya. Wanapanda njia ya kwenda Luhithi, wanakwenda huku wanalia; barabarani iendayo Horonaimu wanaombolezea maangamizi yao.
לבי למואב יזעק בריחה עד צער עגלת שלשיה כי מעלה הלוחית בבכי יעלה בו--כי דרך חורנים זעקת שבר יעערו
6 Maji ya Nimrimu yamekauka na majani yamenyauka; mimea imekauka wala hakuna kitu chochote kibichi kilichobaki.
כי מי נמרים משמות יהיו כי יבש חציר כלה דשא ירק לא היה
7 Kwa hiyo mali waliyoipata na kujiwekea akiba wamezichukua na kuvuka Bonde la Mierebi.
על כן יתרה עשה ופקדתם--על נחל הערבים ישאום
8 Mwangwi wa kilio chao umefika hadi mpakani mwa Moabu, kilio chao cha huzuni kimefika hadi Eglaimu, maombolezo yao hadi Beer-Elimu.
כי הקיפה הזעקה את גבול מואב עד אגלים יללתה ובאר אילים יללתה
9 Maji ya Dimoni yamejaa damu, lakini bado nitaleta pigo jingine juu ya Dimoni: simba juu ya wakimbizi wa Moabu na juu ya wale wanaobaki katika nchi.
כי מי דימון מלאו דם כי אשית על דימון נוספות--לפליטת מואב אריה ולשארית אדמה

< Isaya 15 >