< Hosea 6 >
1 “Njooni, tumrudie Bwana. Ameturarua vipande vipande lakini atatuponya; ametujeruhi lakini atatufunga majeraha yetu.
来吧,我们归向耶和华! 他撕裂我们,也必医治; 他打伤我们,也必缠裹。
2 Baada ya siku mbili atatufufua; katika siku ya tatu atatuinua, ili tuweze kuishi mbele zake.
过两天他必使我们苏醒, 第三天他必使我们兴起, 我们就在他面前得以存活。
3 Tumkubali Bwana, tukaze kumkubali yeye. Kutokea kwake ni hakika kama vile kuchomoza kwa jua; atatujia kama mvua za masika, kama vile mvua za vuli ziinyweshavyo nchi.”
我们务要认识耶和华, 竭力追求认识他。 他出现确如晨光; 他必临到我们像甘雨, 像滋润田地的春雨。
4 “Nifanye nini nawe, Efraimu? Nifanye nini nawe, Yuda? Upendo wako ni kama ukungu wa asubuhi, kama umande wa alfajiri utowekao.
主说:以法莲哪,我可向你怎样行呢? 犹大啊,我可向你怎样做呢? 因为你们的良善如同早晨的云雾, 又如速散的甘露。
5 Kwa hiyo ninawakata ninyi vipande vipande kwa kutumia manabii wangu; nimewaua ninyi kwa maneno ya kinywa changu, hukumu zangu zinawaka kama umeme juu yenu.
因此,我借先知砍伐他们, 以我口中的话杀戮他们; 我施行的审判如光发出。
6 Kwa maana nataka rehema, wala si dhabihu, kumkubali Mungu zaidi kuliko sadaka za kuteketezwa.
我喜爱良善,不喜爱祭祀; 喜爱认识 神,胜于燔祭。
7 Wamevunja Agano kama Adamu: huko hawakuwa waaminifu kwangu.
他们却如亚当背约, 在境内向我行事诡诈。
8 Gileadi ni mji wenye watu waovu, umetiwa madoa kwa nyayo za damu.
基列是作孽之人的城, 被血沾染。
9 Kama wanyangʼanyi wamviziavyo mtu, ndivyo magenge ya makuhani wafanyavyo; wanaulia watu kwenye njia iendayo Shekemu, wakifanya uhalifu wa aibu.
强盗成群,怎样埋伏杀人, 祭司结党,也照样在示剑的路上杀戮, 行了邪恶。
10 Nimeona jambo la kutisha katika nyumba ya Israeli. Huko Efraimu amejitolea kwa ukahaba na Israeli amenajisika.
在以色列家,我见了可憎的事; 在以法莲那里有淫行, 以色列被玷污。
11 “Pia kwa ajili yako, Yuda, mavuno yameamriwa. “Wakati wowote ningerejesha neema ya watu wangu,
犹大啊,我使被掳之民归回的时候, 必有为你所命定的收场。