< Hosea 4 >

1 Sikieni neno la Bwana, enyi Waisraeli, kwa sababu Bwana analo shtaka dhidi yenu ninyi mnaoishi katika nchi: “Hakuna uaminifu, hakuna upendo, hakuna kumjua Mungu katika nchi.
שמעו דבר יהוה בני ישראל כי ריב ליהוה עם יושבי הארץ כי אין אמת ואין חסד ואין דעת אלהים בארץ׃
2 Kuna kulaani tu, uongo na uuaji, wizi na uzinzi, bila kuwa na mipaka, nao umwagaji damu mmoja baada ya mwingine.
אלה וכחש ורצח וגנב ונאף פרצו ודמים בדמים נגעו׃
3 Kwa sababu hii nchi huomboleza, wote waishio ndani mwake wanadhoofika, wanyama wa kondeni, ndege wa angani na samaki wa baharini wanakufa.
על כן תאבל הארץ ואמלל כל יושב בה בחית השדה ובעוף השמים וגם דגי הים יאספו׃
4 “Lakini mtu awaye yote na asilete shtaka, mtu yeyote na asimlaumu mwenzake, kwa maana watu wako ni kama wale waletao mashtaka dhidi ya kuhani.
אך איש אל ירב ואל יוכח איש ועמך כמריבי כהן׃
5 Unajikwaa usiku na mchana, nao manabii hujikwaa pamoja nawe. Kwa hiyo nitamwangamiza mama yako:
וכשלת היום וכשל גם נביא עמך לילה ודמיתי אמך׃
6 watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa, “Kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeacha kuijali sheria ya Mungu wako mimi nami sitawajali watoto wako.
נדמו עמי מבלי הדעת כי אתה הדעת מאסת ואמאסאך מכהן לי ותשכח תורת אלהיך אשכח בניך גם אני׃
7 Kadiri makuhani walivyoongezeka, ndivyo walivyozidi kutenda dhambi dhidi yangu, walibadilisha utukufu wao kwa kitu cha aibu.
כרבם כן חטאו לי כבודם בקלון אמיר׃
8 Hujilisha dhambi za watu wangu na kupendezwa na uovu wao.
חטאת עמי יאכלו ואל עונם ישאו נפשו׃
9 Hata itakuwa: Kama walivyo watu, ndivyo walivyo makuhani. Nitawaadhibu wote wawili kwa ajili ya njia zao na kuwalipa kwa matendo yao.
והיה כעם ככהן ופקדתי עליו דרכיו ומעלליו אשיב לו׃
10 “Watakula lakini hawatashiba; watajiingiza katika ukahaba lakini hawataongezeka, kwa sababu wamemwacha Bwana na kujiingiza wenyewe
ואכלו ולא ישבעו הזנו ולא יפרצו כי את יהוה עזבו לשמר׃
11 katika ukahaba, divai ya zamani na divai mpya, ambavyo huondoa ufahamu
זנות ויין ותירוש יקח לב׃
12 wa watu wangu. Hutaka shauri kutoka kwa sanamu ya mti nao hujibiwa na fimbo ya mti. Roho ya ukahaba imewapotosha, hawana uaminifu kwa Mungu wao.
עמי בעצו ישאל ומקלו יגיד לו כי רוח זנונים התעה ויזנו מתחת אלהיהם׃
13 Wanatoa dhabihu juu ya vilele vya milima na sadaka za kuteketezwa juu ya vilima, chini ya mialoni, milibua na miela, ambako kuna vivuli vizuri. Kwa hiyo binti zenu wamegeukia ukahaba na wake za wana wenu uzinzi.
על ראשי ההרים יזבחו ועל הגבעות יקטרו תחת אלון ולבנה ואלה כי טוב צלה על כן תזנינה בנותיכם וכלותיכם תנאפנה׃
14 “Sitawaadhibu binti zenu wakati wanapogeukia ukahaba, wala wake za wana wenu wanapofanya uzinzi, kwa sababu wanaume wenyewe huandamana na malaya na kutambikia pamoja na makahaba wa mahali pa kuabudia miungu: watu wasiokuwa na ufahamu wataangamia!
לא אפקוד על בנותיכם כי תזנינה ועל כלותיכם כי תנאפנה כי הם עם הזנות יפרדו ועם הקדשות יזבחו ועם לא יבין ילבט׃
15 “Ingawa umefanya uzinzi, ee Israeli, Yuda naye asije akawa na hatia. “Usiende Gilgali, usipande kwenda Beth-Aveni Wala usiape, ‘Hakika kama Bwana aishivyo!’
אם זנה אתה ישראל אל יאשם יהודה ואל תבאו הגלגל ואל תעלו בית און ואל תשבעו חי יהוה׃
16 Waisraeli ni wakaidi, kama mtamba wa ngʼombe ambaye ni mkaidi. Ni jinsi gani basi Bwana anaweza kuwachunga kama wana-kondoo katika shamba la majani?
כי כפרה סררה סרר ישראל עתה ירעם יהוה ככבש במרחב׃
17 Efraimu amejiunga na sanamu, ondokana naye!
חבור עצבים אפרים הנח לו׃
18 Hata wakati wamemaliza vileo vyao wanaendelea na ukahaba wao, watawala wao hupenda sana njia za aibu.
סר סבאם הזנה הזנו אהבו הבו קלון מגניה׃
19 Kisulisuli kitawafagilia mbali na dhabihu zao zitawaletea aibu.
צרר רוח אותה בכנפיה ויבשו מזבחותם׃

< Hosea 4 >