< Hosea 12 >

1 Efraimu anajilisha upepo; hufukuzia upepo wa mashariki kutwa nzima na kuzidisha uongo na jeuri. Anafanya mkataba na Ashuru na kutuma mafuta ya zeituni Misri.
以法莲吃风,且追赶东风, 时常增添虚谎和强暴, 与亚述立约,把油送到埃及。
2 Bwana analo shtaka dhidi ya Yuda, atamwadhibu Yakobo kwa kadiri ya njia zake na kumlipa kwa kadiri ya matendo yake.
耶和华与犹大争辩, 必照雅各所行的惩罚他, 按他所做的报应他。
3 Yakobo akiwa tumboni alishika kisigino cha kaka yake; kama mwanadamu, alishindana na Mungu.
他在腹中抓住哥哥的脚跟, 壮年的时候与 神较力,
4 Alishindana na malaika na kumshinda; alilia na kuomba upendeleo wake. Alimkuta huko Betheli na kuzungumza naye huko:
与天使较力,并且得胜, 哭泣恳求, 在伯特利遇见耶和华。 耶和华—万军之 神在那里晓谕我们以色列人; 耶和华是他可记念的名。
5 Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote, Bwana ndilo jina lake!
6 Lakini ni lazima urudi kwa Mungu wako; dumisha upendo na haki, nawe umngojee Mungu wako siku zote.
所以你当归向你的 神, 谨守仁爱、公平,常常等候你的 神。
7 Mfanyabiashara hutumia vipimo vya udanganyifu; hupenda kupunja.
以法莲是商人, 手里有诡诈的天平,爱行欺骗。
8 Efraimu hujisifu akisema, “Mimi ni tajiri sana; nimetajirika. Pamoja na utajiri wangu wote hawatakuta ndani yangu uovu wowote au dhambi.”
以法莲说: 我果然成了富足,得了财宝; 我所劳碌得来的, 人必不见有什么不义,可算为罪的。
9 “Mimi ndimi Bwana Mungu wenu niliyewaleta kutoka Misri; nitawafanya mkae tena kwenye mahema, kama vile katika siku za sikukuu zenu zilizoamriwa.
自从你出埃及地以来, 我就是耶和华—你的 神; 我必使你再住帐棚,如在大会的日子一样。
10 Niliongea na manabii, nikawapa maono mengi na kusema mifano kupitia wao.”
我已晓谕众先知, 并且加增默示, 借先知设立比喻。
11 Je, Gileadi si mwovu? Watu wake hawafai kitu! Je, hawatoi dhabihu za mafahali huko Gilgali? Madhabahu zao zitakuwa kama malundo ya mawe katika shamba lililolimwa.
基列人没有罪孽吗? 他们全然是虚假的。 人在吉甲献牛犊为祭, 他们的祭坛好像田间犁沟中的乱堆。
12 Yakobo alikimbilia katika nchi ya Aramu; Israeli alitumika ili apate mke, ili aweze kulipa kwa ajili yake alichunga kondoo.
从前雅各逃到亚兰地, 以色列为得妻服事人, 为得妻与人放羊。
13 Bwana alimtumia nabii kumpandisha Israeli kutoka Misri, kwa njia ya nabii alimtunza.
耶和华借先知领以色列从埃及上来; 以色列也借先知而得保存。
14 Lakini Efraimu amemchochea sana hasira; Bwana wake ataleta juu yake hatia yake ya kumwaga damu naye atamlipiza kwa ajili ya dharau yake.
以法莲大大惹动主怒, 所以他流血的罪必归在他身上。 主必将那因以法莲所受的羞辱归还他。

< Hosea 12 >