< Hosea 11 >

1 “Wakati Israeli alipokuwa mtoto, nilimpenda, nilimwita mwanangu kutoka Misri.
“Wakati Israeli alikuwa kijana nilimpenda, na nikamwita mtoto wangu kutoka Misri.
2 Lakini kadiri nilivyomwita Israeli, ndivyo walivyokwenda mbali nami. Walitoa dhabihu kwa Mabaali na kufukiza uvumba kwa vinyago.
Kwa kadiri waliyoitwa, ndivyo walivyoondoka kwangu. Wakawafanyia dhabihu Baali, wakatafuta uvumba kwa sanamu.
3 Mimi ndiye niliyemfundisha Efraimu kutembea, nikiwashika mikono; lakini hawakutambua kuwa ni mimi niliyewaponya.
Lakini mimi ndio niliyemfundisha Efraimu kutembea. Ndiye niliyewainua kwa silaha zao, lakini hawakujua kwamba niliwajali.
4 Niliwaongoza kwa kamba za huruma ya kibinadamu, kwa vifungo vya upendo; niliondoa nira shingoni mwao nami nikainama kuwalisha.
Niliwaongoza kwa kamba za ubinadamu, na mafungo ya upendo. Mimi nilikuwa kama mtu aliyepunguza jozi juu ya taya zao, na nikainama na kuwalisha.
5 “Je, hawatarudi Misri, nayo Ashuru haitawatawala kwa sababu wamekataa kutubu?
Je, hawatarudi nchi ya Misri? Je, Ashuru haitatawala juu yao kwa sababu wanakataa kurudi kwangu?
6 Panga zitametameta katika miji yao, zitaharibu makomeo ya malango yao na kukomesha mipango yao.
Upanga utaanguka juu ya miji yao na kuharibu makomeo ya milango yao; itawaangamiza kwa sababu ya mipango yao wenyewe.
7 Watu wangu wamedhamiria kuniacha. Hata kama wakimwita Yeye Aliye Juu Sana, kwa vyovyote hatawainua.
Watu wangu wameamua kuniacha. Ingawa wanaita kwa Aliye Juu, hakuna mtu atawasaidia.
8 “Efraimu, ninawezaje kukuacha? Ee Israeli, ninawezaje kukutoa? Nitawezaje kukutendea kama Adma? Nitawezaje kukufanya kama Seboimu? Moyo wangu umegeuka ndani yangu, huruma zangu zote zimeamshwa.
Ninawezaje kukuacha, Efraimu? Ninawezaje kukupeleka, Israeli? Ninawezaje kukufanya kama Adma? Ninawezaje kukufanya kama Seboimu? Moyo wangu umebadilika ndani yangu; huruma zangu zote zimeongezeka.
9 Sitatimiza hasira yangu kali, wala sitageuka na kumharibu Efraimu. Kwa kuwa mimi ndimi Mungu, wala si mwanadamu, Aliye Mtakatifu miongoni mwenu. Sitakuja kwa ghadhabu.
Sitafanya hasira yangu kali; Mimi sitawaangamiza Efraimu tena. Kwa maana mimi ni Mungu, wala si mtu; Mimi ni Mtakatifu kati yenu, nami sitakuja katika ghadhabu.
10 Watamfuata Bwana; atanguruma kama simba. Wakati angurumapo, watoto wake watakuja wakitetemeka kutoka magharibi.
Watanifuata, Bwana. Nitanguruma kama simba. Nami nitaomboleza, na watu watakuja wakitetemeka kutoka magharibi.
11 Watakuja wakitetemeka kama ndege wakitoka Misri, kama hua wakitoka Ashuru. Nitawakalisha katika nyumba zao,” asema Bwana.
Watakuja wakitetemeka kama ndege kutoka Misri, kama njiwa kutoka nchi ya Ashuru. Nitawafanya wapate kuishi katika nyumba zao.” Hii ndiyo tamko la Bwana.
12 Efraimu amenizunguka kwa uongo, nyumba ya Israeli kwa udanganyifu. Naye Yuda ni mkaidi dhidi ya Mungu, hata kinyume cha yule mwaminifu Aliye Mtakatifu.
Efraimu ananizunguka kwa maneno ya uongo, na nyumba ya Israeli kwa udanganyifu. Lakini Yuda bado anaendelea nami, Mungu, na ni mwaminifu kwangu, Mtakatifu.

< Hosea 11 >