< Hosea 10 >

1 Israeli alikuwa mzabibu uliostawi sana, alijizalia matunda mwenyewe. Kadiri matunda yake yalivyoongezeka, alijenga madhabahu zaidi; kadiri nchi yake ilivyostawi, alipamba mawe yake ya ibada.
Israeli ni mzabibu mzuri ambao huzaa matunda yake. kwa kadiri matunda yake yanavyoongezeka vivyo hivyo anajenga madhabahu nyingi. Kwa kuwa nchi yake ilizalishwa zaidi, aliboresha nguzo zake.
2 Moyo wao ni mdanganyifu, nao sasa lazima wachukue hatia yao. Bwana atabomoa madhabahu zao na kuharibu mawe yao ya ibada.
Moyo wao ni udanganyifu; sasa wanapaswa kubeba hatia yao. Bwana ataharibu madhabahu zao; ataharibu nguzo zao.
3 Kisha watasema, “Hatuna mfalme kwa sababu hatukumheshimu Bwana. Lakini hata kama tungelikuwa na mfalme, angeweza kutufanyia nini?”
Kwa maana watasema, “Hatuna mfalme, kwa maana hatukumcha Bwana. Na mfalme-angeweza kutufanyia nini?”
4 Wanaweka ahadi nyingi, huapa viapo vya uongo wanapofanya mapatano; kwa hiyo mashtaka huchipuka kama magugu ya sumu katika shamba lililolimwa.
Wanasema maneno tupu na kufanya maagano kwa kuapa uongo. Kwa hivyo haki inakuja kama magugu yenye sumu katika mito ya shamba.
5 Watu wanaoishi Samaria huogopa kwa ajili ya sanamu ya ndama ya Beth-Aveni. Watu wake wataiombolezea, vivyo hivyo kuhani wake wa kuabudu sanamu, wale waliokuwa wamefurahia fahari yake, kwa sababu itaondolewa kutoka kwao kwenda uhamishoni.
Wakazi wa Samaria wataogopa kwa sababu ya ndama za Beth Aveni. Watu wake waliomboleza juu yao, kama walivyofanya wale makuhani wa sanamu ambao walikuwa wamefurahi juu yao na utukufu wao, lakini hawako tena.
6 Itachukuliwa kwenda Ashuru kama ushuru kwa mfalme mkuu. Efraimu atafedheheshwa; Israeli ataaibika kwa ajili ya sanamu zake za mti.
Wao watachukuliwa kwenda Ashuru kama sadaka kwa mfalme mkuu. Efraimu atakuwa na aibu, na Israeli atakuwa na aibu kwa sanamu yake.
7 Samaria na mfalme wake wataelea kama kijiti juu ya uso wa maji.
Mfalme wa Samaria ataangamizwa, kama chipu cha kuni juu ya uso wa maji.
8 Mahali pa kuabudia sanamu pa uovu pataharibiwa: ndiyo dhambi ya Israeli. Miiba na mibaruti itaota na kufunika madhabahu zao. Kisha wataiambia milima, “Tufunikeni!” na vilima, “Tuangukieni!”
Sehemu za juu za uovu zitaharibiwa. Hii ndiyo dhambi ya Israeli! Miti na vichaka vitakua juu ya madhabahu zao. Watu wataiambia milima, “Tufunike sisi!” na kwa vilima, “Tuangukieni!”
9 “Tangu siku za Gibea, mmetenda dhambi, ee Israeli, huko ndiko mlikobaki. Je, vita havikuwapata watenda mabaya huko Gibea?
Ee Israeli, umetenda dhambi tangu siku za Gibea; huko umebaki. Je, vita vitawapata wana wa uovu huko Gibea?
10 Wakati nitakapopenda, nitawaadhibu; mataifa yatakusanywa dhidi yao ili kuwaweka katika vifungo kwa ajili ya dhambi zao mbili.
Nitakapotaka, nitawaadhibu. Mataifa wataungana pamoja nao na kuwaweka katika vifungo kwa uovu wao mara mbili.
11 Efraimu ni mtamba wa ngʼombe aliyefundishwa ambaye hupenda kupura, hivyo nitamfunga nira juu ya shingo yake nzuri. Nitamwendesha Efraimu, Yuda lazima alime, naye Yakobo lazima avunjavunje mabonge ya udongo.
Efraimu ni ndama mwenye mafunzo ambayo anapenda kupura nafaka, hivyo nitaweka jozi juu ya shingo yake nzuri. Efraimu nitauweka jozi; Yuda ataimea; Yakobo atauvuta pigo kwa nafsi yake.
12 Jipandieni wenyewe haki, vuneni matunda ya upendo usio na kikomo, vunjeni ardhi yenu isiyolimwa; kwa kuwa ni wakati wa kumtafuta Bwana, mpaka atakapokuja na kuwanyeshea juu yenu haki.
Jifanyieni haki, vuneni matunda ya uaminifu wa agano. Chimbueni ardhi yenu isiyopandwa, kwa maana ni wakati wa kumtafuta Bwana, mpaka atakapokuja na kuinua haki juu yenu.
13 Lakini mmepanda uovu, mkavuna ubaya, mmekula tunda la udanganyifu. Kwa sababu mmetegemea nguvu zenu wenyewe na wingi wa mashujaa wenu,
Mmelima uovu; mmevuna udhalimu. Mmekula matunda ya udanganyifu kwa sababu uliamini katika mipango yako na katika askari wako wengi.
14 mngurumo wa vita utainuka dhidi ya watu wako, ili kwamba ngome zako zote zitaharibiwa: kama Shalmani alivyoharibu Beth-Arbeli katika siku ile ya vita, wakati mama pamoja na watoto wao walipotupwa kwa nguvu ardhini.
Kwa hiyo mlipuko wa vita utafufuka kati ya watu wako, na miji yako yote yenye ngome itaharibiwa. Itakuwa kama Shalmani aliharibu Beth Arbeli siku ya vita, wakati mama alivunjika vipande vipande na watoto wake.
15 Ndivyo itakavyotokea kwako, ee Betheli, kwa sababu uovu wako ni mkuu. Siku ile itakapopambazuka, mfalme wa Israeli ataharibiwa kabisa.
Kwa hiyo itakuwa kwako, Betheli, kwa sababu ya uovu wako mkubwa. Wakati wa mchana mfalme wa Israeli atakatwa kabisa.

< Hosea 10 >