< Wahebrania 9 >
1 Basi agano lile la kwanza lilikuwa na kanuni zake za kuabudu na pia patakatifu pake pa kidunia.
之前的约定也有它敬拜的规例和现世的圣所。
2 Hema ilitengenezwa. Katika sehemu yake ya kwanza kulikuwa na kinara cha taa, meza na mikate iliyowekwa wakfu; hii sehemu iliitwa Mahali Patakatifu.
会幕的第一个房间里有烛台、桌子和圣饼。这被称为 “圣地。”。
3 Nyuma ya pazia la pili, palikuwa na sehemu iliyoitwa Patakatifu pa Patakatifu,
穿过圣幕的第二层帐幔进入的房间,叫作至圣所,
4 ambapo palikuwa na yale madhabahu ya dhahabu ya kufukizia uvumba, na lile Sanduku la Agano lililofunikwa kwa dhahabu. Sanduku hili lilikuwa na gudulia la dhahabu lenye mana, ile fimbo ya Aroni iliyochipuka, na vile vibao vya mawe vya Agano.
里面有金香坛,有全部包金的“约柜”,柜里有盛着吗哪的金罐、亚伦那曾发芽的手杖和两块石头约板。
5 Juu ya lile Sanduku kulikuwa na makerubi ya Utukufu yakitilia kivuli kile kifuniko ambacho ndicho kiti cha rehema. Lakini hatuwezi kueleza vitu hivi kwa undani sasa.
上面是荣耀的基路伯,罩着施恩座,关于这一切,现在不能一一细说了。
6 Basi vitu hivi vilipokuwa vimepangwa, makuhani waliingia daima katika sehemu ya kwanza ya hema ili kufanya taratibu zao za ibada.
这一切物件都这样预备好了,祭司会进入第一个圣幕房间,履行他的职责。
7 Lakini ni kuhani mkuu peke yake aliyeingia ndani ya sehemu ya pili ya hema. Tena hii ilikuwa mara moja tu kwa mwaka, na hakuingia kamwe bila damu, ambayo alitoa kwa ajili yake mwenyewe na kwa ajili ya dhambi za watu walizotenda bila kukusudia.
至于第二个房间,只有大祭司每年独自进去一起,他的祭祀还要带着血,为自己和人民的无知之罪之罪,把血献上。
8 Kwa njia hii, Roho Mtakatifu alikuwa anaonyesha kwamba, maadamu ile hema ya kwanza ilikuwa bado imesimama, njia ya kuingia Patakatifu pa Patakafifu ilikuwa bado haijafunguliwa.
圣灵借着这事表明,第一个圣地还存在的时候,进入至圣所的路,还没有显明出来。
9 Huu ulikuwa mfano kwa ajili ya wakati wa sasa, kuonyesha kwamba sadaka na dhabihu zilizokuwa zikitolewa hazikuweza kusafisha dhamiri ya mtu anayeabudu.
这是给我们现在人的一个例证,让我们看见所献的礼物和祭物不能让敬拜者的良心更清明。
10 Lakini hizi zilishughulika tu na vyakula na vinywaji, pamoja na taratibu mbalimbali za kunawa kwa nje, kanuni kwa ajili ya mwili zilizowekwa hadi wakati utimie wa matengenezo mapya.
它们只是宗教规定--关于食物和饮料,以及涉及清洗的各种仪式--这些规定是在神的新方式与他建立关系之前制定的。
11 Kristo alipokuja akiwa Kuhani Mkuu wa mambo mema ambayo tayari yameshawasili, alipitia kwenye hema iliyo kuu zaidi na bora zaidi, ambayo haikutengenezwa kwa mikono ya binadamu, hii ni kusema, ambayo si sehemu ya uumbaji huu.
基督已经来了,作了我们现在所拥有的美好事物的大祭司;他进入更伟大、更完备的礼拜堂,这并非人手所做,也是不属于这被创造的世界。
12 Hakuingia kwa njia ya damu ya mbuzi na ya ndama; lakini aliingia Patakatifu pa Patakatifu mara moja tu kwa damu yake mwenyewe, akiisha kupata ukombozi wa milele. (aiōnios )
他不是用山羊和牛犊的血进入,而是用自己的血。他只进入一次至圣所,就使我们永远自由。。 (aiōnios )
13 Damu ya mbuzi na ya mafahali, na majivu ya mitamba walivyonyunyiziwa wale waliokuwa najisi kwa taratibu za kiibada viliwatakasa, hata kuwaondolea uchafu wa nje.
即使是山羊和公牛的血或母牛的灰,洒在不洁的人身上,尚且可以使他们成为圣洁,身体洁净,
14 Basi ni zaidi aje damu ya Kristo, ambaye kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na waa, itatusafisha dhamiri zetu kutokana na matendo yaletayo mauti, ili tupate kumtumikia Mungu aliye hai! (aiōnios )
何况基督的血呢?他借着永远的灵,把自己无罪的生命献给上帝,他的血不是更能洁净我们的良心,脱离过往罪行,这样我们就可以事奉永生的上帝了? (aiōnios )
15 Kwa sababu hii Kristo ni mpatanishi wa agano jipya, ili kwamba wale walioitwa waweze kupokea ile ahadi ya urithi wa milele: kwa vile yeye alikufa awe ukombozi wao kutoka kwa dhambi walizozitenda chini ya agano la kwanza. (aiōnios )
因此,他作了新约定关系的中间人,借着他的死,救赎了人们在第一份约定关系中犯下的罪行,让那些蒙召之人,获得永远继承的承诺。 (aiōnios )
16 Kwa habari ya wosia, ni muhimu kuthibitisha kifo cha yule aliyeutoa,
凡要实施遗嘱,必须证实立遗嘱的人死了;
17 kwa sababu wosia huwa na nguvu tu wakati mtu ameshakufa; kamwe hauwezi kutumika wakati yule aliyeuandika bado yuko hai.
因为人死了,遗嘱才能确立,立遗嘱的人还活着的时候,遗嘱决不生效。
18 Hii ndiyo sababu hata lile agano la kwanza halikuweza kutekelezwa pasipo damu.
因此,第一份约定才会用血立下:
19 Mose alipotangaza kila amri kwa watu wote, alichukua damu ya ndama na ya mbuzi, pamoja na maji, sufu nyekundu na matawi ya mti wa hisopo, akanyunyizia kile kitabu na watu wote.
摩西按照律法,向所有人民宣布了各种诫命,就曾用牛犊和山羊的血和水,朱红色羊毛与牛膝草,洒在律法书和人民身上,
20 Alisema, “Hii ndiyo damu ya agano, ambalo Mungu amewaamuru kulitii.”
他对他们说:“这就是上帝告诉你们,他想要与你们立约的血。”
21 Vivyo hivyo alinyunyizia damu hiyo kwenye ile hema pamoja na kila kifaa kilichotumika ndani yake kwa taratibu za ibada.
他还把血洒在圣幕和各样敬拜使用的器皿上。
22 Kwa kweli sheria hudai kwamba, karibu kila kitu kitakaswe kwa damu, wala pasipo kumwaga damu, hakuna msamaha wa dhambi.
按着仪式的律法,几乎一切都要用血来洁净,如果没有流血,仪式上就无法洗刷罪恶的污点。
23 Kwa hiyo, ilikuwa muhimu kwa nakala za vitu vile vya mbinguni vitakaswe kwa dhabihu hizi, lakini vitu halisi vya mbinguni vilihitaji dhabihu bora kuliko hizi.
如果照着天堂的样子去做时必须这样洁净,天上的物体,就应该用更美的祭品去洁净。
24 Kwa maana Kristo hakuingia kwenye patakatifu palipofanywa kwa mikono ya mwanadamu, ambao ni mfano wa kile kilicho halisi. Yeye aliingia mbinguni penyewe, ili sasa aonekane mbele za Mungu kwa ajili yetu.
因为基督并未进如人手搭建的至圣所,那不过是原始建筑的模仿。基督进入了天堂,现在替我们说话,显露在上帝的面前。
25 Wala hakuingia mbinguni ili apate kujitoa mwenyewe mara kwa mara, kama vile kuhani mkuu aingiavyo Patakatifu pa Patakatifu kila mwaka kwa damu ambayo si yake mwenyewe.
他不必多次献上自己,好像大祭司每年进入至圣所,但他献祭的血并不是他自己的血。
26 Ingekuwa hivyo, ingempasa Kristo kuteswa mara nyingi tangu kuumbwa kwa ulimwengu. Lakini sasa ametokea mara moja tu katika mwisho wa nyakati aiondoe dhambi kwa kujitoa mwenyewe kuwa dhabihu. (aiōn )
如果这样,从创世以来,基督就该受过许多次苦了。并没有:就在这一次,在这当前时代的末期,他通过牺牲自己消除罪。 (aiōn )
27 Kama vile mwanadamu alivyowekewa kufa mara moja tu na baada ya kufa akabili hukumu,
正如人只死一次,然后被审判。
28 vivyo hivyo Kristo alitolewa mara moja tu kuwa dhabihu ili azichukue dhambi za watu wengi. Naye atakuja mara ya pili, sio kuchukua dhambi, bali kuwaletea wokovu wale wanaomngoja kwa shauku.
基督也是如此。他曾为消除很多人的罪而牺牲一次,他会再来,不是为了消除罪,而是为了拯救那些等待他的人。