< Wahebrania 7 >
1 Kwa kuwa huyu Melkizedeki alikuwa mfalme wa Salemu na kuhani wa Mungu Aliye Juu Sana. Alipokutana na Abrahamu akirudi kutoka kuwashinda hao wafalme, Melkizedeki alimbariki,
Jer ovaj Melhisedek bješe car Salimski, sveštenik Boga najvišega, koji srete Avraama kad se vraæaše s boja careva, i blagoslovi ga;
2 naye Abrahamu alimpa sehemu ya kumi ya kila kitu. Kwanza, jina hilo Melkizedeki maana yake ni “mfalme wa haki.” Na pia “mfalme wa Salemu” maana yake ni “mfalme wa amani.”
Kojemu i Avraam dade desetak od svega. Prvo dakle znaèi car pravde, potom i car Salimski, to jest car mira;
3 Hana Baba wala mama, hana ukoo, hana mwanzo wala mwisho wa siku zake. Kama Mwana wa Mungu, yeye adumu akiwa kuhani milele.
Bez oca, bez matere, bez roda, ne imajuæi ni poèetka danima, ni svršetka životu, a isporeðen sa sinom Božijim, i ostaje sveštenik dovijeka.
4 Tazama jinsi alivyokuwa mkuu: Hata Abrahamu, baba yetu mkuu, alimpa sehemu ya kumi ya nyara zake.
Ali pogledajte koliki je ovaj kome je i Avraam patrijarh dao desetak od plijena.
5 Basi sheria inawaagiza wana wa Lawi ambao hufanyika makuhani kupokea sehemu ya kumi kutoka kwa watu ambao ni ndugu zao, ingawa ndugu zao ni wazao wa Abrahamu.
Istina, i oni od sinova Levijevijeh koji primiše sveštenstvo, imaju zapovijest da uzimaju po zakonu desetak od naroda, to jest braæe svoje, ako su i izišli iz bedara Avraamovijeh.
6 Huyu Melkizedeki, ingawa hakufuatia ukoo wake kutoka kwa Lawi, lakini alipokea sehemu ya kumi kutoka kwa Abrahamu na kumbariki yeye aliyekuwa na zile ahadi.
Ali onaj koji se ne broji od njihova roda, uze desetak od Avraama, i blagoslovi onoga koji ima obeæanje.
7 Wala hakuna shaka kwamba mdogo hubarikiwa na aliye mkuu kumliko yeye.
Ali bez svakoga izgovora manje blagoslovi veæe.
8 Kwa upande mmoja, sehemu ya kumi hupokelewa na wale ambao hupatikana na kufa; lakini kwa upande mwingine hupokelewa na yeye ambaye hushuhudiwa kuwa yu hai.
I tako ovdje uzimaju desetak ljudi koji umiru, a onamo onaj za kojega se posvjedoèi da živi.
9 Mtu anaweza hata kusema kwamba Lawi, ambaye hupokea sehemu ya kumi, alitoa hiyo sehemu ya kumi kupitia kwa Abrahamu,
I, da ovako reèem, Levije koji uze desetak, dao je desetak kroz Avraama:
10 kwa sababu Melkizedeki alipokutana na Abrahamu, Lawi alikuwa bado katika viuno vya baba yake wa zamani.
Jer bijaše još u bedrima oèinima kad ga srete Melhisedek.
11 Kama ukamilifu ungeweza kupatikana kwa njia ya ukuhani wa Walawi (kwa kuwa katika msingi huo, sheria ilitolewa kwa watu), kwa nini basi imekuwepo haja ya kuja kuhani mwingine: kuhani kwa mfano wa Melkizedeki, wala si kwa mfano wa Aroni?
Ako je dakle savršenstvo postalo kroz Levitsko sveštenstvo jer je narod pod njim zakon primio kaka je još potreba bila govoriti da æe drugi sveštenik postati po redu Melhisedekovu a ne po redu Aronovu?
12 Kwa kuwa yanapotokea mabadiliko ya ukuhani, pia lazima yawepo mabadiliko ya sheria.
Jer kad se promijeni sveštenstvo, mora se i zakon promijeniti.
13 Yeye ambaye mambo haya yanasemwa alikuwa wa kabila lingine, na hakuna mtu wa kabila hilo aliyewahi kuhudumu katika madhabahu.
Jer za koga se ovo govori on je od drugoga koljena, od kojega niko ne pristupi k oltaru.
14 Kwa maana ni dhahiri kwamba Bwana wetu alitoka katika uzao wa Yuda, tena kuhusu kabila hilo Mose hakusema lolote kwa habari za makuhani.
Jer je poznato da Gospod naš od koljena Judina iziðe, za koje koljeno Mojsije ne govori ništa o sveštenstvu.
15 Tena hayo tuliyosema yako wazi zaidi kama akitokea kuhani mwingine kama Melkizedeki,
I još je više poznato da æe po redu Melhisedekovu drugi sveštenik postati,
16 yeye ambaye amefanyika kuhani si kwa misingi ya sheria kama ilivyokuwa kwa baba zake, bali kwa misingi ya uwezo wa uzima usioharibika.
Koji nije postao po zakonu tjelesne zapovijesti nego po sili života vjeènoga.
17 Kwa maana imeshuhudiwa kwamba: “Wewe ni kuhani milele, kwa mfano wa Melkizedeki.” (aiōn )
Jer svjedoèi: ti si sveštenik vavijek po redu Melhisedekovu. (aiōn )
18 Kwa upande mmoja, ile amri ya mwanzo isiyofaa na dhaifu imebatilishwa
Tako se ukida preðašnja zapovijest, što bi slaba i zaludna.
19 (kwa maana sheria haikufanya kitu chochote kuwa kikamilifu). Kwa upande mwingine, tumeletewa tumaini lililo bora zaidi ambalo linatuleta karibu na Mungu.
Jer zakon nije ništa savršio; a postavi bolji nad, kroz koji se približujemo k Bogu.
20 Nalo tumaini hilo halikutolewa pasipo kiapo! Wengine walikuwa makuhani pasipo kiapo chochote,
I još ne bez zakletve;
21 lakini Yesu alifanywa kuhani kwa kiapo wakati Mungu alimwambia: “Bwana ameapa naye hatabadilisha mawazo yake: ‘Wewe ni kuhani milele.’” (aiōn )
Jer oni bez zakletve postaše sveštenici; a ovaj sa zakletvom kroz onoga koji mu govori: zakle se Gospod i neæe se raskajati: ti si sveštenik vavijek po redu Melhisedekovu. (aiōn )
22 Kwa ajili ya kiapo hiki, Yesu amekuwa mdhamini wa agano lililo bora zaidi.
Toliko boljega zavjeta posta Isus jamac.
23 Basi pamekuwepo na makuhani wengi wa aina hiyo, kwa kuwa kifo kiliwazuia kuendelea na huduma yao ya ukuhani.
I oni mnogi biše sveštenici, jer im smrt ne dade da ostanu.
24 Lakini kwa sababu Yesu anaishi milele, anao ukuhani wa kudumu. (aiōn )
A ovaj, buduæi da ostaje vavijek, ima vjeèno sveštenstvo. (aiōn )
25 Kwa hiyo anaweza kuwaokoa kabisa wale wanaomjia Mungu kupitia kwake, kwa sababu yeye adumu daima kuomba kwa ajili yao.
Zato i može vavijek spasti one koji kroza nj dolaze k Bogu, kad svagda živi da se može moliti za njih.
26 Kwa kuwa ilitupasa tuwe na Kuhani Mkuu wa namna hii, yaani, aliye mtakatifu, asiye na lawama, asiye na dosari, aliyetengwa na wenye dhambi na kuinuliwa juu ya mbingu.
Jer takov nama trebaše poglavar sveštenièki: svet, bezazlen, èist, odvojen od grješnika, i koji je bio više nebesa;
27 Yeye hahitaji kutoa dhabihu siku kwa siku kwa ajili ya dhambi, kwanza kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe, kisha kwa ajili ya dhambi za watu kama wale makuhani wakuu wengine. Yeye alitoa dhabihu kwa ajili ya dhambi zao mara moja tu, alipojitoa mwenyewe.
Kojemu nije potrebno svaki dan, kao sveštenicima, najprije za svoje grijehe žrtve prinositi, a potom za narodne, jer on ovo uèini jednom, kad sebe prinese.
28 Kwa kuwa sheria huwaweka makuhani wakuu watu ambao ni dhaifu; lakini lile neno la kiapo, lililokuja baada ya sheria, lilimweka Mwana, ambaye amefanywa kuwa mkamilifu milele. (aiōn )
Jer zakon postavlja ljude za sveštenike koji imaju slabost; a rijeè zakletve koja je reèena po zakonu, postavi sina vavijek savršena. (aiōn )