< Wahebrania 3 >

1 Kwa hiyo ndugu watakatifu, mnaoshiriki mwito wa mbinguni, mtafakarini Yesu, mtume na Kuhani Mkuu wa ukiri wetu.
Therefore, holy brothers, partakers of a heavenly calling, consider the Apostle and High Priest of our confession: Jesus,
2 Alikuwa mwaminifu kwa yeye aliyemweka, kama vile Mose alivyokuwa mwaminifu katika nyumba yote ya Mungu.
who was faithful to him who appointed him, as also Moses was in all his house.
3 Yesu ameonekana anastahili heshima kubwa kuliko Mose, kama vile mjenzi wa nyumba alivyo wa heshima kubwa kuliko nyumba yenyewe.
For he has been counted worthy of more glory than Moses, because he who built the house has more honor than the house.
4 Kwa kuwa kila nyumba hujengwa na mtu fulani, lakini Mungu ni mjenzi wa kila kitu.
For every house is built by someone; but he who built all things is God.
5 Basi Mose kama mtumishi alikuwa mwaminifu katika nyumba yote ya Mungu, akishuhudia kwa yale ambayo yangetamkwa baadaye.
Moses indeed was faithful in all his house as a servant, for a testimony of those things which were afterward to be spoken,
6 Lakini Kristo ni mwaminifu kama Mwana katika nyumba ya Mungu. Sisi ndio nyumba yake, kama tutashikilia sana ujasiri wetu na tumaini tunalojivunia.
but Christ is faithful as a Son over his house. We are his house, if we hold fast our confidence and the glorying of our hope firm to the end.
7 Kwa hiyo, kama Roho Mtakatifu asemavyo: “Leo, kama mkiisikia sauti yake,
Therefore, even as the Holy Spirit says, “Today if you will hear his voice,
8 msiifanye mioyo yenu migumu, kama mlivyofanya katika uasi, wakati ule wa kujaribiwa jangwani,
do not harden your hearts as in the rebellion, in the day of the trial in the wilderness,
9 ambapo baba zenu walinijaribu na kunipima ingawa kwa miaka arobaini walikuwa wameyaona matendo yangu.
where your fathers tested me and tried me, and saw my deeds for forty years.
10 Hiyo ndiyo sababu nilikasirikia kizazi kile, nami nikasema, ‘Siku zote mioyo yao imepotoka, nao hawajazijua njia zangu.’
Therefore I was displeased with that generation, and said, ‘They always err in their heart, but they did not know my ways.’
11 Hivyo nikatangaza kwa kiapo katika hasira yangu, ‘Kamwe hawataingia rahani mwangu.’”
As I swore in my wrath, ‘They will not enter into my rest.’”
12 Ndugu zangu, angalieni, asiwepo miongoni mwenu mtu mwenye moyo mwovu usioamini, unaojitenga na Mungu aliye hai.
Beware, brothers, lest perhaps there might be in any one of you an evil heart of unbelief, in falling away from the living God;
13 Lakini mtiane moyo mtu na mwenzake kila siku, maadamu iitwapo Leo, ili asiwepo hata mmoja wenu mwenye kufanywa mgumu kwa udanganyifu wa dhambi.
but exhort one another day by day, so long as it is called “today”, lest any one of you be hardened by the deceitfulness of sin.
14 Kwa kuwa tumekuwa washiriki wa Kristo, kama tukishikamana tu kwa uthabiti na tumaini letu la kwanza hadi mwisho.
For we have become partakers of Christ, if we hold the beginning of our confidence firm to the end,
15 Kama ilivyonenwa: “Leo, kama mkiisikia sauti yake, msiifanye mioyo yenu migumu kama mlivyofanya wakati wa kuasi.”
while it is said, “Today if you will hear his voice, do not harden your hearts, as in the rebellion.”
16 Basi ni nani waliosikia lakini bado wakaasi? Je, si wale wote waliotoka Misri wakiongozwa na Mose?
For who, when they heard, rebelled? Was not it all those who came out of Egypt led by Moses?
17 Lakini ni nani aliowakasirikia miaka arobaini? Je, si wale waliofanya dhambi ambao miili yao ilianguka jangwani?
With whom was he displeased forty years? Was not it with those who sinned, whose bodies fell in the wilderness?
18 Ni nani hao ambao Mungu aliapa kuwa kamwe hawataingia rahani mwake isipokuwa ni wale waliokataa kutii?
To whom did he swear that they would not enter into his rest, but to those who were disobedient?
19 Hivyo tunaona kwamba hawakuweza kuingia kwa sababu ya kutokuamini kwao.
We see that they were not able to enter in because of unbelief.

< Wahebrania 3 >