< Wahebrania 13 >

1 Endeleeni kupendana kama ndugu.
Let brotherly love continue.
2 Msisahau kuwakaribisha wageni, kwa kuwa kwa kufanya hivyo, watu wengine waliwakaribisha malaika pasipo kujua.
Don’t forget to show hospitality to strangers, for in doing so, some have entertained angels without knowing it.
3 Wakumbukeni wale waliofungwa gerezani kana kwamba ninyi mmefungwa pamoja nao. Pia wakumbukeni wale wanaotendewa vibaya, kana kwamba ni ninyi wenyewe mnateswa.
Remember those who are in bonds, as bound with them, and those who are ill-treated, since you are also in the body.
4 Ndoa na iheshimiwe na watu wote, nayo malazi yawe safi, kwa kuwa Mungu atawahukumu wazinzi na waasherati wote.
Let marriage be held in honor among all, and let the bed be undefiled; but God will judge the sexually immoral and adulterers.
5 Yalindeni maisha yenu msiwe na tabia ya kupenda fedha, bali mridhike na vile mlivyo navyo, kwa sababu Mungu amesema, “Kamwe sitakuacha, wala sitakupungukia.”
Be free from the love of money, content with such things as you have, for he has said, “I will in no way leave you, neither will I in any way forsake you.”
6 Kwa hiyo tunaweza kusema kwa ujasiri, “Bwana ni msaada wangu; sitaogopa. Mwanadamu anaweza kunitenda nini?”
So that with good courage we say, “The Lord is my helper. I will not fear. What can man do to me?”
7 Wakumbukeni viongozi wenu, wale waliowaambia neno la Mungu. Angalieni matokeo ya mwenendo wa maisha yao mkaiige imani yao.
Remember your leaders, men who spoke to you the word of God, and considering the results of their conduct, imitate their faith.
8 Yesu Kristo ni yeye yule jana, leo na hata milele. (aiōn g165)
Jesus Christ is the same yesterday, today, and forever. (aiōn g165)
9 Msichukuliwe na kila aina ya mafundisho ya kigeni. Ni vyema mioyo yenu iimarishwe kwa neema, wala si kwa sheria kuhusu utaratibu wa vyakula, ambavyo havina faida kwa wale wanaozishika hizo sheria.
Don’t be carried away by various and strange teachings, for it is good that the heart be established by grace, not by foods, through which those who were so occupied were not benefited.
10 Sisi tunayo madhabahu ambayo wale wanaohudumu katika hema hawana haki ya kula vile vitu vilivyowekwa juu yake.
We have an altar from which those who serve the holy tabernacle have no right to eat.
11 Kuhani mkuu huchukua damu ya wanyama na kuiingiza Patakatifu pa Patakatifu, kama sadaka ya dhambi, lakini miili ya hao wanyama huteketezwa nje ya kambi.
For the bodies of those animals, whose blood is brought into the holy place by the high priest as an offering for sin, are burned outside of the camp.
12 Vivyo hivyo, Yesu naye aliteswa nje ya lango la mji ili awatakase watu kwa damu yake mwenyewe.
Therefore Jesus also, that he might sanctify the people through his own blood, suffered outside of the gate.
13 Kwa hiyo, basi na tumwendee nje ya kambi, tukiichukua aibu aliyobeba.
Let’s therefore go out to him outside of the camp, bearing his reproach.
14 Kwa kuwa hapa hatuna mji udumuo, bali tunautafuta ule ujao.
For we don’t have here an enduring city, but we seek that which is to come.
15 Basi kwa njia ya Yesu, tuzidi kumtolea Mungu dhabihu ya sifa, yaani matunda ya midomo inayolikiri Jina lake.
Through him, then, let’s offer up a sacrifice of praise to God continually, that is, the fruit of lips which proclaim allegiance to his name.
16 Na msiache kutenda mema na kushirikiana vile vitu mlivyo navyo, kwa kuwa dhabihu kama hizo ndizo zinazompendeza Mungu.
But don’t forget to be doing good and sharing, for with such sacrifices God is well pleased.
17 Watiini viongozi wenu na kujinyenyekeza chini ya mamlaka yao. Kwa maana wao wanakesha kwa ajili yenu kama watu watakaopaswa kutoa hesabu. Watiini ili wafanye kazi yao kwa furaha, wala si kama mzigo, maana hiyo haitakuwa na faida kwenu.
Obey your leaders and submit to them, for they watch on behalf of your souls, as those who will give account, that they may do this with joy and not with groaning, for that would be unprofitable for you.
18 Tuombeeni. Tuna hakika kuwa tunayo dhamiri safi na shauku ya kuishi kwa uadilifu kwa kila njia.
Pray for us, for we are persuaded that we have a good conscience, desiring to live honorably in all things.
19 Ninawasihi zaidi mniombee ili nipate kurudishwa kwenu upesi.
I strongly urge you to do this, that I may be restored to you sooner.
20 Basi Mungu wa amani, ambaye kwa damu ya Agano la milele alimleta tena kutoka kwa wafu Bwana wetu Yesu, yule Mchungaji Mkuu wa kondoo, (aiōnios g166)
Now may the God of peace, who brought again from the dead the great shepherd of the sheep with the blood of an eternal covenant, our Lord Jesus, (aiōnios g166)
21 awafanye ninyi wakamilifu mkiwa mmekamilishwa katika kila jambo jema ili mpate kutenda mapenzi yake, naye atende ndani yetu kile kinachompendeza machoni Pake, kwa njia ya Yesu Kristo, ambaye utukufu una yeye milele na milele. Amen. (aiōn g165)
make you complete in every good work to do his will, working in you that which is well pleasing in his sight, through Jesus Christ, to whom be the glory forever and ever. Amen. (aiōn g165)
22 Ndugu zangu, nawasihi mchukuliane na maneno yangu ya maonyo, kwa kuwa nimewaandikia waraka mfupi tu.
But I exhort you, brothers, endure the word of exhortation, for I have written to you in few words.
23 Nataka ninyi mjue kwamba ndugu yetu Timotheo amefunguliwa kutoka gerezani. Akifika mapema, nitakuja pamoja naye kuwaona.
Know that our brother Timothy has been freed, with whom, if he comes shortly, I will see you.
24 Wasalimuni viongozi wenu wote na watakatifu wote. Wale wa kutoka Italia wanawasalimu.
Greet all of your leaders and all the saints. The Italians greet you.
25 Neema iwe nanyi nyote. Amen.
Grace be with you all. Amen.

< Wahebrania 13 >