< Habakuki 3 >

1 Sala ya nabii Habakuki iliyoimbwa kwa shigionothi.
תפלה לחבקוק הנביא על שגינות׃
2 Bwana, nimezisikia sifa zako; nami naogopa kwa matendo yako, Ee Bwana. Fufua kazi yako katikati ya miaka, katikati ya miaka tangaza habari yako; katika ghadhabu kumbuka rehema.
יהוה שמעתי שמעך יראתי יהוה פעלך בקרב שנים חייהו בקרב שנים תודיע ברגז רחם תזכור׃
3 Mungu alitoka Temani, yeye Aliye Mtakatifu kutoka Mlima Parani. Utukufu wake ulifunika mbingu, na sifa zake zikaifunika dunia.
אלוה מתימן יבוא וקדוש מהר פארן סלה כסה שמים הודו ותהלתו מלאה הארץ׃
4 Mngʼao wake ulikuwa kama jua lichomozalo; mionzi ilimulika kutoka mkononi mwake, ambako nguvu zake zilifichwa.
ונגה כאור תהיה קרנים מידו לו ושם חביון עזה׃
5 Tauni ilimtangulia; maradhi ya kuambukiza yalifuata nyayo zake.
לפניו ילך דבר ויצא רשף לרגליו׃
6 Alisimama, akaitikisa dunia; alitazama, na kuyafanya mataifa yatetemeke. Milima ya zamani iligeuka mavumbi na vilima vilivyozeeka vikaanguka. Njia zake ni za milele.
עמד וימדד ארץ ראה ויתר גוים ויתפצצו הררי עד שחו גבעות עולם הליכות עולם לו׃
7 Niliona watu wa Kushani katika dhiki, na makazi ya Midiani katika maumivu makali.
תחת און ראיתי אהלי כושן ירגזון יריעות ארץ מדין׃
8 Ee Bwana, uliikasirikia mito? Je, ghadhabu yako ilikuwa dhidi ya vijito? Je, ulighadhibikia bahari ulipoendesha farasi wako na magari yako ya ushindi?
הבנהרים חרה יהוה אם בנהרים אפך אם בים עברתך כי תרכב על סוסיך מרכבתיך ישועה׃
9 Uliufunua upinde wako na kuita mishale mingi. Uliigawa dunia kwa mito;
עריה תעור קשתך שבעות מטות אמר סלה נהרות תבקע ארץ׃
10 milima ilikuona ikatetemeka. Mafuriko ya maji yakapita huko; vilindi vilinguruma na kuinua mawimbi yake juu.
ראוך יחילו הרים זרם מים עבר נתן תהום קולו רום ידיהו נשא׃
11 Jua na mwezi vilisimama kimya mbinguni katika mngʼao wa mishale yako inayoruka, na katika mngʼao wa mkuki wako umeremetao.
שמש ירח עמד זבלה לאור חציך יהלכו לנגה ברק חניתך׃
12 Kwa ghadhabu ulipita juu ya dunia, na katika hasira ulikanyaga mataifa.
בזעם תצעד ארץ באף תדוש גוים׃
13 Ulikuja kuwaokoa watu wako, kumwokoa uliyemtia mafuta. Ulimponda kiongozi wa nchi ya uovu, ukamvua toka kichwani hadi wayo.
יצאת לישע עמך לישע את משיחך מחצת ראש מבית רשע ערות יסוד עד צואר סלה׃
14 Kwa mkuki wake mwenyewe ulitoboa kichwa chake wakati mashujaa wake walifurika nje kwa kishindo kututawanya, wakifurahi kama walio karibu kutafuna wale wanyonge waliokuwa mafichoni.
נקבת במטיו ראש פרזו יסערו להפיצני עליצתם כמו לאכל עני במסתר׃
15 Ulikanyaga bahari kwa farasi wako, ukisukasuka maji makuu.
דרכת בים סוסיך חמר מים רבים׃
16 Nilisikia na moyo wangu ukagonga kwa nguvu, midomo yangu ikatetemeka kwa hofu niliposikia sauti; uchakavu ukanyemelea mifupa yangu, na miguu yangu ikatetemeka. Hata hivyo nitasubiri kwa uvumilivu siku ya maafa kuyajilia mataifa yaliyotuvamia.
שמעתי ותרגז בטני לקול צללו שפתי יבוא רקב בעצמי ותחתי ארגז אשר אנוח ליום צרה לעלות לעם יגודנו׃
17 Ingawa mtini hauchanui maua na hakuna zabibu juu ya mizabibu, ingawaje mzeituni hauzai, na hata mashamba hayatoi chakula, iwapo hakuna kondoo katika banda, wala ngʼombe katika zizi,
כי תאנה לא תפרח ואין יבול בגפנים כחש מעשה זית ושדמות לא עשה אכל גזר ממכלה צאן ואין בקר ברפתים׃
18 hata hivyo nitashangilia katika Bwana, nitamfurahia Mungu Mwokozi wangu.
ואני ביהוה אעלוזה אגילה באלהי ישעי׃
19 Bwana Mwenyezi ni nguvu yangu; huifanya miguu yangu kama miguu ya ayala, huniwezesha kupita juu ya vilima. Kwa kiongozi wa uimbaji. Kwa vinanda vyangu vya nyuzi.
יהוה אדני חילי וישם רגלי כאילות ועל במותי ידרכני למנצח בנגינותי׃

< Habakuki 3 >