< Habakuki 2 >
1 Nitasimama katika zamu yangu, na kujiweka mwenyewe juu ya maboma; nitatazama nione atakaloniambia, na ni jibu gani nitakalotoa kuhusu lalamiko hili.
I will stand on my watch-tower, And set myself on the bulwark, And watch to see what he will say to me, And what I shall answer to my expostulation.
2 Kisha Bwana akajibu: “Andika ufunuo huu, na ukaufanye wazi juu ya vibao, ili mpiga mbiu akimbie nao.
And Jehovah answered me, and said, Write the vision, and make it plain upon tablets, That he may run that readeth it.
3 Kwa kuwa ufunuo huu unasubiri wakati uliokubalika; unazungumzia mambo ya mwisho, na kamwe hautakosea. Iwapo utakawia, wewe usubiri; kwa hakika utakuja na hautachelewa.
For the vision is yet for an appointed time, But it hasteneth to the end; it shall not deceive; If it tarry, wait for it; For it shall surely come; it shall not long delay.
4 “Tazama, amejaa majivuno; anavyovitamani si vya unyofu: lakini mwenye haki ataishi kwa imani yake:
Behold, the soul of him that is puffed up shall not be at ease; But the just shall live by his faithfulness.
5 hakika mvinyo humsaliti; ni mwenye kiburi na hana amani. Kwa sababu ni mlafi kama kuzimu na kama kifo kamwe hatosheki; anajikusanyia mataifa yote na kuchukua watu wote mateka. (Sheol )
Behold, the man of wine is outrageous; The proud man remaineth not at rest; He enlargeth his desire as the grave; He is as death, and cannot be satisfied; He gathereth to himself all the nations, And collecteth to himself all the kingdoms. (Sheol )
6 “Je, watu wote hawatamsuta kwa dhihaka na kumbeza, wakisema, “‘Ole wake yeye akusanyaye bidhaa zilizoibwa na kujifanyia utajiri kwa kutoza kwa nguvu! Ataendelea hivi kwa muda gani?’
Shall not all of them utter a song against him, Yea, songs of reproach and derision concerning him? And say, Woe to him that heapeth up that which belongeth not to him! For how long a time? That ladeth himself with goods taken in pledge!
7 Je, wadai wako hawatainuka ghafula? Je, hawataamka na kukufanya utetemeke? Kisha utakuwa mhanga kwao.
Shall not they suddenly rise up that will oppress thee, And awake, that will harass thee? Yea, thou shalt be their booty.
8 Kwa kuwa umeteka nyara mataifa mengi, watu waliobaki watakuteka nyara wewe. Kwa kuwa umemwaga damu ya mtu; umeharibu nchi na miji, na kila mmoja ndani yake.
Because thou hast plundered many kingdoms, All the residue of the nations shall plunder thee: For the blood of men, and for violence against the land, Against the city and all its inhabitants.
9 “Ole wake yeye ajengaye milki yake kwa mapato ya udhalimu, awekaye kiota chake juu, ili kukimbia makucha ya uharibifu!
Woe to him that procureth unjust gain for his house, That he may set his nest on high, That he may be delivered from the evil hand!
10 Umefanya shauri la maangamizi ya watu wengi, ukiaibisha nyumba yako mwenyewe, na kupotewa na maisha yako.
Thou hast devised shame for thine house; By destroying many nations, thou hast brought ruin upon thyself.
11 Mawe ya kuta yatapiga kelele, na mihimili ya kazi ya mbao itarudisha mwangwi wake.
For the stone from the wall crieth out, And the beam from the timber answereth it.
12 “Ole wake yeye ajengaye mji kwa kumwaga damu na kuusimamisha mji kwa uhalifu!
Woe to him that buildeth a town by blood, And establisheth a city by iniquity!
13 Je, Bwana Mwenye Nguvu Zote hakuonyesha kwamba kazi ya wanadamu ni mafuta tu kwa ajili ya moto, na kwamba mataifa yanajichosha bure?
Behold, it is determined by Jehovah of hosts, That nations shall labor for the fire, And kingdoms weary themselves for naught.
14 Kwa kuwa dunia itajazwa na maarifa ya utukufu wa Bwana, kama maji yaifunikavyo bahari.
For the earth shall be filled with the knowledge of the glory of Jehovah, As the waters cover the sea.
15 “Ole wake yeye awapaye jirani zake kileo, akiimimina kutoka kwenye kiriba cha mvinyo mpaka wamelewa, ili apate kutazama miili yao iliyo uchi.
Woe to him who giveth his neighbor drink; Who poureth out the strong wine, and maketh him drunken, That he may look upon his nakedness!
16 Utajazwa na aibu badala ya utukufu. Sasa ni zamu yako! Kunywa na ujifunue! Kikombe kutoka kwenye mkono wa kuume wa Bwana kinakujia, na aibu itafunika utukufu wako.
Thou shalt be filled with shame instead of glory; Drink thou also, and show thy foreskin! To thee shall come the cup in the right hand of Jehovah, And foul shame shall be upon thy glory.
17 Ukatili ulioifanyia Lebanoni utakufunika, na uharibifu uliowafanyia wanyama utakutisha. Kwa sababu umemwaga damu ya mtu; umeharibu nchi na miji na kila mmoja aliyeko ndani yake.
For the violence done to Lebanon shall cover thee, And the destruction of the beasts which made them afraid, On account of the blood of men, and violence against the land, Against the city and all its inhabitants.
18 “Sanamu ina thamani gani, kwani mwanadamu ndiye alichonga? Ama kinyago kinachofundisha uongo? Kwa kuwa yeye aliyekitengeneza hutegemea kazi ya mikono yake mwenyewe; hutengeneza sanamu zisizoweza kuzungumza.
What profiteth the graven image, When the maker hath graven it? Or the molten image, and the teacher of lies, That the artificer trusteth in his work, When he maketh dumb idols?
19 Ole wake yeye auambiaye mti, ‘Uwe hai!’ Ama asemaye na jiwe lisilo na uhai, ‘Amka!’ Je, linaweza kuongoza? Limefunikwa kwa dhahabu na fedha; hakuna pumzi ndani yake.
Woe to him who saith to the wood, Awake! To the dumb stone, Arise! Will it teach? Behold, it is overlaid with gold and silver, And there is no breath within it.
20 Lakini Bwana yuko katika Hekalu lake takatifu; dunia yote na inyamaze mbele yake.”
But Jehovah is in his Holy temple; Be silent before him, all the earth!