< Mwanzo 9 >

1 Ndipo Mungu akambariki Noa na wanawe, akiwaambia, “Zaeni mkaongezeke kwa idadi na mkaijaze tena dunia.
ויברך אלהים את נח ואת בניו ויאמר להם פרו ורבו ומלאו את הארץ
2 Wanyama wote wa duniani, ndege wote wa angani, kila kiumbe kitambaacho juu ya ardhi, na samaki wote wa baharini wamekabidhiwa mikononi mwenu, nao watawaogopa na kuwahofu.
ומוראכם וחתכם יהיה על כל חית הארץ ועל כל עוף השמים בכל אשר תרמש האדמה ובכל דגי הים בידכם נתנו
3 Kila kitu chenye uhai kiendacho kitakuwa chakula chenu. Kama vile nilivyowapa mimea mbalimbali, sasa nawapa kila kitu.
כל רמש אשר הוא חי לכם יהיה לאכלה כירק עשב נתתי לכם את כל
4 “Lakini kamwe msile nyama ambayo bado ina damu ya uhai wake, kwa maana damu ni uhai.
אך בשר בנפשו דמו לא תאכלו
5 Hakika damu ya uhai wenu nitaidai. Nitaidai kutoka kwa kila mnyama. Kutoka kwa kila mwanadamu pia nitaidai kwa ajili ya uhai wa mtu mwenzake.
ואך את דמכם לנפשתיכם אדרש מיד כל חיה אדרשנו ומיד האדם מיד איש אחיו--אדרש את נפש האדם
6 “Yeyote amwagaye damu ya mwanadamu, damu yake itamwagwa na mwanadamu, kwa kuwa katika mfano wa Mungu, Mungu alimuumba mwanadamu.
שפך דם האדם באדם דמו ישפך כי בצלם אלהים עשה את האדם
7 Kuhusu ninyi, zaeni mwongezeke kwa wingi, mzidi katika dunia na kuijaza.”
ואתם פרו ורבו שרצו בארץ ורבו בה
8 Ndipo Mungu akamwambia Noa na wanawe pamoja naye:
ויאמר אלהים אל נח ואל בניו אתו לאמר
9 “Sasa mimi ninaweka Agano langu nanyi, pamoja na uzao wenu baada yenu,
ואני הנני מקים את בריתי אתכם ואת זרעכם אחריכם
10 pia na kila kiumbe hai kilichokuwa pamoja nanyi: Ndege, wanyama wa kufugwa na wanyama wote wa porini, wale wote waliotoka katika safina pamoja nanyi, kila kiumbe hai duniani.
ואת כל נפש החיה אשר אתכם בעוף בבהמה ובכל חית הארץ אתכם מכל יצאי התבה לכל חית הארץ
11 Ninaweka Agano nanyi: Kamwe uhai hautafutwa tena kwa gharika, kamwe haitakuwepo tena gharika ya kuangamiza dunia.”
והקמתי את בריתי אתכם ולא יכרת כל בשר עוד ממי המבול ולא יהיה עוד מבול לשחת הארץ
12 Mungu akasema, “Hii ni ishara ya Agano ninalofanya kati yangu na ninyi na kila kiumbe hai kilicho pamoja nanyi, Agano kwa vizazi vyote vijavyo:
ויאמר אלהים זאת אות הברית אשר אני נתן ביני וביניכם ובין כל נפש חיה אשר אתכם--לדרת עולם
13 Nimeweka upinde wangu wa mvua mawinguni, nao utakuwa ishara ya Agano nifanyalo kati yangu na dunia.
את קשתי נתתי בענן והיתה לאות ברית ביני ובין הארץ
14 Wakati wowote ninapotanda mawingu juu ya dunia na upinde wa mvua ukijitokeza mawinguni,
והיה בענני ענן על הארץ ונראתה הקשת בענן
15 nitakumbuka Agano langu kati yangu na ninyi na viumbe vyote vilivyo hai vya kila aina. Kamwe maji hayatakuwa tena gharika ya kuangamiza uhai wote.
וזכרתי את בריתי אשר ביני וביניכם ובין כל נפש חיה בכל בשר ולא יהיה עוד המים למבול לשחת כל בשר
16 Wakati wowote upinde wa mvua unapotokea mawinguni, nitauona na kukumbuka Agano la milele kati ya Mungu na viumbe vyote vilivyo hai vya kila aina duniani.”
והיתה הקשת בענן וראיתיה לזכר ברית עולם בין אלהים ובין כל נפש חיה בכל בשר אשר על הארץ
17 Hivyo Mungu akamwambia Noa, “Hii ndiyo ishara ya Agano ambalo nimelifanya kati yangu na viumbe vyote vilivyo hai duniani.”
ויאמר אלהים אל נח זאת אות הברית אשר הקמתי ביני ובין כל בשר אשר על הארץ
18 Wana wa Noa waliotoka ndani ya safina ni: Shemu, Hamu na Yafethi. (Hamu ndiye alikuwa baba wa Kanaani.)
ויהיו בני נח היצאים מן התבה--שם וחם ויפת וחם הוא אבי כנען
19 Hawa ndio waliokuwa wana watatu wa Noa, kutokana nao watu walienea katika dunia.
שלשה אלה בני נח ומאלה נפצה כל הארץ
20 Noa akawa mkulima, akawa mtu wa kwanza kupanda mizabibu.
ויחל נח איש האדמה ויטע כרם
21 Alipokunywa huo mvinyo wake akalewa na akalala uchi kwenye hema lake.
וישת מן היין וישכר ויתגל בתוך אהלה
22 Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake na kuwaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje.
וירא חם אבי כנען את ערות אביו ויגד לשני אחיו בחוץ
23 Lakini Shemu na Yafethi wakachukua nguo wakaitanda mabegani mwao wote wawili, kisha wakaenda kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao. Nyuso zao zilielekea upande mwingine ili wasiuone uchi wa baba yao.
ויקח שם ויפת את השמלה וישימו על שכם שניהם וילכו אחרנית ויכסו את ערות אביהם ופניהם אחרנית וערות אביהם לא ראו
24 Noa alipolevuka kutoka kwenye mvinyo wake na kujua lile ambalo mwanawe mdogo kuliko wote alilokuwa amemtendea,
וייקץ נח מיינו וידע את אשר עשה לו בנו הקטן
25 akasema, “Alaaniwe Kanaani! Atakuwa mtumwa wa chini sana kuliko watumwa wote kwa ndugu zake.”
ויאמר ארור כנען עבד עבדים יהיה לאחיו
26 Pia akasema, “Abarikiwe Bwana, Mungu wa Shemu! Kanaani na awe mtumwa wa Shemu.
ויאמר ברוך יהוה אלהי שם ויהי כנען עבד למו
27 Mungu na apanue mipaka ya Yafethi; Yafethi na aishi katika mahema ya Shemu, na Kanaani na awe mtumwa wake.”
יפת אלהים ליפת וישכן באהלי שם ויהי כנען עבד למו
28 Baada ya gharika Noa aliishi miaka 350.
ויחי נח אחר המבול שלש מאות שנה וחמשים שנה
29 Noa alikuwa na jumla ya miaka 950, ndipo akafa.
ויהיו כל ימי נח תשע מאות שנה וחמשים שנה וימת

< Mwanzo 9 >