< Mwanzo 6 >

1 Watu walipoanza kuongezeka idadi katika uso wa dunia na watoto wa kike wakazaliwa kwao,
And it came to pass, when men began to multiply on the face of the earth, and daughters were born to them,
2 wana wa Mungu wakawaona kuwa hao binti za wanadamu walikuwa wazuri wa sura, wakaoa yeyote miongoni mwao waliyemchagua.
That the sons of God saw the daughters of men that they [were] fair; and they took them wives of all whom they chose.
3 Ndipo Bwana akasema, “Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye ni wa kufa, siku zake zitakuwa miaka 120.”
And the LORD said, My spirit shall not always strive with man, for that he also [is] flesh: yet his days shall be a hundred and twenty years.
4 Wanefili walikuwako duniani siku hizo, na baadaye, hao wana wa Mungu walipoingia kwa binti za wanadamu na kuzaa nao. Wanefili walikuwa mashujaa na watu waliojulikana wa zamani hizo.
There were giants in the earth in those days; and also after that, when the sons of God came in to the daughters of men, and they bore [children] to them: the same [became] mighty men, who [were] of old, men of renown.
5 Bwana akaona jinsi uovu wa mwanadamu ulivyokuwa mkubwa duniani, na ya kuwa kila mwelekeo wa mawazo ya moyo wake wakati wote ulikuwa mbaya tu.
And God saw that the wickedness of man [was] great in the earth, and [that] every imagination of the thoughts of his heart [was] only evil continually.
6 Bwana akasikitika kwamba alimuumba mwanadamu duniani, moyo wa Mungu ukajaa masikitiko.
And the LORD repented that he had made man on the earth, and it grieved him at his heart.
7 Kwa hiyo Bwana akasema, “Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemuumba kutoka kwenye uso wa dunia, wanadamu na wanyama, pamoja na viumbe vitambaavyo na ndege wa angani. Kwa maana nasikitika kuwaumba.”
And the LORD said, I will destroy man whom I have created, from the face of the earth, both man and beast, and the creeping animal, and the fowls of the air; for I repent that I have made them.
8 Lakini Noa akapata kibali machoni pa Bwana.
But Noah found grace in the eyes of the LORD.
9 Hivi ndivyo vizazi vya Noa. Noa alikuwa mtu wa haki, na mkamilifu miongoni mwa watu wa wakati wake, tena alitembea na Mungu.
These [are] the generations of Noah: Noah was a just man, [and] perfect in his generations, [and] Noah walked with God.
10 Noa alikuwa na wana watatu: Shemu, Hamu na Yafethi.
And Noah begat three sons, Shem, Ham, and Japheth.
11 Wakati huu dunia ilikuwa imejaa uharibifu na ukatili machoni pa Mungu.
The earth also was corrupt before God; and the earth was filled with violence.
12 Mungu akaona jinsi dunia ilivyoharibika, kwa maana watu wote duniani walikuwa wameharibu njia zao.
And God looked upon the earth, and behold, it was corrupt: for all flesh had corrupted his way upon the earth.
13 Kwa hiyo Mungu akamwambia Noa, “Nitawaangamiza watu wote, kwa kuwa dunia imejaa ukatili kwa sababu yao. Hakika mimi nitaangamiza watu pamoja na dunia.
And God said to Noah, The end of all flesh is come before me; for the earth is filled with violence through them: and behold, I will destroy them with the earth.
14 Kwa hiyo jitengenezee safina kubwa kwa mbao za mvinje, tengeneza vyumba ndani yake na uipake lami ndani na nje.
Make thee an ark of gopher-wood: rooms shalt thou make in the ark, and shalt pitch it within and without with pitch.
15 Hivi ndivyo utakavyoitengeneza: Safina iwe na urefu wa dhiraa 300, upana wake dhiraa hamsini na kimo chake dhiraa thelathini.
And this [is the fashion] in which thou shalt make it: the length of the ark [shall be] three hundred cubits, the breadth of it fifty cubits, and the height of it thirty cubits.
16 Itengenezee paa na umalizie safina kwa kuacha nafasi ya dhiraa moja juu. Weka mlango ubavuni mwa safina, na uifanye ya ghorofa ya chini, ya kati na ya juu.
A window shalt thou make to the ark, and in a cubit shalt thou finish it above; and the door of the ark shalt thou set in its side: [with] lower, second, and third [stories] shalt thou make it.
17 Nitaleta gharika ya maji juu ya nchi ili kuangamiza uhai wote chini ya mbingu, kila kiumbe chenye pumzi ya uhai ndani yake. Kila kitu juu ya nchi kitaangamia.
And behold, I, even I do bring a flood of waters upon the earth, to destroy all flesh, in which [is] the breath of life, from under heaven: [and] every thing that [is] on the earth shall die.
18 Lakini Mimi nitaweka Agano langu na wewe, nawe utaingia ndani ya Safina, wewe pamoja na mke wako, wanao na wake zao.
But with thee will I establish my covenant: and thou shalt come into the ark, thou, and thy sons, and thy wife, and thy sons' wives with thee.
19 Utaingiza ndani ya Safina kila aina ya kiumbe hai wawili wawili, wa kiume na wa kike, ili kuwahifadhi hai pamoja na wewe.
And of every living thing of all flesh, two of every [sort] shalt thou bring into the ark, to keep [them] alive with thee: they shall be male and female.
20 Wawili wa kila aina ya ndege, wa kila aina ya mnyama na wa kila aina ya kitambaacho ardhini watakuja kwako ili wahifadhiwe hai.
Of fowls after their kind, and of cattle after their kind, of every creeping animal of the earth after its kind, two of every [sort] shall come to thee, to keep [them] alive.
21 Utachukua kila aina ya chakula kitakacholiwa, na ukiweke akiba kama chakula kwa ajili yako na yao.”
And take thou to thee of all food that is eaten, and thou shalt gather [it] to thee; and it shall be for food for thee, and for them.
22 Noa akafanya kila kitu kama vile Mungu alivyomwamuru.
Thus did Noah; according to all that God commanded him, so did he.

< Mwanzo 6 >

The World is Destroyed by Water
The World is Destroyed by Water