< Mwanzo 5 >

1 Hii ni orodha iliyoandikwa ya vizazi vya Adamu. Wakati Mungu alipomuumba Adamu, alimfanya kwa sura ya Mungu.
Hii ni orodha ya vizazi vya Adamu. Katika siku ambayo Mungu alimuumba mtu, aliwaumba katika mfano wake mwenyewe.
2 Aliwaumba mwanaume na mwanamke, akawabariki. Walipokwisha kuumbwa, akawaita “mwanadamu.”
Mwanaume na mwanamke aliwaumba. Akawabariki na akawaita Adam wakati walipoumbwa.
3 Adamu alipokuwa ameishi miaka 130, alikuwa na mwana aliyekuwa na sura yake, mwenye kufanana naye. Akamwita Sethi.
Wakati Adamu alipokuwa ameishi miaka 130, akamzaa mwana katika sura yake mwenyewe, kwa mfano wake, na akamuita jina lake Sethi.
4 Baada ya Sethi kuzaliwa, Adamu aliishi miaka 800, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike.
Baada ya Adamu kumzaa Sethi, aliishi miaka mia nane. Akawazaa wana wengi waume na wake.
5 Adamu aliishi jumla ya miaka 930, ndipo akafa.
Adamu akaishi miaka 930 kisha akafariki.
6 Sethi alipokuwa ameishi miaka 105, akamzaa Enoshi.
Wakati Sethi alipokuwa ameishi miaka 105, akamzaa Enoshi.
7 Baada ya kumzaa Enoshi, Sethi aliishi miaka 807, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike.
Baada ya kumzaa Enoshi, akaishi miaka 807 na akawazaa wana wengi waume na wake.
8 Sethi aliishi jumla ya miaka 912, ndipo akafa.
Sethi akaishi miaka 912 kisha akafariki.
9 Enoshi alipokuwa ameishi miaka tisini, akamzaa Kenani.
Wakati Enoshi alipokuwa ameishi miaka tisini, akamzaa Kenani.
10 Baada ya kumzaa Kenani, Enoshi aliishi miaka 815, naye alikuwa na watoto wengine wa kiume na wa kike.
Baada ya kumzaa Kenani, Enoshi aliishi miaka 815. Akazaa wana wengi wa ume na wake.
11 Enoshi aliishi jumla ya miaka 905, ndipo akafa.
Enoshi aliishi miaka 905 na kisha akafariki.
12 Kenani alipokuwa ameishi miaka sabini, akamzaa Mahalaleli.
Wakati Kanani alipokuwa ameishi miaka sabini, akamzaa Mahalaleli.
13 Baada ya kumzaa Mahalaleli, Kenani aliishi miaka 840, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike.
Baada ya kumzaa Mahalaleli, Kenani aliishi miaka 840. Akawazaa wana wengi wa ume na wake.
14 Kenani aliishi jumla ya miaka 910, ndipo akafa.
Kenani aliishi miaka 910, na kisha akafariki.
15 Mahalaleli alipokuwa ameishi miaka sitini na mitano, akamzaa Yaredi.
Mahalaleli alipokuwa ameishi miaka sitini na tano, alimzaa Yaredi.
16 Baada ya kumzaa Yaredi, Mahalaleli aliishi miaka 830, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike.
Baada ya kumzaa Yaredi, Mahalaleli aliishi miaka 830. Akazaa wana wengi wa ume na wake.
17 Mahalaleli aliishi jumla ya miaka 895, ndipo akafa.
Mahalaleli aliishi miaka 895 na kisha akafariki.
18 Yaredi alipokuwa ameishi miaka 162, akamzaa Enoki.
Yaredi alipokuwa ameishi miaka 162, alimzaa Henoko.
19 Baada ya kumzaa Enoki, Yaredi aliishi miaka 800, naye akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike.
Baada ya kumzaa Henoko, Yaredi aliishi miaka mianane. Akazaa wana wengi waume na wake.
20 Yaredi aliishi jumla ya miaka 962, ndipo akafa.
Yaredi aliishi miaka 962 na kisha akafariki.
21 Enoki alipokuwa ameishi miaka sitini na mitano, akamzaa Methusela.
Henoko alipokuwa ameishi miaka sitini na tano, akamzaa Methusela.
22 Baada ya kumzaa Methusela, Enoki alitembea na Mungu miaka 300, na akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike.
Henoko akaenenda na Mungu miaka miatatu baada ya kumzaa Methusela. Aliwazaa wana wengi wa ume na wake.
23 Enoki aliishi jumla ya miaka 365.
Henoko aliishi miaka 365.
24 Enoki akatembea na Mungu, kisha akatoweka, kwa sababu Mungu alimchukua.
Henoko alienenda na Mungu, na kisha alitoweka, kwa kuwa Mungu alimtwaa.
25 Methusela alipokuwa ameishi miaka 187, akamzaa Lameki.
Wakati Methusela alipokuwa ameishi miaka 187, alimzaa Lameki.
26 Baada ya kumzaa Lameki, Methusela aliishi miaka 782, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike.
Baada ya kumzaa Lameki, Methusela aliishi miaka 782. Akawazaa wana wengi wa ume na wake.
27 Methusela aliishi jumla ya miaka 969, ndipo akafa.
Methusela aliishi miaka 969. Kisha akafariki.
28 Lameki alipokuwa ameishi miaka 182, alimzaa mwana.
Wakati Lameki alipokuwa ameishi miaka 182, alimzaa mwana.
29 Akamwita jina lake Noa, akasema, “Yeye ndiye atakayetufariji katika kazi na maumivu makali ya mikono yetu yaliyosababishwa na ardhi iliyolaaniwa na Bwana.”
Akamuita jina lake Nuhu, akisema, “Huyu ndiye atatupatia pumziko kutoka katika kazi yetu na kutoka katika kazi ya taabu ya mikono yetu, ambayo lazima tuifanye kwa sababu ya ardhi ambayo Yahwe ameilaani.”
30 Baada ya Noa kuzaliwa, Lameki aliishi miaka 595, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike.
Lameki aliishi miaka 595 baada ya kumzaa baba wa Nuhu. Akazaa wanawengi wa ume na wake.
31 Lameki aliishi jumla ya miaka 777, ndipo akafa.
Lameki aliishi miaka 777. Kisha akafariki.
32 Baada ya Noa kuishi miaka 500, aliwazaa Shemu, Hamu na Yafethi.
Baada ya Nuhu kuishi miaka miatano, akamzaa Shemu, Hamu, na Yafethi.

< Mwanzo 5 >