< Mwanzo 5 >
1 Hii ni orodha iliyoandikwa ya vizazi vya Adamu. Wakati Mungu alipomuumba Adamu, alimfanya kwa sura ya Mungu.
2 Aliwaumba mwanaume na mwanamke, akawabariki. Walipokwisha kuumbwa, akawaita “mwanadamu.”
3 Adamu alipokuwa ameishi miaka 130, alikuwa na mwana aliyekuwa na sura yake, mwenye kufanana naye. Akamwita Sethi.
4 Baada ya Sethi kuzaliwa, Adamu aliishi miaka 800, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike.
5 Adamu aliishi jumla ya miaka 930, ndipo akafa.
6 Sethi alipokuwa ameishi miaka 105, akamzaa Enoshi.
7 Baada ya kumzaa Enoshi, Sethi aliishi miaka 807, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike.
8 Sethi aliishi jumla ya miaka 912, ndipo akafa.
9 Enoshi alipokuwa ameishi miaka tisini, akamzaa Kenani.
10 Baada ya kumzaa Kenani, Enoshi aliishi miaka 815, naye alikuwa na watoto wengine wa kiume na wa kike.
11 Enoshi aliishi jumla ya miaka 905, ndipo akafa.
12 Kenani alipokuwa ameishi miaka sabini, akamzaa Mahalaleli.
13 Baada ya kumzaa Mahalaleli, Kenani aliishi miaka 840, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike.
14 Kenani aliishi jumla ya miaka 910, ndipo akafa.
15 Mahalaleli alipokuwa ameishi miaka sitini na mitano, akamzaa Yaredi.
16 Baada ya kumzaa Yaredi, Mahalaleli aliishi miaka 830, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike.
17 Mahalaleli aliishi jumla ya miaka 895, ndipo akafa.
18 Yaredi alipokuwa ameishi miaka 162, akamzaa Enoki.
19 Baada ya kumzaa Enoki, Yaredi aliishi miaka 800, naye akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike.
20 Yaredi aliishi jumla ya miaka 962, ndipo akafa.
21 Enoki alipokuwa ameishi miaka sitini na mitano, akamzaa Methusela.
22 Baada ya kumzaa Methusela, Enoki alitembea na Mungu miaka 300, na akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike.
23 Enoki aliishi jumla ya miaka 365.
24 Enoki akatembea na Mungu, kisha akatoweka, kwa sababu Mungu alimchukua.
25 Methusela alipokuwa ameishi miaka 187, akamzaa Lameki.
26 Baada ya kumzaa Lameki, Methusela aliishi miaka 782, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike.
27 Methusela aliishi jumla ya miaka 969, ndipo akafa.
28 Lameki alipokuwa ameishi miaka 182, alimzaa mwana.
29 Akamwita jina lake Noa, akasema, “Yeye ndiye atakayetufariji katika kazi na maumivu makali ya mikono yetu yaliyosababishwa na ardhi iliyolaaniwa na Bwana.”
30 Baada ya Noa kuzaliwa, Lameki aliishi miaka 595, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike.
31 Lameki aliishi jumla ya miaka 777, ndipo akafa.
32 Baada ya Noa kuishi miaka 500, aliwazaa Shemu, Hamu na Yafethi.