< Mwanzo 49 >

1 Ndipo Yakobo akawaita wanawe na kusema: “Kusanyikeni kunizunguka ili niweze kuwaambia lile litakalowatokea siku zijazo.
ויקרא יעקב אל בניו ויאמר האספו ואגידה לכם את אשר יקרא אתכם באחרית הימים׃
2 “Kusanyikeni na msikilize, enyi wana wa Yakobo, msikilizeni baba yenu Israeli.
הקבצו ושמעו בני יעקב ושמעו אל ישראל אביכם׃
3 “Reubeni, wewe ni mzaliwa wangu wa kwanza, nguvu zangu, tunda la kwanza la nguvu zangu, umepita kwa heshima, umepita kwa uwezo.
ראובן בכרי אתה כחי וראשית אוני יתר שאת ויתר עז׃
4 Usiyezuiwa kama maji, basi hutakuwa mkuu tena, kwa kuwa ulipanda kwenye kitanda cha baba yako, kwenye kitanda changu na kukinajisi.
פחז כמים אל תותר כי עלית משכבי אביך אז חללת יצועי עלה׃
5 “Simeoni na Lawi ni wana ndugu: panga zao ni silaha za jeuri.
שמעון ולוי אחים כלי חמס מכרתיהם׃
6 Mimi na nisiingie katika baraza lao, nami nisiunganike katika kusanyiko lao, kwa kuwa wamewaua watu katika hasira yao, walikata mishipa ya miguu ya mafahali kama walivyopenda.
בסדם אל תבא נפשי בקהלם אל תחד כבדי כי באפם הרגו איש וברצנם עקרו שור׃
7 Hasira yao na ilaaniwe, kwa kuwa ni kali mno, nayo ghadhabu yao ni ya ukatili! Nitawatawanya katika Yakobo Na kuwasambaza katika Israeli.
ארור אפם כי עז ועברתם כי קשתה אחלקם ביעקב ואפיצם בישראל׃
8 “Yuda, ndugu zako watakusifu; mkono wako utakuwa shingoni mwa adui zako; wana wa baba yako watakusujudia.
יהודה אתה יודוך אחיך ידך בערף איביך ישתחוו לך בני אביך׃
9 Ee Yuda, wewe ni mwana simba; unarudi toka mawindoni, mwanangu. Kama simba hunyemelea na kulala chini, kama simba jike: nani athubutuye kumwamsha?
גור אריה יהודה מטרף בני עלית כרע רבץ כאריה וכלביא מי יקימנו׃
10 Fimbo ya ufalme haitaondoka kwa Yuda, wala fimbo ya mtawala kati ya miguu yake, hadi aje yeye ambaye milki ni yake, ambaye utii wa mataifa ni wake.
לא יסור שבט מיהודה ומחקק מבין רגליו עד כי יבא שילה ולו יקהת עמים׃
11 Atamfunga punda wake katika mzabibu, naye mwana-punda wake kwenye tawi lililo bora zaidi; atafua mavazi yake katika divai, majoho yake katika damu ya mizabibu.
אסרי לגפן עירה ולשרקה בני אתנו כבס ביין לבשו ובדם ענבים סותה׃
12 Macho yake yatakuwa mekundu kwa divai, meno yake yatakuwa meupe kwa maziwa.
חכלילי עינים מיין ולבן שנים מחלב׃
13 “Zabuloni ataishi pwani ya bahari na kuwa bandari za kuegesha meli; mpaka wake utapanuka kuelekea Sidoni.
זבולן לחוף ימים ישכן והוא לחוף אניות וירכתו על צידן׃
14 “Isakari ni punda mwenye nguvu ambaye amelala kati ya mizigo yake.
יששכר חמר גרם רבץ בין המשפתים׃
15 Aonapo palivyo pazuri mahali pake pa kupumzika na jinsi nchi yake inavyopendeza, atainamisha bega lake kwenye mzigo na kujitolea kwa ajili ya kazi ngumu.
וירא מנחה כי טוב ואת הארץ כי נעמה ויט שכמו לסבל ויהי למס עבד׃
16 “Dani atahukumu watu wake kwa haki kama mmoja wa makabila ya Israeli.
דן ידין עמו כאחד שבטי ישראל׃
17 Dani atakuwa nyoka kando ya barabara, nyoka mwenye sumu kando ya njia, yule aumaye visigino vya farasi ili yule ampandaye aanguke chali.
יהי דן נחש עלי דרך שפיפן עלי ארח הנשך עקבי סוס ויפל רכבו אחור׃
18 “Ee Bwana, nautafuta wokovu wako.
לישועתך קויתי יהוה׃
19 “Gadi atashambuliwa ghafula na kundi la washambuliaji, lakini yeye atawageukia na kuwashinda kabisa.
גד גדוד יגודנו והוא יגד עקב׃
20 “Chakula cha Asheri kitakuwa kinono, naye atatoa chakula kitamu kimfaacho mfalme.
מאשר שמנה לחמו והוא יתן מעדני מלך׃
21 “Naftali ni kulungu jike aliyeachiwa huru azaaye watoto wazuri.
נפתלי אילה שלחה הנתן אמרי שפר׃
22 “Yosefu ni mzabibu uzaao, mzabibu uzaao ulio kando ya chemchemi, ambao matawi yake hutanda ukutani.
בן פרת יוסף בן פרת עלי עין בנות צעדה עלי שור׃
23 Kwa uchungu wapiga mshale walimshambulia, wakampiga mshale kwa ukatili.
וימררהו ורבו וישטמהו בעלי חצים׃
24 Lakini upinde wake ulibaki imara, mikono yake ikatiwa nguvu, na mkono wa Mwenye Nguvu wa Yakobo, kwa sababu ya Mchungaji, Mwamba wa Israeli,
ותשב באיתן קשתו ויפזו זרעי ידיו מידי אביר יעקב משם רעה אבן ישראל׃
25 kwa sababu ya Mungu wa baba yako, anayekusaidia, kwa sababu ya Mwenyezi, yeye anayekubariki kwa baraka za mbinguni juu, baraka za kilindi kilichoko chini, baraka za matitini na za tumbo la uzazi.
מאל אביך ויעזרך ואת שדי ויברכך ברכת שמים מעל ברכת תהום רבצת תחת ברכת שדים ורחם׃
26 Baraka za baba yako ni kubwa kuliko baraka za milima ya kale, nyingi kuliko vilima vya kale. Baraka hizo zote na zikae juu ya kichwa cha Yosefu, juu ya paji la yule mkuu miongoni mwa ndugu zake.
ברכת אביך גברו על ברכת הורי עד תאות גבעת עולם תהיין לראש יוסף ולקדקד נזיר אחיו׃
27 “Benyamini ni mbwa mwitu mlafi mwenye njaa kuu; asubuhi hurarua mawindo yake, jioni hugawa nyara.”
בנימין זאב יטרף בבקר יאכל עד ולערב יחלק שלל׃
28 Haya yote ndiyo makabila kumi na mawili ya Israeli, na hivi ndivyo baba yao alivyowaambia alipowabariki, akimpa kila mmoja baraka inayomfaa.
כל אלה שבטי ישראל שנים עשר וזאת אשר דבר להם אביהם ויברך אותם איש אשר כברכתו ברך אתם׃
29 Ndipo alipowapa maelekezo haya: “Mimi niko karibu kukusanywa kwa watu wangu. Mnizike pamoja na baba zangu kwenye pango katika shamba la Efroni, Mhiti,
ויצו אותם ויאמר אלהם אני נאסף אל עמי קברו אתי אל אבתי אל המערה אשר בשדה עפרון החתי׃
30 pango lililoko katika shamba la Makpela, karibu na Mamre huko Kanaani, ambalo Abrahamu alinunua kwa ajili ya mahali pa kuzikia kutoka kwa Efroni, Mhiti, pamoja na shamba.
במערה אשר בשדה המכפלה אשר על פני ממרא בארץ כנען אשר קנה אברהם את השדה מאת עפרן החתי לאחזת קבר׃
31 Huko ndiko Abrahamu na Sara mkewe walikozikwa, huko akazikwa Isaki na Rebeka mkewe, na huko nilimzika Lea.
שמה קברו את אברהם ואת שרה אשתו שמה קברו את יצחק ואת רבקה אשתו ושמה קברתי את לאה׃
32 Shamba hilo na pango lililoko ndani yake lilinunuliwa kutoka kwa Wahiti.”
מקנה השדה והמערה אשר בו מאת בני חת׃
33 Baada ya Yakobo kumaliza kutoa maelekezo hayo kwa wanawe, akarudisha miguu yake kitandani, akapumua pumzi ya mwisho, na akakusanywa kwa watu wake.
ויכל יעקב לצות את בניו ויאסף רגליו אל המטה ויגוע ויאסף אל עמיו׃

< Mwanzo 49 >