< Mwanzo 40 >
1 Baada ya muda, mnyweshaji na mwokaji wa mfalme wa Misri, wakamkosea bwana wao, mfalme wa Misri.
這事以後,埃及王的酒政和膳長得罪了他們的主-埃及王,
2 Farao akawakasirikia hawa maafisa wake wawili, mnyweshaji mkuu na mwokaji mkuu,
法老就惱怒酒政和膳長這二臣,
3 akawaweka chini ya ulinzi katika nyumba ya mkuu wa kikosi cha ulinzi katika gereza lile lile alimofungwa Yosefu.
把他們下在護衛長府內的監裏,就是約瑟被囚的地方。
4 Mkuu wa kikosi cha ulinzi akawakabidhi kwa Yosefu, naye akawahudumia. Walipokuwa wamekaa chini ya ulinzi kwa muda,
護衛長把他們交給約瑟,約瑟便伺候他們;他們有些日子在監裏。
5 kila mmoja wa hao wawili waliokuwa wamewekwa gerezani, yaani mnyweshaji na mwokaji wa mfalme wa Misri, waliota ndoto usiku mmoja, na kila ndoto ilikuwa na maana yake tofauti.
被囚在監之埃及王的酒政和膳長二人同夜各做一夢,各夢都有講解。
6 Yosefu alipowajia asubuhi yake, akawaona kwamba walikuwa na huzuni.
到了早晨,約瑟進到他們那裏,見他們有愁悶的樣子。
7 Ndipo Yosefu akawauliza maafisa hao wa Farao waliokuwa chini ya ulinzi pamoja naye nyumbani mwa bwana wake, akasema, “Mbona nyuso zenu zimejaa huzuni leo?”
他便問法老的二臣,就是與他同囚在他主人府裏的,說:「你們今日為甚麼面帶愁容呢?」
8 Wakamjibu, “Sisi sote tuliota ndoto, lakini hapakuwa na mtu yeyote wa kuzifasiri.” Ndipo Yosefu akawaambia, “Je, kufasiri ndoto si kazi ya Mungu? Niambieni ndoto zenu.”
他們對他說:「我們各人做了一夢,沒有人能解。」約瑟說:「解夢不是出於上帝嗎?請你們將夢告訴我。」
9 Basi mkuu wa wanyweshaji akamweleza Yosefu ndoto yake. Akamwambia, “Katika ndoto yangu niliona mzabibu mbele yangu,
酒政便將他的夢告訴約瑟說:「我夢見在我面前有一棵葡萄樹,
10 nao mzabibu ulikuwa na matawi matatu. Mara tu ulipoanza kuchipua, maua yalichanua na vishada vyake vikawa zabibu zilizoiva.
樹上有三根枝子,好像發了芽,開了花,上頭的葡萄都成熟了。
11 Kikombe cha Farao kilikuwa mkononi mwangu, nikazitwaa zabibu, nikazikamua katika kikombe cha Farao, na nikaweka kikombe mkononi mwake.”
法老的杯在我手中,我就拿葡萄擠在法老的杯裏,將杯遞在他手中。」
12 Yosefu akamwambia, “Hii ndiyo maana yake: Matawi matatu ni siku tatu.
約瑟對他說:「你所做的夢是這樣解:三根枝子就是三天;
13 Katika siku hizi tatu, Farao atakutoa gerezani na kukuweka tena kwenye nafasi yako, nawe utaweka kikombe cha Farao mikononi mwake, kama vile ulivyokuwa unafanya ulipokuwa mnyweshaji wake.
三天之內,法老必提你出監,叫你官復原職,你仍要遞杯在法老的手中,和先前作他的酒政一樣。
14 Lakini wakati mambo yatakapokuwia mazuri, unikumbuke, unifanyie wema, useme mema juu yangu kwa Farao ili niondoke huku gerezani.
但你得好處的時候,求你記念我,施恩與我,在法老面前提說我,救我出這監牢。
15 Kwa maana nilichukuliwa kwa nguvu kutoka nchi ya Waebrania, na hata hapa nilipo sikufanya lolote linalostahili niwekwe gerezani.”
我實在是從希伯來人之地被拐來的;我在這裏也沒有做過甚麼,叫他們把我下在監裏。」
16 Yule mwokaji mkuu alipoona kuwa Yosefu amefasiri ikiwa na maana nzuri, akamwambia Yosefu, “Mimi pia niliota ndoto: Kichwani mwangu kulikuwepo vikapu vitatu vya mikate.
膳長見夢解得好,就對約瑟說:「我在夢中見我頭上頂着三筐白餅;
17 Katika kikapu cha juu kulikuwa na aina zote za vyakula vilivyookwa kwa ajili ya Farao, lakini ndege walikuwa wakivila kutoka kwenye kikapu nilichokuwa nimebeba kichwani.”
極上的筐子裏有為法老烤的各樣食物,有飛鳥來吃我頭上筐子裏的食物。」
18 Yosefu akamwambia, “Hii ndiyo maana yake: Vikapu vitatu ni siku tatu.
約瑟說:「你的夢是這樣解:三個筐子就是三天;
19 Katika siku hizi tatu, Farao atakata kichwa chako na kukutundika juu ya mti. Nao ndege watakula nyama ya mwili wako.”
三天之內,法老必斬斷你的頭,把你掛在木頭上,必有飛鳥來吃你身上的肉。」
20 Mnamo siku ya tatu, ilikuwa kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Farao, naye akawaandalia maafisa wake wote karamu. Akawatoa gerezani mnyweshaji mkuu na mwokaji mkuu, akawaweka mbele ya maafisa wake:
到了第三天,是法老的生日,他為眾臣僕設擺筵席,把酒政和膳長提出監來,
21 Ndipo akamrudisha mnyweshaji mkuu kwenye nafasi yake, ili aweke kikombe mikononi mwa Farao tena,
使酒政官復原職,他仍舊遞杯在法老手中;
22 lakini akamwangika yule mwokaji mkuu, sawasawa na jinsi Yosefu alivyowaambia katika tafsiri yake.
但把膳長掛起來,正如約瑟向他們所解的話。
23 Pamoja na hayo, mnyweshaji mkuu hakumkumbuka Yosefu, bali alimsahau.
酒政卻不記念約瑟,竟忘了他。