< Mwanzo 36 >

1 Hivi ndivyo vizazi vya Esau (yaani Edomu).
Hivi ndivyo vizazi vya Esau (aliyeitwa pia Edom).
2 Esau akaoa wake kutoka miongoni mwa wanawake wa Kanaani: Ada binti wa Eloni Mhiti, Oholibama binti wa Ana, mjukuu wa kike wa Sibeoni Mhivi,
Esau akachukua wakeze kutoka kwa Wakanaani. Hawa walikuwa wake zake: Ada binti Eloni Mhiti; Oholibama binti Ana, mjukuu wa Zibeoni Mhivi; na
3 pia akaoa Basemathi binti wa Ishmaeli, dada yake Nebayothi.
Basemathi, binti Ishmaeli, dada wa Nebayothi.
4 Ada akamzalia Esau Elifazi, Basemathi akamzaa Reueli,
Ada akamzaa Elifazi kwa Esau, na Basemathi akamzaa Reueli.
5 Oholibama akamzaa Yeushi, Yalamu na Kora. Hawa ndio wana wa Esau waliozaliwa kwake huko Kanaani.
Oholibama akamzaa Yeushi, Yalamu, na Kora. Hawa walikuwa wana wa Esau waliozaliwa kwake katika nchi ya Kananaani.
6 Esau akawachukua wake zake, watoto wake wa kiume na wa kike na wote wa nyumbani mwake, mifugo yake pamoja na wanyama wake wengine wote na mali yake yote ambayo alikuwa ameipata akiwa Kanaani, akahamia katika nchi iliyo mbali na Yakobo ndugu yake.
Esau akawachukua wakeze, wanawe, binti zake, na watu wote wa nyumba yake, mifugo wake - wanyama wake wote, na mali yake yote, aliyokuwa amekusanya katika nchi ya Kanaani, na akaenda katika nchi iliyoko mbali kutoka kwa Yakobo nduguye.
7 Mali zao zilikuwa nyingi sana kiasi kwamba haikuwa rahisi wao kuishi pamoja, nchi waliyokuwa wakiishi isingewatosha wote kwa ajili ya mifugo yao.
Alifanya hivi kwa sababu mali zao zilikuwa nyingi sana kwa wao kuishi pamoja. Nchi waliyokuwa wamekaa isingeweza kuwafaa kwa mifugo yao.
8 Kwa hiyo Esau (ambaye ni Edomu) aliishi katika nchi ya kilima huko Seiri.
Hivyo Esau, aliyejulikana pia kama Edomu, akakaa katika nchi ya kilima Seiri.
9 Hawa ndio wazao wa Esau, baba wa Waedomu, katika nchi ya kilima cha Seiri.
Hivi ndivyo vizazi vya Esau, babu wa Waedomu katika nchi ya mlima Seiri.
10 Haya ndiyo majina ya wana wa Esau: Elifazi, mwana wa Esau ambaye mkewe Ada alimzalia; na Reueli, mwana wa Esau ambaye mkewe Basemathi alimzalia.
Haya yalikuwa majina ya wana wa Esau: Elifazi mwana wa Ada, mkewe Esau; Reueli mwana wa Basemathi, mkewe Esau.
11 Wana wa Elifazi ni: Temani, Omari, Sefo, Gatamu na Kenazi.
Wana wa Elifazi walikuwa Temani, Omari, Zefo, Gatamu, na Kenazi.
12 Elifazi mwana wa Esau alikuwa pia na suria aliyeitwa Timna, ambaye alimzalia Amaleki. Hawa ndio waliokuwa wajukuu wa Ada mke wa Esau.
Timna, suria wa Elifazi, mwana wa Esau, akamzaa Amaleki. Hawa walikuwa wajukuu wa Ada, mkewe Esau.
13 Wana wa Reueli ni: Nahathi, Zera, Shama na Miza. Hawa ndio waliokuwa wajukuu wa Basemathi mkewe Esau.
Hawa walikuwa wana wa Reueli: Nahathi, Zera, Shama, na Miza. Hawa walikuwa wajukuu wa Basemathi, mkewe Esau.
14 Wana wa Oholibama binti Ana, mkewe Esau, aliyekuwa mjukuu wa Sibeoni, aliomzalia Esau ni: Yeushi, Yalamu na Kora.
Hawa walikuwa wana wa Oholibama, mkewe Esau, aliyekuwa binti Ana na mjukuu wa Zibeoni. Alimzalia Esau Yeushi, Yalamu, na Kora.
15 Hawa ndio waliokuwa wakuu miongoni mwa wazao wa Esau: Wakuu wa wana wa Elifazi, mzaliwa wa kwanza wa Esau ni: Temani, Omari, Sefo, Kenazi,
Hizi zilikuwa koo kati ya vizazi vya Esau: uzao wa Elifazi, mzaliwa wa kwanza wa Esau: Temani, Omari, Zefo, Kenazi, Kora,
16 Kora, Gatamu na Amaleki. Hawa ndio waliokuwa wakuu waliotoka kwa Elifazi huko Edomu, waliokuwa wajukuu wa kiume wa Ada.
Gatamu, na Amaleki. Hivi vilikuwa vizazi vya koo kutoka kwa Elifazi katika nchi ya Edomu. Walikuwa wajukuu wa Ada.
17 Wakuu wa wana wa Reueli, mwana wa Esau ni: Nahathi, Zera, Shama na Miza. Hawa ndio wakuu waliotoka kwa Reueli huko Edomu, waliokuwa wajukuu wa kiume wa Basemathi mkewe Esau.
Hizi zilikuwa koo kutoka kwa Reueli, mwana wa Esau: Nahathi, Zera, Shama, Miza. Hizi zilikuwa koo kutoka kwa Reueli katika nchi ya Edomu. Walikuwa wajukuu wa Basemathi, mkewe Esau.
18 Wakuu wa wana wa Esau ambao mkewe Oholibama alimzalia ni: Yeushi, Yalamu na Kora. Hawa ndio wakuu waliotoka kwa mke wa Esau, Oholibama binti Ana.
Hizi zilikuwa koo za Oholibama, mkewe Esau: Yeushi, Yalamu, Kora. Hizi ni koo zilizotoka kwa Oholibama mkewe Esau, binti Ana.
19 Hawa ndio waliokuwa wana wa Esau (ndiye Edomu), na hawa ndio waliokuwa wakuu wao.
Hawa walikuwa wana wa Esau na koo zao.
20 Hawa ndio walikuwa wana wa Seiri, Mhori, waliokuwa wakiishi katika nchi ile: Lotani, Shobali, Sibeoni, Ana,
Hawa walikuwa wana wa Seiri Mhori, wenyeji wa nchi hiyo: Lotani, Shobali, Zibeoni, Ana,
21 Dishoni, Eseri na Dishani. Hawa ndio wana wa Seiri huko Edomu waliokuwa wakuu kwa Wahori.
Dishoni, Ezeri, na Dishani. Hizi zilikuwa koo the Wahori, wenyeji wa Seiri katika nchi ya Edomu.
22 Wana wa Lotani walikuwa: Hori na Homamu. Timna alikuwa dada yake Lotani.
Wana wa Lotani walikuwa Hori na Hemani, na Timna alikuwa dada wa Lotani.
23 Wana wa Shobali walikuwa: Alvani, Manahathi, Ebali, Shefo na Onamu.
Hawa walikuwa wana wa Shobali: Alvani, Manahathi, Ebali, Shefo, na Onamu.
24 Wana wa Sibeoni walikuwa: Aiya na Ana. Huyu Ana ndiye aligundua chemchemi ya maji moto jangwani alipokuwa akichunga punda za Sibeoni baba yake.
Hawa walikuwa wana wa Zibeoni: Aia na Ana. Huyu ndiye Ana aliyeona chemichemi za moto nyikani, alipokuwa akichunga punda wa Zibeoni babaye.
25 Watoto wa Ana walikuwa: Dishoni na Oholibama binti wa Ana.
Hawa walikuwa watoto wa Ana: Dishoni na Oholibama, binti Ana.
26 Wana wa Dishoni walikuwa: Hemdani, Eshbani, Ithrani na Kerani.
Hawa walikuwa wana wa Dishoni: Hemdani, Eshbani, Ithrani, na Kerani.
27 Wana wa Eseri walikuwa: Bilhani, Zaavani na Akani.
Hawa walikuwa wana wa Ezeri: Bilhani, Zaavani, na Akani.
28 Wana wa Dishani walikuwa: Usi na Arani.
Hawa walikuwa wana wa Dishani: Uzi na Arani.
29 Hawa ndio waliokuwa wakuu wa Wahori: Lotani, Shobali, Sibeoni, Ana,
Hizi zilikuwa koo za Wahori: Lotani, Shobali, Zibeoni, na Ana,
30 Dishoni, Eseri na Dishani. Hawa ndio walikuwa wakuu wa Wahori, kufuatana na makundi yao, katika nchi ya Seiri.
Dishoni, Ezeri, Dishani: hizi zilikuwa koo za Wahori, kulingana na ukoo ulivyoorodheshwa katika nchi ya Seiri.
31 Wafuatao ni wafalme waliotawala Edomu kabla ya mfalme yeyote wa Israeli kutawala:
Hawa walikuwa wafalme waliomiliki katika nchi ya Edomu kabla ya mfalme yeyote kumilika juu ya Waisraeli:
32 Bela mwana wa Beori alikuwa mfalme wa Edomu. Mji wake uliitwa Dinhaba.
Bela mwana wa Beori, alitawala huko Edomu, na jina la mji wake lilikuwa Dinhaba.
33 Bela alipofariki, Yobabu mwana wa Zera kutoka Bosra akawa mfalme baada yake.
Bela alipofariki, kisha Yobabu mwana wa Zera kutoka Bozra, akatawala mahali pake.
34 Yobabu alipofariki, Hushamu kutoka nchi ya Watemani akawa mfalme baada yake.
Yobabu alipofariki, Hushamu aliyekuwa wa nchi ya Watemani, akatawala mahali pake.
35 Hushamu alipofariki, Hadadi mwana wa Bedadi, aliyeshinda Midiani katika nchi ya Moabu, akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Avithi.
Hushamu alipofariki, Hadadi mwana wa Bedadi aliyewashinda Wamidiani katika nchi ya Moabu, akatawala mahali pake. Jina la mji wake lilikuwa Avithi.
36 Hadadi alipofariki, Samla kutoka Masreka akawa mfalme baada yake.
Hadadi alipofariki, kisha Samla wa Masreka akatawala mahali pake.
37 Samla alipofariki, Shauli kutoka Rehobothi ngʼambo ya Mto Frati akawa mfalme baada yake.
Samla alipofariki, kisha Shauli wa Rehobothi kando ya mto alitawala mahali pake.
38 Shauli alipofariki, Baal-Hanani mwana wa Akbori akawa mfalme baada yake.
Shauli alipofariki, kisha Baali Hanani mwana wa Akbori akatawala mahali pake.
39 Baal-Hanani mwana wa Akbori alipofariki, Hadadi akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Pau, na mkewe aliitwa Mehetabeli binti Matredi, binti Me-Zahabu.
Baali Hanani mwana wa Akbori, alipokufa, kisha Hadari akatawala mahali pake. Jina la mji wake lilikuwa Pau. Jina la mkewe lilikuwa Mehetabeli, binti Matredi, mjukuu wa Me Zahabu.
40 Hawa ndio wakuu waliotokana na Esau, kwa majina, kufuatana na koo zao na nchi zao: Timna, Alva, Yethethi,
Haya ndiyo yalikuwa majina ya wakuu wa koo kutoka uzao wa Esau, kwa kufuata koo zao na maeneo yao, kwa majina yao: Timna, Alva, Yethethi,
41 Oholibama, Ela, Pinoni,
Oholibama, Ela, Pinoni,
42 Kenazi, Temani, Mibsari,
Kenazi, Temani, Mbza,
43 Magdieli na Iramu. Hawa ndio walikuwa wakuu wa Edomu, kufuatana na makazi yao katika nchi waliyoimiliki. Huyu ndiye alikuwa Esau, baba wa Waedomu.
Magdieli, na Iramu. Hawa walikuwa wakuu wa ukoo wa Edomu, kwa kufuata makao yao katika nchi waliyomiliki. Nao ni Esau, baba wa Waedomu.

< Mwanzo 36 >