< Mwanzo 10 >
1 Hawa ndio wazao wa Noa: Shemu, Hamu na Yafethi, ambao walizaa wana baada ya gharika.
Hivi ndivyo vilikuwa vizazi vya wana wa Nuhu, ambao ni, Shemu, Hamu, na Yafethi. Wana wa kiume walizaliwa kwao baada ya gharika.
2 Wana wa Yafethi walikuwa: Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Mesheki na Tirasi.
Wana wa Yafethi walikuwa Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Masheki, na Tirasi.
3 Wana wa Gomeri walikuwa: Ashkenazi, Rifathi na Togarma.
Na wana wa Gomeri walikuwa Ashikenazi, Rifathi na Togama.
4 Wana wa Yavani walikuwa: Elisha, Tarshishi, Kitimu na Rodanimu.
Wana wa Yavani walikuwa Elisha, Tarshishi, Kitimu, na Dodanimu.
5 (Kutokana na hawa mataifa ya Pwani yalienea katika nchi zao, kwa koo zao katika mataifa yao, kila moja kwa lugha yake.)
Kutoka kwa hawa watu wa pwani waligawanyika na kwenda kwenye ardhi zao, kila mtu na lugha yake, kufuatana na koo zao, kwa mataifa yao.
6 Wana wa Hamu walikuwa: Kushi, Misraimu, Putu na Kanaani.
Wana wa Hamu walikuwa Kushi, Misraimu, Putu, na Kanaani.
7 Wana wa Kushi walikuwa: Seba, Havila, Sabta, Raama na Sabteka. Wana wa Raama walikuwa: Sheba na Dedani.
Wana wa Kushi walikuwa Seba, Havila, Sabta, Raama, na Sabteka. Wana wa Raama walikuwa Sheba na Dedani.
8 Kushi akamzaa Nimrodi, ambaye alikua akawa mtu shujaa duniani.
Kushi akamzaa Nimrodi, ambaye alikuwa hodari wa kwanza juu ya nchi.
9 Alikuwa mwindaji hodari mbele za Bwana. Ndiyo sababu watu husema, “Kama Nimrodi, hodari wa kuwinda mbele za Bwana.”
Alikuwa mwindaji mkuu mbele ya Yahwe. Hii ndiyo sababu hunenwa, “Kama Nimrod mwindaji mkuu mbele za Yahwe.”
10 Vituo vyake vya kwanza katika ufalme wake vilikuwa Babeli, Ereki, Akadi na Kalne katika Shinari.
Miji ya kwanza ya ufalme wake ilikuwa Babeli, Ereku, Akadi na Kalne, katika ichi ya Shinari.
11 Kutoka nchi ile alikwenda Ashuru, ambako alijenga Ninawi, Rehoboth-iri, Kala,
Kutoka katika nchi ile alikwenda Ashuru na akajenga Ninawi, Rehoboth- iri na Kala,
12 na Reseni, iliyo kati ya Ninawi na Kala; huo ndio mji mkubwa.
na Raseni ambao ulikuwa kati ya Ninawi na Kala. Ulikuwa mji mkubwa.
13 Misraimu alikuwa baba wa: Waludi, Waanami, Walehabi, Wanaftuhi,
Misraimu akazaa Waludi, Waanami, Walehabi, na Wanaftuhi,
14 Wapathrusi, Wakasluhi (hao ndio asili ya Wafilisti), na Wakaftori.
Wapathrusi na Wakasluhi ( ambao kwao Wafilisti walitokea), na Wakaftori.
15 Kanaani alikuwa baba wa: Sidoni mzaliwa wake wa kwanza, Hethi,
Kanaani akamzaa Sidono, mwanawe wa kwanza, na Hethi,
16 Wayebusi, Waamori, Wagirgashi,
pia na Myebusi, na Mwamori, Mgirgashi,
17 Wahivi, Waariki, Wasini,
Mhivi, Mwarki, Msini,
18 Waarvadi, Wasemari na Wahamathi. Baadaye koo za Wakanaani zilitawanyika,
Mwarvadi, Msemari, na Mhamathi. Baadaye koo za wakanaani zikasambaa.
19 na mipaka ya Kanaani ilienea kutoka Sidoni kuelekea Gerari hadi Gaza, kisha kuelekea Sodoma, Gomora, Adma na Seboimu, hadi kufikia Lasha.
Mpaka wa Wakanaani ulianzia Sidoni, katika mwelekeo wa Gerari, hata Gaza, na kama kuelekea Sodoma, Gomora, Adma, na Seboimu hata Lasha.
20 Hawa ni wana wa Hamu kwa koo zao na lugha zao, katika nchi zao na mataifa yao.
Hawa walikuwa wana wa Ham, kwa koo zao, kwa lugha zao, katika ardhi zao na katika mataifa yao.
21 Shemu ambaye ni ndugu mkubwa wa Yafethi, kwake kulizaliwa wana pia. Shemu alikuwa baba wa wana wote wa Eberi.
Pia walizaliwa wana kwa Shemu, ndugu yake mkubwa wa Yafethi. Shemu pia alikuwa baba yao na watu wote wa Eberi.
22 Wana wa Shemu walikuwa: Elamu, Ashuru, Arfaksadi, Ludi na Aramu.
Wana wa Shemu walikuwa Elamu, Ashuru, Alfaksadi, Ludi, na Aramu.
23 Wana wa Aramu walikuwa: Usi, Huli, Getheri na Mesheki.
Wana wa Aramu walikuwa ni Usi, Huli, Getheri, na Mashi.
24 Arfaksadi alikuwa baba wa Shela, naye Shela akamzaa Eberi.
Arfaksadi akamzaa Sela, na Sela akamzaa Eber.
25 Eberi akapata wana wawili: Mmoja wao aliitwa Pelegi, kwa kuwa wakati wake ndipo dunia iligawanyika; nduguye aliitwa Yoktani.
Eberi akazaa wana wawili wa kiume. Jina la mmoja aliitwa Pelegi maana katika siku zake nchi iligawanyika. Jina la ndugu yake aliitwa Yoktani.
26 Yoktani alikuwa baba wa: Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera,
Yoktani akamzaa Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera,
27 Hadoramu, Uzali, Dikla,
Hadoram, Uzali, Dikla,
28 Obali, Abimaeli, Sheba,
Obali, Abimaeli, Sheba,
29 Ofiri, Havila na Yobabu. Hawa wote walikuwa wana wa Yoktani.
Ofiri, Havila, na Yobabi. Hawa wote walikuwa wana wa Yoktani.
30 Nchi waliyoishi ilienea toka Mesha kuelekea Sefari kwenye nchi ya vilima iliyoko mashariki.
Mpaka wao ulikuwa unaanzia Mesha, hadi Sefari, mlima wa mashariki.
31 Hao ndio wana wa Shemu kwa koo zao na lugha zao, katika nchi zao na mataifa yao.
Hawa walikuwa wana wa Shemu, kulingana na koo zao na lugha zao, katika ardhi zao kulingana na mataifa yao.
32 Hizi ndizo koo za wana wa Noa, kufuatana na vizazi vyao, katika mataifa yao. Kutokana na hawa mataifa yalienea duniani kote baada ya gharika.
Hizi zilikuwa koo za wana wa Nuhu, kulingana na vizazi vyao, kwa mataifa yao. Kutokea kwa hawa mataifa yaligawanyika na kwenda juu ya nchi baada ya gharika.