< Wagalatia 1 >
1 Paulo mtume: si mtume wa wanadamu wala aliyetumwa na mwanadamu, bali na Yesu Kristo na Mungu Baba aliyemfufua Yesu kutoka kwa wafu;
我保祿宗徒──我蒙召為宗徒,非由於人,也並非藉著人,而是由於耶穌基督和使祂由死者中復活的天主父──
2 na ndugu wote walio pamoja nami: Kwa makanisa ya Galatia:
我和同我在一起的眾弟兄,致書給迦拉達眾教會:
3 Neema iwe nanyi na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana wetu Yesu Kristo,
恩寵與平安由天主我們的父及主耶穌基督賜與你們!
4 aliyejitoa kwa ajili ya dhambi zetu ili apate kutuokoa katika ulimwengu huu wa sasa ulio mbaya, sawasawa na mapenzi yake yeye aliye Mungu na Baba yetu. (aiōn )
這基督按照天主我們父的旨意, 為我們的罪惡捨棄了自己,為救我們脫離此邪惡的世代。 (aiōn )
5 Utukufu una yeye milele na milele. Amen. (aiōn )
願光榮歸於天主,至於無窮之世! 阿們。 (aiōn )
6 Nashangaa kwamba mnamwacha upesi hivyo yeye aliyewaita kwa neema ya Kristo na kuifuata Injili nyingine,
我真奇怪,你們竟這樣快離開了那以基督的恩寵召叫你們的天主,而歸向了另一福音;
7 ambayo kwa kweli si Injili kamwe, ila kwa dhahiri kuna watu wanaowachanganya na wanaotaka kuipotosha Injili ya Kristo.
其實,並沒有別的福音,只是有一些人攪亂你們,企圖以改變基督的福音而已。
8 Lakini hata ikiwa sisi au malaika atokaye mbinguni akihubiri Injili nyingine tofauti na ile tuliyowahubiria sisi, basi mtu huyo alaaniwe milele!
但是,無論誰,即使是我們,或是從天上降下的一位天使,若給你們宣講的福音,與我們給你們宣講的福音不同,當受詛咒。
9 Kama vile tulivyokwisha kusema kabla, sasa nasema tena, ikiwa mtu yeyote atawahubiria Injili kinyume na ile mliyoipokea na alaaniwe milele!
我們以前說過,如今我再說:誰若給你們宣講福音與你們所接受的不同,當受詛咒。
10 Je, sasa mimi ninatafuta kukubaliwa na wanadamu au kukubaliwa na Mungu? Au nataka kuwapendeza wanadamu? Kama ningekuwa bado najaribu kuwapendeza wanadamu, nisingekuwa mtumishi wa Kristo.
那麼,我如今是討人的喜愛,或是討天主的喜愛呢﹖難道我是尋求人的歡心嗎﹖如果我還求人的歡心,我就不是基督的僕役。
11 Ndugu zangu, nataka mjue kwamba Injili niliyowahubiria haikutokana na wanadamu.
弟兄們! 我告訴你們:我所宣講的福音,並不是由人而來的,
12 Kwa maana mimi sikuipokea hiyo Injili kutoka kwa mwanadamu, wala sikufundishwa na mtu, bali niliipata kwa ufunuo kutoka kwa Yesu Kristo.
因為,我不是由人得來的,也不是由人學來的,而是由耶穌基督的啟示得來的。
13 Ninyi mmekwisha kusikia juu ya maisha yangu ya zamani nilipokuwa katika dini ya Kiyahudi, jinsi nilivyolitesa kanisa la Mungu kwa nguvu na kujaribu kuliangamiza.
你們一定聽說過,我從前尚在猶太教中的行動:我怎樣激烈地迫害過天主的教會,竭力想把她消滅;
14 Nami niliendelea sana katika dini ya Kiyahudi kuliko Wayahudi wengi wa rika yangu maana nilijitahidi sana katika desturi za baba zangu.
我在猶太教中比我本族許多同年的人更為激進,對我祖先的傳授更富熱忱。
15 Lakini ilipompendeza Mungu, aliyenitenga tangu tumboni mwa mama yangu na kuniita kwa neema yake,
但是,從母胎中已經選拔我,以恩寵召叫我的天主,卻決意
16 alimdhihirisha Mwanawe kwangu, ili nipate kumhubiri miongoni mwa watu wa Mataifa. Mimi sikushauriana na mwanadamu yeyote,
將祂的聖子啟示給我,叫我在異民中傳揚祂。我當時沒有與任何人商量,
17 wala sikupanda kwenda Yerusalemu kuwaona hao waliokuwa mitume kabla yangu, bali nilikwenda mara moja Arabuni na kisha nikarudi Dameski.
也沒有上耶路撒冷去見那些在我在以前作宗徒的人,我立即去了阿剌伯,然後又回到大馬士革。
18 Kisha baada ya miaka mitatu nilipanda kwenda Yerusalemu kuonana na Kefa na nilikaa naye siku kumi na tano.
此後,過了三年,我才上耶路撒冷去拜見刻法,在他那裡逗留了十五天,
19 Lakini sikumwona mtume mwingine yeyote isipokuwa Yakobo, ndugu yake Bwana.
除了主的兄雅各伯,我沒有看見別的宗徒。
20 Nawahakikishia mbele za Mungu kuwa ninayowaandikia si uongo.
我給你們寫的都是真的,我在天主前作證,我決沒有說謊。
21 Baadaye nilikwenda sehemu za Syria na Kilikia.
此後,我往敘利亞和基里基雅地域去了。
22 Lakini mimi binafsi sikujulikana kwa makanisa ya huko Uyahudi yaliyo katika Kristo.
那時,猶太境內屬於基督的各教會,都沒有見過我的面;
23 Wao walisikia habari tu kwamba, “Mtu yule ambaye hapo kwanza alikuwa akitutesa sasa anahubiri imani ile ile aliyokuwa akijaribu kuiangamiza.”
只是聽說過:「那曾經迫害我們的,如今卻傳揚他曾經想消滅的信仰了。」
24 Nao wakamtukuza Mungu kwa sababu yangu.
他們就為了我而光榮天主。