< Ezra 7 >

1 Baada ya mambo haya, wakati wa utawala wa Artashasta mfalme wa Uajemi, Ezra mwana wa Seraya, mwana wa Azaria, mwana wa Hilkia,
And after these things, in the reign of Artaxerxes king of Persia, Ezra son of Seraiah, son of Azariah, son of Hilkiah,
2 mwana wa Shalumu, mwana wa Sadoki, mwana wa Ahitubu,
son of Shallum, son of Zadok, son of Ahitub,
3 mwana wa Amaria, mwana wa Azaria, mwana wa Merayothi,
son of Amariah, son of Azariah, son of Meraioth,
4 mwana wa Zerahia, mwana wa Uzi, mwana wa Buki,
son of Zerahiah, son of Uzzi, son of Bukki,
5 mwana wa Abishua, mwana wa Finehasi, mwana wa Eleazari, mwana wa kuhani mkuu Aroni.
son of Abishua, son of Phinehas, son of Eleazar, son of Aaron the head priest;
6 Huyu Ezra alipanda kutoka Babeli. Alikuwa mwalimu mwenye ujuzi mzuri katika sheria ya Mose, ambayo Bwana, Mungu wa Israeli, alikuwa ametoa. Mfalme alikuwa amempa Ezra kila kitu alichoomba, kwa maana Bwana Mungu wake alikuwa pamoja naye.
Ezra himself has come up from Babylon, and he [is] a scribe ready in the Law of Moses, that YHWH God of Israel gave, and the king gives to him—according to the hand of his God YHWH on him—all his request.
7 Pia baadhi ya Waisraeli, wakiwemo makuhani, Walawi, waimbaji, mabawabu na watumishi wa Hekalu, nao walikuja Yerusalemu mwaka wa saba wa utawala wa Mfalme Artashasta.
And there go up of the sons of Israel, and of the priests, and the Levites, and the singers, and the gatekeepers, and the Nethinim, to Jerusalem, in the seventh year of Artaxerxes the king.
8 Ezra aliwasili Yerusalemu mwezi wa tano wa mwaka wa saba wa utawala wa Mfalme Artashasta.
And he comes to Jerusalem in the fifth month, that [is in] the seventh year of the king,
9 Ezra alianza safari yake kutoka Babeli tangu siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza, naye akawasili Yerusalemu siku ya kwanza ya mwezi wa tano, kwa maana mkono wa neema wa Mungu wake ulikuwa juu yake.
for on the first of the month he has founded the ascent from Babylon, and on the first of the fifth month he has come to Jerusalem, according to the good hand of his God on him,
10 Kwa maana Ezra alikuwa amejitoa kwa moyo wote kujifunza na kushika sheria ya Bwana na kuwafundisha watu wa Israeli amri na sheria zake.
for Ezra has prepared his heart to seek the Law of YHWH, and to do, and to teach in Israel statute and judgment.
11 Hii ni nakala ya barua ambayo Mfalme Artashasta alikuwa amempa Ezra aliyekuwa kuhani na mwalimu, mtu aliyeelimika katika mambo yahusuyo maagizo na amri za Bwana kwa Israeli.
And this [is] a copy of the letter that King Artaxerxes gave to Ezra the priest, the scribe, a scribe of the words of the commands of YHWH, and of His statutes on Israel:
12 Artashasta, mfalme wa wafalme, Kwa Ezra kuhani, mwalimu wa Sheria ya Mungu wa mbinguni: Salamu.
“Artaxerxes, king of kings, to Ezra the priest, a perfect scribe of the Law of the God of the heavens, and at such a time:
13 Sasa naamuru kwamba mtu yeyote Mwisraeli katika ufalme wangu, pamoja na makuhani na Walawi, ambaye anataka kwenda Yerusalemu pamoja nawe aweza kwenda.
By me has been made a decree that everyone who is willing, in my kingdom, of the people of Israel and of its priests and Levites, to go to Jerusalem with you, go;
14 Unatumwa na mfalme na washauri wake saba kuchunguza kuhusu Yuda na Yerusalemu kulingana na Sheria ya Mungu wako, iliyoko mkononi mwako.
because that from the king and his seven counselors you are sent, to inquire concerning Judah and concerning Jerusalem, with the Law of God that [is] in your hand,
15 Zaidi ya hayo, uchukue pamoja nawe fedha na dhahabu ambazo mfalme na washauri wake wamempa Mungu wa Israeli kwa hiari, Mungu ambaye maskani yake yako Yerusalemu,
and to carry silver and gold that the king and his counselors willingly offered to the God of Israel, whose dwelling place [is] in Jerusalem,
16 pia fedha na dhahabu zote unazoweza kupata kutoka jimbo la Babeli, pamoja na sadaka za hiari watakazotoa watu na makuhani kwa ajili ya Hekalu la Mungu wao katika Yerusalemu.
and all the silver and gold that you find in all the province of Babylon, with the free-will offerings of the people, and of the priests, offering willingly, for the house of their God that [is] in Jerusalem,
17 Hakikisha kwamba fedha hizi zimetumika kununua mafahali, kondoo dume na wana-kondoo pamoja na sadaka za nafaka na sadaka za vinywaji, uvitoe dhabihu juu ya madhabahu ya Hekalu la Mungu wenu katika Yerusalemu.
therefore you speedily buy with this money, bullocks, rams, lambs, and their presents, and their drink-offerings, and bring them near to the altar of the house of your God that [is] in Jerusalem,
18 Kisha wewe na Wayahudi ndugu zako mnaweza kufanya lolote linaloonekana jema sana kwa fedha na dhahabu zilizosalia, kulingana na mapenzi ya Mungu wenu.
and that which to you and to your brothers is good to do with the rest of the silver and gold, according to the will of your God you do.
19 Uvitoe kwa Mungu wa Yerusalemu vyombo vyote ulivyokabidhiwa kwa ajili ya ibada katika Hekalu la Mungu wako.
And the vessels that are given to you, for the service of the house of your God, make perfect before the God of Jerusalem;
20 Kitu kingine chochote kinachohitajika kwa ajili ya Hekalu la Mungu wenu ambacho unatakiwa kukitoa, waweza kukitoa kutoka hazina ya mfalme.
and the rest of the necessary things of the house of your God, that it falls to you to give, you give from the treasure-house of the king.
21 Mimi, Mfalme Artashasta, sasa naagiza watunza hazina wote wa Ngʼambo ya Mto Frati kutoa kwa bidii chochote kwa Ezra kuhani na mwalimu wa Sheria ya Mungu wa mbinguni atakachohitaji kwenu,
And by me—I Artaxerxes the king—is made a decree to all treasurers who [are] beyond the river, that all that Ezra the priest, scribe of the Law of the God of the heavens, asks of you, be done speedily:
22 talanta 100 za fedha, ngano kori 100, divai bathi 100, mafuta ya zeituni bathi 100, na chumvi kiasi chochote.
To silver one hundred talents, and to wheat one hundred cors, and to wine one hundred baths, and to oil one hundred baths, and salt without reckoning;
23 Chochote ambacho Mungu wa mbinguni ameagiza, kifanyike kwa ukamilifu kwa ajili ya Hekalu la Mungu wa mbinguni. Kwa nini pawepo ghadhabu dhidi ya utawala wa mfalme na wanawe?
all that [is] by the decree of the God of the heavens, let be done diligently for the house of the God of the heavens; for why is there wrath against the kingdom of the king and his sons?
24 Pia ninyi fahamuni kuwa hamna mamlaka ya kuwatoza kodi, ushuru au ada makuhani, Walawi, waimbaji, mabawabu, watumishi wa Hekalu au wafanyakazi wengine kwenye nyumba ya Mungu.
And to you we are making known, that on any of the priests and Levites, singers, gatekeepers, Nethinim, and servants of the house of God, tribute and custom there is no authority to lift up.
25 Nawe Ezra, kufuatana na hekima ya Mungu wenu uliyo nayo, weka mahakimu na waamuzi wote wanaozifahamu sheria za Mungu wenu ili watoe haki kwa watu wote wa Ngʼambo ya Mto Frati. Nawe inakupasa umfundishe yeyote ambaye hazifahamu.
And you, Ezra, according to the wisdom of your God, that [is] in your hand, appoint magistrates—even judges who may be judging—judging all the people who are beyond the river, to all knowing the Law of your God, and he who has not known, you cause to know;
26 Yeyote ambaye hataitii sheria ya Mungu wenu pia sheria ya mfalme, hakika lazima aadhibiwe kwa kuuawa, kuhamishwa, kunyangʼanywa mali au kufungwa gerezani.
and any who does not do the Law of your God, and the law of the king, judgment is done speedily on him, whether to death, or to banishment, or to confiscation of riches, and to bonds.”
27 Sifa ziwe kwa Bwana, Mungu wa baba zetu, Mungu ambaye kwa njia hii ameweka ndani ya moyo wa mfalme kuipa heshima nyumba ya Bwana iliyoko Yerusalemu, kwa namna hii
Blessed [is] YHWH, God of our fathers, who has given such a thing as this in the heart of the king, to beautify the house of YHWH that [is] in Jerusalem,
28 ambaye ameniongezea kibali chake mbele ya mfalme, washauri wake na maafisa wote wa mfalme wenye uwezo. Kwa kuwa mkono wa Bwana Mungu wangu ulikuwa pamoja nami, nilijipa moyo nikakusanya watu walio viongozi kutoka Israeli wakwee pamoja nami.
and to me has stretched out kindness before the king and his counselors, and before all the mighty heads of the king: and I have strengthened myself as the hand of my God YHWH [is] on me, and I gather out of Israel heads to go up with me.

< Ezra 7 >