< Ezra 3 >

1 Mwezi wa saba ulipowadia baada ya Waisraeli kukaa katika miji yao, watu wote walikusanyika huko Yerusalemu kama mtu mmoja.
Ilikuwa miezi saba baaada ya watu wa Israeli kurudi kwenye miji yao, ndipo walipojikusanya pamoja kama mtu mmoja katika Yerusalem.
2 Yeshua mwana wa Yosadaki na makuhani wenzake, Zerubabeli mwana wa Shealtieli pamoja na wenzake walianza kujenga madhabahu ya Mungu wa Israeli ili kumtolea dhabihu za sadaka za kuteketezwa kwa moto juu yake, kulingana na ilivyoandikwa katika Sheria ya Mose mtu wa Mungu.
Yeshua mwana wa Yosadaki na kaka yake kuhani, na Zerubabeli mwana wa Sheatieli na kaka yake wakainuka na kujenga madhabahu ya Mungu wa Israeli na kutoa sadaka ya kuteketezwa kama ilivyoagizwa katika sheria ya Musa, Mtu wa Mungu.
3 Ingawa waliwaogopa watu waliowazunguka, walijenga madhabahu juu ya ule msingi wake, wakamtolea Bwana dhabihu za sadaka za kuteketezwa kwa moto juu yake za asubuhi na za jioni.
Ndipo wakaanzisha madhabahu juu ya msingi, kwa hofu waliokuwa nayo kwa sababu ya watu wa nchi/ Wakatoa sadaka ya kuteketezwa kwa Yahwe asubuhi na jioni.
4 Kisha kulingana na kile kilichoandikwa, wakaiadhimisha Sikukuu ya Vibanda wakitoa idadi ya sadaka za kuteketezwa kama ilivyohitajika kila siku sawasawa na ilivyoagizwa.
Pia vilevile wakaichunguza sikukuu ya vibanda kama ilivyoandikwa na wakatoa sadaka ya kuteketezwa siku kwa siku kama ilivyoagizwa, kila siku kwa siku yake.
5 Baada ya hayo, walitoa sadaka za kuteketezwa za kawaida, sadaka za Mwezi Mwandamo na dhabihu zote za sikukuu takatifu za Bwana zilizoamriwa, pamoja na zile sadaka za hiari zilizotolewa kwa Bwana.
Kulikuwa na sadaka ya kila siku ya kuteketezwa na mwezi mara moja na sadaka za siku ya Yahwe za kudumu, pamoja na sadaka zote za hiari.
6 Ingawa bado msingi wa Hekalu la Bwana ulikuwa haujawekwa, watu walianza kutoa sadaka za kuteketezwa kwa moto kwa Bwana tangu siku ya kwanza ya mwezi wa saba.
Walianza kutoa sadaka za kuteketezwa za Yahwe siku ya kwanza ya mwezi wa saba, ingawa hekalu lilikuwa halijaanza kujengwa.
7 Kisha watu wakawapa mafundi wa uashi na useremala fedha, wakawapa watu wa Sidoni na Tiro vyakula, vinywaji na mafuta ili waweze kuleta magogo ya mierezi kwa njia ya bahari kutoka Lebanoni hadi Yafa, kama alivyoagiza Koreshi mfalme wa Uajemi.
Hivyo wakatoa fedha kwa wahunzi na fundi wa mkono, na wakawapa chakula, vinywaji na mafuta kwa watu wa Sidoni na Tiro, ili kwamba walete miti ya mierezi kupitia baharini kutoka Lebanoni mpaka Yafa, na kama walivyo ruhusiwa na mfalme Koreshi wa Uajemi.
8 Katika mwezi wa pili wa mwaka wa pili baada ya Waisraeli kufika kwenye nyumba ya Mungu huko Yerusalemu, Zerubabeli mwana wa Shealtieli, Yeshua mwana wa Yosadaki na ndugu zao wengine (makuhani, Walawi na wote waliorejea Yerusalemu kutoka uhamishoni) walianza kazi, wakiteua Walawi wenye umri kuanzia miaka ishirini au zaidi kusimamia ujenzi wa nyumba ya Bwana.
Ndipo mwezi wa pili katika mwaka wa pili baadae wakaja kwenye nyumba ya Mungu Yerusalem, Zerubabeli, Yoshua mwana wa Yosadaki, na baadhi ya makuhani na walawi na wale walikuja kutoka uhamishoni kurudi Yerusalem wakaanza kazi. Wakawachagua walawi walikuwa na miaka ishirini na zaidi kusimamia kazi ya nyumba ya Yahwe,
9 Yeshua na wanawe, pamoja na ndugu zake, Kadmieli na wanawe (wazao wa Hodavia), wana wa Henadadi na wana wao na ndugu zao, Walawi wote walijiunga pamoja kusimamia wale waliofanya kazi katika nyumba ya Mungu.
Yoshua akamsimamisha kijana wake na kaka yake, Kadmiel na watoto wake, na kizazi cha yuda kusimamia kufanya kazi katika nyumba ya Mungu. Pamoja na wao kulikuwa na wana wa Henadadi, na uzao wao, na pia jamaa zao walawi.
10 Wajenzi walipoweka msingi wa Hekalu la Bwana, makuhani wakiwa wamevalia mavazi yao wakiwa na tarumbeta na Walawi (wana wa Asafu) wakiwa na matoazi, walishika nafasi zao za kumtukuza Bwana, kama ilivyoagizwa na Daudi mfalme wa Israeli.
Wajenzi wakasimamisha msingi wa Hekalu la Yahwe, Na hii ikawawezesha makuhani kusimama na mavazi yao wakiwa na tarumbeta, na walawi wana wa Asafu, kumtukuza Yahwe kwa matoazi, kama mkono wa mfalme Daudi wa Israel alivyoagiza.
11 Waliimba nyimbo za sifa na za shukrani kwa Bwana hivi: “Yeye ni mwema; upendo wake kwa Israeli wadumu milele.” Watu wote wakapaza sauti kubwa za sifa kwa Bwana, kwa sababu msingi wa nyumba ya Bwana ulikuwa umewekwa.
Waliimba kwa kumsifu na kumshukuru Yahwe. “Yeye ni mwema! Agano lake ni kweli kwa Israel ladumu milele.”Watu wote wakapiga kelele kwa sauti kuu za shangwe wakimsifu Yahwe kwa sababu misingi ya Hekalu ilikuwa imekamilika.
12 Lakini wengi wa makuhani wazee, Walawi na viongozi wa jamaa waliokuwa wameona Hekalu la mwanzoni, walilia kwa sauti walipoona msingi wa Hekalu hili ukiwekwa, huku wengine wengi wakipiga kelele kwa furaha.
Lakini wengi wa Makuhani, walawi, wakuu wa kale, na wazeee wa zamani walioiona nyumba ya kwanza, wakati misingi ilipowekwa wakaishuhudia kwa macho yao, walilia kwa sauti. Lakiniwengi walipiga kelele kwa sauti za shangwe na furaha na sauti za kushangaza.
13 Hakuna mtu ambaye angeweza kutofautisha sauti hizo za furaha na za kilio, kwa sababu watu walipiga kelele sana. Nayo hiyo sauti ikasikika mbali.
Na matokeo yake, watu hawakuweza kutofautisha sauti za furaha na sauti za shangwe na sauti za watu waliokuwa wanalia, kwa kuwa watu walikuwa wanalia kwa sauti kuu ya shangwe na sauti ilisikika kutoka mbali.

< Ezra 3 >