< Ezra 2 >

1 Basi hawa ndio watu wa jimbo waliotoka uhamishoni, ambao Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuwa amewachukua mateka hadi Babeli (walirudi Yerusalemu na Yuda, kila mmoja kwenye mji wake,
Hawa ndio watu katika jimbo waliochukuliwa mateka na kwenda na mfalme Nebukadneza, yeye aliwachukua utumwani Babeli, watu wakarudi katika miji yao ya Yerusalem na Yuda.
2 wakiwa wamefuatana na Zerubabeli, Yeshua, Nehemia, Seraya, Reelaya, Mordekai, Bilshani, Mispari, Bigwai, Rehumu na Baana): Orodha ya wanaume kati ya watu wa Israeli ilikuwa:
Walikuja pamoja na Zerubabeli, Yoshua, Nehemia, Seraya, Reelaya, Mordekai, Bilshani, Mispari., Bigwai, Rehumu, na Baana. Hii ndio idadi ya wanaume ya watu wa Israeli.
3 wazao wa Paroshi 2,172
Waporoshi: 2, 172
4 wazao wa Shefatia 372
Wana wa Shefatia: 372
5 wazao wa Ara 775
Wana wa Ara: 775.
6 wazao wa Pahath-Moabu (wa jamaa ya Yeshua na Yoabu) 2,812
Wana wa Path-Moabu, kupitia Yeshua na Yoabu: 2, 812.
7 wazao wa Elamu 1,254
Wana wa Eliamu: 1, 254.
8 wazao wa Zatu 945
Wana wa Zatu: 945.
9 wazao wa Zakai 760
Wana wa Zakai: 760.
10 wazao wa Bani 642
Wana wa Binui: 642.
11 wazao wa Bebai 623
Wana wa Bebai: 623.
12 wazao wa Azgadi 1,222
Wana wa Azgadi: 1, 222.
13 wazao wa Adonikamu 666
Wana wa Adonikamu: 666.
14 wazao wa Bigwai 2,056
Wana wa Bigwai: 2, 056.
15 wazao wa Adini 454
Wana wa Adini: 454.
16 wazao wa Ateri (kupitia Hezekia) 98
Wana wa Ateri kupitia Hezekiah: tisini na nane.
17 wazao wa Besai 323
Wana wa Besai: 323.
18 wazao wa Yora 112
Wana wa Harifu: 112.
19 wazao wa Hashumu 223
Wanaume wa Hashimu: 223.
20 wazao wa Gibari 95
Wanaume wa Gibeoni: Tisini na tano.
21 watu wa Bethlehemu 123
Wanaume wa Bethlehemu: 123.
22 watu wa Netofa 56
Wanaume wa Netofa: Hamsini na sita.
23 watu wa Anathothi 128
Wanaume wa Anathothi: 128.
24 watu wa Azmawethi 42
Wanaume wa Beth-Azmawethi: Arobaini na mbili.
25 wazao wa Kiriath-Yearimu, Kefira na Beerothi 743
Wanaume wa Kiriath-Yearimu, na Kefira, na Beerothi: Mia saba arobaini na tatu.
26 wazao wa Rama na Geba 621
Wanaume wa Rama na Geba: 621.
27 watu wa Mikmashi 122
Wanaume wa Mikmashi: 122.
28 watu wa Betheli na Ai 223
Wanaume wa Betheli, na Ai: 223.
29 wazao wa Nebo 52
Wanaume wa Nebo: Hamsini na mbili.
30 wazao wa Magbishi 156
Wanaume wa Magbishi: 156.
31 wazao wa Elamu ile ingine 1,254
Wanaume wengine wa Elamu: 1, 254.
32 wazao wa Harimu 320
nne. Wanaume wa Harimu: 320.
33 wazao wa Lodi, Hadidi na Ono 725
Wanaume wa Lodi, na Hadidi, na Ono: 725.
34 wazao wa Yeriko 345
Wanaume wa Yeriko: 345.
35 wazao wa Senaa 3,630
Wanaume wa Senaa: 3, 630.
36 Makuhani: wazao wa Yedaya (kwa jamaa ya Yeshua) 973
Wana wa Yedaya kuhani wa nyumba ya Yoshua: 973.
37 wazao wa Imeri 1,052
Wana wa Imeri: 1, 052.
38 wazao wa Pashuri 1,247
Wana wa Pashuri: 1, 247.
39 wazao wa Harimu 1,017
Wana wa Harimu: 1, 017.
40 Walawi: wazao wa Yeshua na Kadmieli (kupitia jamaa ya Hodavia) 74
Walawi: Wana wa Yeshua, na Kadmieli, wana wa Hodavia: Sabini na
41 Waimbaji: wazao wa Asafu 128
nne. Waimbaji hekaluni wana wa Asafu: 128.
42 Mabawabu wa lango la Hekalu: wazao wa Shalumu, Ateri, Talmoni, Akubu, Hatita na Shobai 139
Walinzi: wana wa Shalumu, Ateri na, Talmoni, Akubu, Hatita na Shobai: 139 jumla.
43 Watumishi wa Hekalu: wazao wa Siha, Hasufa, Tabaothi,
Wale walichaguliwa kuhudumu ndani ya Hekalu: wana wa Siha, Hasufa, Tabaothi:
44 wazao wa Kerosi, Siaha, Padoni,
Keros, Siaha, Padoni.
45 wazao wa Lebana, Hagaba, Akubu,
Lebana, Hagaba, Akubu,
46 wazao wa Hagabu, Shalmai, Hanani,
Hagabu, Salmai, Hanani
47 wazao wa Gideli, Gahari, Reaya,
Wana wa Gideli, Gahari, Reaya,
48 wazao wa Resini, Nekoda, Gazamu,
Resini, Nekoda, Gazamu,
49 wazao wa Uza, Pasea, Besai,
Uza, Pasea, Besai,
50 wazao wa Asna, Meunimu, Nefusimu,
Asna, Meunimu, Nefusimu:
51 wazao wa Bakbuki, Hakufa, Harhuri,
Wana wa Bakbuki, Hakufa, Harhuri:
52 wazao wa Basluthi, Mehida, Harsha,
Basluthi, Mehida, Barsha:
53 wazao wa Barkosi, Sisera, Tema,
Barkosi, Sisera, Tema:
54 wazao wa Nesia na Hatifa.
Nesia, Tefa
55 Wazao wa watumishi wa Solomoni: wazao wa Sotai, Hasaferethi, Peruda,
Wana wa watumishi wa Selemani: Wana wa Sotai, Soferethi, Peruda,
56 wazao wa Yaala, Darkoni, Gideli,
Yaala, Darkoni, Gideli,
57 wazao wa Shefatia, Hatili, Pokereth-Hasebaimu na Ami.
Shefatia, Hatili, Pokereth-Sebaimu, Amoni,
58 Watumishi wa Hekalu wote na wazao wa watumishi wa Solomoni 392
Walikuwa jumla ya watumishi mia tatu tisini na mbili waliochaguliwa kutumika katika Hekalu pamoja na wana wa watumishi wa Selemani.
59 Wafuatao walikuja kutoka miji ya Tel-Mela, Tel-Harsha, Kerubu, Adoni na Imeri, lakini hawakuweza kuthibitisha kwamba jamaa zao zilikuwa uzao wa Israeli:
Wale ambao walitoka Tel-mela, Tel-harsha, Kerubu, Adani, na Imeri, Lakini hawakuweza kuthibitisha kizazi chao kilitoka Israeli-
60 wazao wa Delaya, Tobia na Nekoda 652
pamoja na mia sita hamsini na mbili wana wa Delaya, Tobia na Nekoda.
61 Kutoka miongoni mwa makuhani: Wazao wa Hobaya, Hakosi, Barzilai (mtu aliyekuwa amemwoa binti wa Barzilai, Mgileadi, naye akaitwa kwa jina hilo).
Vilevile, kutoka kwa wana wa kuhani: Wana wa Habaya, Hakosi, Barzilai (ambaye alipata mke kutoka kwa binti ya Barzilai, Mgileadi na akaitwa kwa jina lao)
62 Hawa walitafuta orodha za jamaa zao, lakini hawakuonekana humo, kwa hiyo waliondolewa kutoka kundi la makuhani kwa kuwa walihesabiwa kuwa najisi.
Walitafuta kumbukumbu ya kizazi chao, lakini haikupatikana, hivyo wakaondolewa kwenye ukuhani kama wasiosafi.
63 Mtawala aliagiza kuwa wasile chochote miongoni mwa vyakula vitakatifu hadi kuwe kuhani atakayehudumu kwa Urimu na Thumimu.
Hivyo kiongozi akawakataza wasile kitu chochote kitakatifu kilichotakaswa mpaka kuhani mwenye Urimu na Thumimu athibitishe.
64 Jumla ya watu wote waliorudi walikuwa 42,360;
Jumla ya kundi 42, 360,
65 tena zaidi ya hao walikuwepo watumishi wa kiume na wa kike 7,337; pia walikuwamo waimbaji wanaume na wanawake 200.
ukiondoa watumishi na wasaidizi (wao walikuwa 7, 337) waimbaji Hekaluni wanaume na wanawake (mia mbili)
66 Walikuwa na farasi 736, nyumbu 245,
Farasi wao: 736, Nyumbu wao: 245.
67 ngamia 435 na punda 6,720.
Ngamia wao: 435. Punda wao: 6, 720.
68 Walipofika kwenye nyumba ya Bwana huko Yerusalemu, baadhi ya viongozi wa jamaa walitoa sadaka za hiari kwa ajili ya kujenga upya nyumba ya Mungu katika eneo lake.
Walipokwenda kwenye nyumba ya Yahwe Yerusalem, wakuu wa mababa walijitoa kwa hiari kujenga nyumba.
69 Wakatoa kwa kadiri ya uwezo wao na kutia katika hazina darkoni 61,000 za dhahabu, mane 5,000 za fedha, na mavazi 100 ya ukuhani kwa ajili ya kazi hiyo.
Walitoa kadiri ya uwezo wao katika kufadhili kazi: Dhahabu za darkoni sitini na moja elfu, mane za fedha elfi tano na mavazi mia moja ya makuhani.
70 Makuhani, Walawi, waimbaji, mabawabu, na watumishi wa Hekalu waliishi katika miji yao wenyewe, pamoja na baadhi ya watu wengine, nao Waisraeli waliosalia waliishi katika miji yao.
Basi makuhani na walawi, watu, waimbaji hekaluni, na walinzi wa getini, na wale waliochaguliwa kutumika katika Hekalu walikaa katika miji yao. Watu wote katika Israel walikuwa katika miji yao.

< Ezra 2 >