< Ezra 10 >
1 Wakati Ezra alipokuwa anaomba na kuungama, huku akilia na kujitupa chini mbele ya nyumba ya Mungu, umati mkubwa wa Waisraeli, wanaume, wanawake na watoto walikusanyika kumzunguka. Nao pia wakalia sana.
Wakati Ezra akiomba na kutubu, akalia na kujirusha chini mbele ya nyumba ya Mungu, kusanyiko kubwa la wanaume Israel, wanawake na watoto wakakusanyika kwake, kwa kuwa watu walikuwa wakilia sana.
2 Kisha Shekania mwana wa Yehieli, mmoja wa wazao wa Elamu, akamwambia Ezra, “Tumekosa uaminifu kwa Mungu wetu kwa kuoa wanawake wa kigeni kutoka mataifa yanayotuzunguka. Lakini pamoja na hili, bado liko tumaini kwa ajili ya Israeli.
Shekania mtoto wa Yehieli, mwana wa Elamu akamwambia Ezra, “Tumekuwa sio waaminifu kwa Mungu na tumeoa wanawake wa kigeni kutoka nchi nyingine. Lakini pamoja na hilo, bado kuna tumaini kwa Israel.
3 Sasa na tufanye agano mbele za Mungu wetu kuwafukuza hawa wanawake wote pamoja na watoto wao, kulingana na maonyo ya bwana wangu pamoja na wale ambao wanaogopa amri za Mungu wetu. Hili na lifanyike sawasawa na hii Sheria.
sasa natuweke agano pamoja na Mungu wetu kuwaondoa wanawake wote na watoto wao kulingana na maelekezo ya Bwana, na maelekezo ya wale wanaotetemeka kutokana na amri za Mungu wetu. na hii ifanyike kutokana na sheria.
4 Inuka, suala hili lipo mikononi mwako. Sisi tutaungana nawe, uwe na ujasiri ukatende hili.”
Simama, jambo hili linakuhusu wewe, na sisis tuko pamoja na wewe, Uwe imara na kufanya hili.
5 Basi Ezra akainuka na kuwaapisha makuhani viongozi, Walawi na Israeli yote kufanya lile lililokuwa limependekezwa. Nao wakaapa.
Hivyo Ezra akasimama na kufanya makuhani na walawi na waisrael wote wakaahidi kufanya kwa njia hiyo. Hivyo wote wakatoa kiapo.
6 Ndipo Ezra akaondoka hapo mbele ya nyumba ya Mungu akaenda kwenye chumba cha Yehohanani mwana wa Eliashibu. Wakati alipokuwa hapo, hakula chakula wala hakunywa maji, kwa sababu aliendelea kuomboleza kuhusu kukosa uaminifu kwa watu wa uhamishoni.
Ndipo Ezra akainuka kutoka mbele ya nyumba ya Mungu na kwenda kwenye chumba ya Yehohanani mtoto wa Eliashibu, Yeye hakula mkate au kunywa maji. Tangu alipokuwa akiomboleza kuhusiana na wale wenye imani haba waliokuwa uhamishoni.
7 Ndipo lilipotolewa tangazo Yuda yote na Yerusalemu kwa watu wote waliokuwa uhamishoni kukusanyika Yerusalemu.
Hivyo wakatuma neno katika Yuda na Yerusalem kwa watu wote waliorudi kutoka utumwani kukusanyika Yerusalem.
8 Yeyote ambaye hangejitokeza kwa muda wa siku tatu angepoteza mali yake yote, kulingana na uamuzi wa maafisa na wazee, naye mtu huyo angefukuzwa kutoka kusanyiko la watu waliokuwa uhamishoni.
Yeyote ambaye hakuja katika siku tatu kutokana na maelekezo kutoka kwa wakuu na viongozi atachukuliwa mali zote na atatengwa na kusanyiko kuu la watu ambao walikuja kutoka uhamisho.
9 Katika muda wa siku tatu, watu wote wa Yuda na Benyamini wakawa wamekusanyika huko Yerusalemu. Kwenye siku ya ishirini ya mwezi wa tisa, watu wote walikuwa wameketi ndani ya uwanja mbele ya nyumba ya Mungu, wakiwa na majonzi mno kwa tukio hilo na kwa sababu ya mvua kubwa.
Hivyo watu wote wa Yuda na Benjamini wakakusanyika Yerusalem kwa siku tatu. Ilikuwa ni mwezi wa tisa na siku ya ishirini ya mwezi. watu wote wakasimama mbele ya nyumba ya Mungu na wakatetemeka kwa sababu ya neno na mvua.
10 Ndipo Kuhani Ezra aliposimama akawaambia, “Mmekosa uaminifu, mmeoa wanawake wa kigeni, mkaongezea hatia ya Israeli.
Ezra kuhani akasimama na kusema, “Ninyi wenyewe mmefanya uasi, ninyi mmeishi na wanawake wa kigeni na kuongeza makosa ya Israel.
11 Sasa tubuni kwa Bwana, Mungu wa baba zenu mkafanye mapenzi yake. Jitengeni na mataifa wanaowazunguka na wake zenu wa kigeni.”
Lakini sasa mpeni sifa Yahwe, Mungu wa watangulizi wenu, na mfanye mapenzi yake, mjitenge na watu wa nchi na wanawake wa kigeni.
12 Kusanyiko lote likajibu kwa sauti kubwa: “Uko sawa kabisa! Ni lazima tufanye kama unavyosema.
Kusanyiko lote likajibu kwa sauti. “Tutatenda kama ulivyosema,
13 Lakini hapa pana watu wengi na ni wakati wa mvua, hivyo hatuwezi kusimama nje. Hata hivyo, shauri hili haliwezi kumalizika kwa siku moja au mbili, kwa sababu tumefanya dhambi kubwa katika jambo hili.
haijalishi, kuna watu wengi na ni kipindi cha mvua. Hatuna nguvu ya kusimama nje na hii si siku moja au mbili za kufanya kazi, kwa kuwa tumekosea katika jambo hili.
14 Maafisa wetu na wafanye kwa niaba ya kusanyiko lote. Kisha kila mmoja katika miji yetu ambaye ameoa mwanamke wa kigeni aje kwa wakati uliopangwa, akiwa pamoja na wazee na waamuzi wa kila mji, hadi hasira kali ya Mungu wetu katika shauri hili itakapoondolewa kwetu.”
Hivyo wakuu wetu wawakilishe kusanyiko lote, iwe kwamba wote walioruhusu wanawake wa kigeni kuishi katika miji yetu waje katika muda uliopangwa na viongozi wa mji na waamuzi wa mji hadi hapo hasira ya Mungu itakapoondoka kutoka kwetu.
15 Yonathani mwana wa Asaheli na Yazeya mwana wa Tikwa peke yao, wakiungwa mkono na Meshulamu na Shabethai Mlawi, ndio waliopinga jambo hili.
Yonathan mtoto Asaheli na Yazeya mwana wa Tikwa wakapinga hili, Meshulamu na Shabethai mlawi wakawaunga mkono wao.
16 Basi watu wa uhamishoni wakafanya kama ilivyokuwa imependekezwa. Kuhani Ezra akachagua wanaume waliokuwa viongozi wa jamaa, mmoja kutoka kila mgawanyo wa jamaa, nao wote wakachaguliwa kwa majina. Katika siku ya kwanza ya mwezi wa kumi waliketi kuchunguza mashauri hayo.
Hivyo watu waliotoka uhamishoni wakafanya hivi, Ezra kuhani akachagua wanaume, viongozi watamgulizi wa ukoo na nyumba, wao wote kwa majina na wakaliangalia suala hili siku ya kwanza ya mwezi wa kumi.
17 Katika siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza wakawa wamemaliza kushughulikia wanaume wote waliokuwa wameoa wanawake wa kigeni.
Siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza wakawa wamemaliza kuchunguza wale wanaume walioishi na wanawake wa kigeni.
18 Miongoni mwa wazao wa makuhani, wafuatao walikuwa wameoa wanawake wa kigeni: Kutoka wazao wa Yeshua mwana wa Yosadaki na ndugu zake: Maaseya, Eliezeri, Yaribu na Gedalia.
Miongoni mwa wana wa kikuhani kuna wale walioishi na wanawake wa kigeni. Miongoni mwa wana wa Yoshua mtoto wa Yosadaki na kaka zake ambao walikuwa Maasela, Eliazeri, na Yaribu na Gedalia.
19 (Wote walitoa nadhiri kwa kuandika kwa mikono yao kuwafukuza wake zao, kwa hatia yao, kila mmoja akatoa kondoo dume kutoka kundini mwake kama sadaka ya hatia.)
Hivyo wakaamua kuwaondoa wake zao. kwa kuwa walikuwa na makosa, wakatoa sadaka ya kondoo kwenye mifugo kwa ajili ya makosa yao.
20 Kutoka wazao wa Imeri: Hanani na Zebadia.
Miongoni mwa wana wa Imeri, Hanani, na Zebadia.
21 Kutoka wazao wa Harimu: Maaseya, Eliya, Shemaya, Yehieli na Uzia.
Miongoni mwa wana wa Harimu, Maaseya, na Eliya na Shemaya, na Yehieli na Uzia.
22 Kutoka wazao wa Pashuri: Elioenai, Maaseya, Ishmaeli, Nethaneli, Yozabadi na Elasa.
Miongoni mwa wana wa Pashuri, Elasa
23 Miongoni mwa Walawi: Yozabadi, Shimei, Kelaya (ndiye Kelita), Pethahia, Yuda na Eliezeri.
Miongoni mwa walawi: Yozabadi na Shimei na Kelaya (ndiye Kelita) na Pethaia, na Yuda na Eliezeri. Miongoni mwa waimbaji Eliashibu na. Miongoni mwa walinzi Shalumu, Telemu na Uri.
24 Kutoka waimbaji: Eliashibu. Kutoka mabawabu: Shalumu, Telemu na Uri.
Miongoni mwa Israel waliobaki -
25 Miongoni mwa Waisraeli wengine: Kutoka wazao wa Paroshi: Ramia, Izia, Malkiya, Miyamini, Eleazari, Malkiya na Benaya.
Miongoni mwa wana wa Paroshi, Ramia na Izia na Malkiya na Miyamini na Eliazari na Malkiya na Benaya
26 Kutoka wazao wa Elamu: Matania, Zekaria, Yehieli, Abdi, Yeremothi na Eliya.
Miongoni mwa wana wa Elamu Mataniana Zekaria, na yeehieli, na Abdi na Yeremothi na Eliya.
27 Kutoka wazao wa Zatu: Elioenai, Eliashibu, Matania, Yeremothi, Zabadi na Aziza.
Miongoni mwa wana wa Zatu: Elionai, na Eliashibu, na Matania na Yeremothi na Zabadi na Aziza.
28 Kutoka uzao wa Bebai: Yehohanani, Hanania, Zabai na Athlai.
Miongoni mwa wana wa Bebai Yehohanani, na Hanania na Zakai na Athlai.
29 Kutoka wazao wa Bani: Meshulamu, Maluki, Adaya, Yashubu, Sheali na Yeremothi.
Miongoni mwa wana wa bani: Meshulami na Maluki, na Adaya na Yashubu na Sheali na Yeremothi.
30 Kutoka wazao wa Pahath-Moabu: Adna, Kelali, Benaya, Maaseya, Matania, Bezaleli, Binui na Manase.
Miongoni mwa wana wa Pahath-Moabu, Adna, na kelali, na Benaya na Maaseya, na Matania, na Besaleli na Binti na Manase.
31 Kutoka wazao wa Harimu: Eliezeri, Ishiya, Malkiya, Shemaya, Shimeoni,
Na miongoni mwa wana wa Harimu: Eliezeri na Ishiya, na Malkiya na Shemaya na Shimeoni, na
32 Benyamini, Maluki, na Shemaria.
Benyamini na Maluki na Shemaria
33 Kutoka wazao wa Hashumu: Matenai, Matata, Zabadi, Elifeleti, Yeremai, Manase na Shimei.
Miongoni mwa wana Hashumu: Matenai, na Matatana Zabadi, na Elifereti na Yeremai, na Manase, na Shimei.
34 Kutoka wazao wa Bani: Maadai, Amramu, Ueli,
Miongoni mwa wana wa Bani: Maadai, na Amramu na Aueli, na
35 Benaya, Bedeya, Keluhi,
Benaya, na Bedeya na Keluhi, na
36 Vania, Meremothi, Eliashibu,
wania, na Meremothi, Eliashibu,
37 Matania, Matenai na Yaasu.
Matania, na Matenai. na
38 Kutoka wazao wa Binui: Shimei,
Yaasi. Miongoni mwa wana wa Binui: Shimei,
39 Shelemia, Nathani, Adaya,
Sheremia, na Nathani, na Adaya, na
40 Maknadebai, Shashai, Sharai,
Maknadebai, na Shashai, na Sharai
41 Azareli, Shelemia, Shemaria,
Azareri, na Sheremia, na Shemaria, na
42 Shalumu, Amaria na Yosefu.
Shalumu, na Amaria, na Yusufu.
43 Kutoka wazao wa Nebo: Yeieli, Matithia, Zabadi, Zebina, Yadai, Yoeli na Benaya.
Miongoni wa wana wa Nebo: Yeieli, na Mathiana zabadi, na Zebina, na Ido, na Yoeli na Benaya.
44 Hawa wote walikuwa wameoa wanawake wa kigeni, na baadhi yao walikuwa wamezaa nao watoto.
Hawa wote walikuwa wameoa wanawake wa kigeni na walikuwa wamezaa watoto baadhi yao.