< Ezra 10 >

1 Wakati Ezra alipokuwa anaomba na kuungama, huku akilia na kujitupa chini mbele ya nyumba ya Mungu, umati mkubwa wa Waisraeli, wanaume, wanawake na watoto walikusanyika kumzunguka. Nao pia wakalia sana.
וכהתפלל עזרא וכהתודתו בכה ומתנפל לפני בית האלהים נקבצו אליו מישראל קהל רב מאד אנשים ונשים וילדים--כי בכו העם הרבה בכה
2 Kisha Shekania mwana wa Yehieli, mmoja wa wazao wa Elamu, akamwambia Ezra, “Tumekosa uaminifu kwa Mungu wetu kwa kuoa wanawake wa kigeni kutoka mataifa yanayotuzunguka. Lakini pamoja na hili, bado liko tumaini kwa ajili ya Israeli.
ויען שכניה בן יחיאל מבני עולם (עילם) ויאמר לעזרא--אנחנו מעלנו באלהינו ונשב נשים נכריות מעמי הארץ ועתה יש מקוה לישראל על זאת
3 Sasa na tufanye agano mbele za Mungu wetu kuwafukuza hawa wanawake wote pamoja na watoto wao, kulingana na maonyo ya bwana wangu pamoja na wale ambao wanaogopa amri za Mungu wetu. Hili na lifanyike sawasawa na hii Sheria.
ועתה נכרת ברית לאלהינו להוציא כל נשים והנולד מהם בעצת אדני והחרדים במצות אלהינו וכתורה יעשה
4 Inuka, suala hili lipo mikononi mwako. Sisi tutaungana nawe, uwe na ujasiri ukatende hili.”
קום כי עליך הדבר ואנחנו עמך חזק ועשה
5 Basi Ezra akainuka na kuwaapisha makuhani viongozi, Walawi na Israeli yote kufanya lile lililokuwa limependekezwa. Nao wakaapa.
ויקם עזרא וישבע את שרי הכהנים הלוים וכל ישראל לעשות כדבר הזה--וישבעו
6 Ndipo Ezra akaondoka hapo mbele ya nyumba ya Mungu akaenda kwenye chumba cha Yehohanani mwana wa Eliashibu. Wakati alipokuwa hapo, hakula chakula wala hakunywa maji, kwa sababu aliendelea kuomboleza kuhusu kukosa uaminifu kwa watu wa uhamishoni.
ויקם עזרא מלפני בית האלהים וילך אל לשכת יהוחנן בן אלישיב וילך שם לחם לא אכל ומים לא שתה--כי מתאבל על מעל הגולה
7 Ndipo lilipotolewa tangazo Yuda yote na Yerusalemu kwa watu wote waliokuwa uhamishoni kukusanyika Yerusalemu.
ויעבירו קול ביהודה וירושלם לכל בני הגולה--להקבץ ירושלם
8 Yeyote ambaye hangejitokeza kwa muda wa siku tatu angepoteza mali yake yote, kulingana na uamuzi wa maafisa na wazee, naye mtu huyo angefukuzwa kutoka kusanyiko la watu waliokuwa uhamishoni.
וכל אשר לא יבוא לשלשת הימים כעצת השרים והזקנים--יחרם כל רכושו והוא יבדל מקהל הגולה
9 Katika muda wa siku tatu, watu wote wa Yuda na Benyamini wakawa wamekusanyika huko Yerusalemu. Kwenye siku ya ishirini ya mwezi wa tisa, watu wote walikuwa wameketi ndani ya uwanja mbele ya nyumba ya Mungu, wakiwa na majonzi mno kwa tukio hilo na kwa sababu ya mvua kubwa.
ויקבצו כל אנשי יהודה ובנימן ירושלם לשלשת הימים הוא חדש התשיעי--בעשרים בחדש וישבו כל העם ברחוב בית האלהים מרעידים על הדבר ומהגשמים
10 Ndipo Kuhani Ezra aliposimama akawaambia, “Mmekosa uaminifu, mmeoa wanawake wa kigeni, mkaongezea hatia ya Israeli.
ויקם עזרא הכהן ויאמר אלהם אתם מעלתם ותשיבו נשים נכריות--להוסיף על אשמת ישראל
11 Sasa tubuni kwa Bwana, Mungu wa baba zenu mkafanye mapenzi yake. Jitengeni na mataifa wanaowazunguka na wake zenu wa kigeni.”
ועתה תנו תודה ליהוה אלהי אבתיכם--ועשו רצונו והבדלו מעמי הארץ ומן הנשים הנכריות
12 Kusanyiko lote likajibu kwa sauti kubwa: “Uko sawa kabisa! Ni lazima tufanye kama unavyosema.
ויענו כל הקהל ויאמרו קול גדול כן כדבריך (כדברך) עלינו לעשות
13 Lakini hapa pana watu wengi na ni wakati wa mvua, hivyo hatuwezi kusimama nje. Hata hivyo, shauri hili haliwezi kumalizika kwa siku moja au mbili, kwa sababu tumefanya dhambi kubwa katika jambo hili.
אבל העם רב והעת גשמים ואין כח לעמוד בחוץ והמלאכה לא ליום אחד ולא לשנים--כי הרבינו לפשע בדבר הזה
14 Maafisa wetu na wafanye kwa niaba ya kusanyiko lote. Kisha kila mmoja katika miji yetu ambaye ameoa mwanamke wa kigeni aje kwa wakati uliopangwa, akiwa pamoja na wazee na waamuzi wa kila mji, hadi hasira kali ya Mungu wetu katika shauri hili itakapoondolewa kwetu.”
יעמדו נא שרינו לכל הקהל וכל אשר בערינו ההשיב נשים נכריות יבא לעתים מזמנים ועמהם זקני עיר ועיר ושפטיה עד להשיב חרון אף אלהינו ממנו--עד לדבר הזה
15 Yonathani mwana wa Asaheli na Yazeya mwana wa Tikwa peke yao, wakiungwa mkono na Meshulamu na Shabethai Mlawi, ndio waliopinga jambo hili.
אך יונתן בן עשהאל ויחזיה בן תקוה עמדו על זאת ומשלם ושבתי הלוי עזרם
16 Basi watu wa uhamishoni wakafanya kama ilivyokuwa imependekezwa. Kuhani Ezra akachagua wanaume waliokuwa viongozi wa jamaa, mmoja kutoka kila mgawanyo wa jamaa, nao wote wakachaguliwa kwa majina. Katika siku ya kwanza ya mwezi wa kumi waliketi kuchunguza mashauri hayo.
ויעשו כן בני הגולה ויבדלו עזרא הכהן אנשים ראשי האבות לבית אבתם וכלם בשמות וישבו ביום אחד לחדש העשירי לדריוש הדבר
17 Katika siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza wakawa wamemaliza kushughulikia wanaume wote waliokuwa wameoa wanawake wa kigeni.
ויכלו בכל--אנשים ההשיבו נשים נכריות עד יום אחד לחדש הראשון
18 Miongoni mwa wazao wa makuhani, wafuatao walikuwa wameoa wanawake wa kigeni: Kutoka wazao wa Yeshua mwana wa Yosadaki na ndugu zake: Maaseya, Eliezeri, Yaribu na Gedalia.
וימצא מבני הכהנים אשר השיבו נשים נכריות מבני ישוע בן יוצדק ואחיו--מעשיה ואליעזר ויריב וגדליה
19 (Wote walitoa nadhiri kwa kuandika kwa mikono yao kuwafukuza wake zao, kwa hatia yao, kila mmoja akatoa kondoo dume kutoka kundini mwake kama sadaka ya hatia.)
ויתנו ידם להוציא נשיהם ואשמים איל צאן על אשמתם
20 Kutoka wazao wa Imeri: Hanani na Zebadia.
ומבני אמר חנני וזבדיה
21 Kutoka wazao wa Harimu: Maaseya, Eliya, Shemaya, Yehieli na Uzia.
ומבני חרם--מעשיה ואליה ושמעיה ויחיאל ועזיה
22 Kutoka wazao wa Pashuri: Elioenai, Maaseya, Ishmaeli, Nethaneli, Yozabadi na Elasa.
ומבני פשחור--אליועיני מעשיה ישמעאל נתנאל יוזבד ואלעשה
23 Miongoni mwa Walawi: Yozabadi, Shimei, Kelaya (ndiye Kelita), Pethahia, Yuda na Eliezeri.
ומן הלוים--יוזבד ושמעי וקליה הוא קליטא פתחיה יהודה ואליעזר
24 Kutoka waimbaji: Eliashibu. Kutoka mabawabu: Shalumu, Telemu na Uri.
ומן המשררים אלישיב ומן השערים שלם וטלם ואורי
25 Miongoni mwa Waisraeli wengine: Kutoka wazao wa Paroshi: Ramia, Izia, Malkiya, Miyamini, Eleazari, Malkiya na Benaya.
ומישראל--מבני פרעש רמיה ויזיה ומלכיה ומימן ואלעזר ומלכיה ובניה
26 Kutoka wazao wa Elamu: Matania, Zekaria, Yehieli, Abdi, Yeremothi na Eliya.
ומבני עילם--מתניה זכריה ויחיאל ועבדי וירימות ואליה
27 Kutoka wazao wa Zatu: Elioenai, Eliashibu, Matania, Yeremothi, Zabadi na Aziza.
ומבני זתוא--אליועני אלישיב מתניה וירמות וזבד ועזיזא
28 Kutoka uzao wa Bebai: Yehohanani, Hanania, Zabai na Athlai.
ומבני בבי--יהוחנן חנניה זבי עתלי
29 Kutoka wazao wa Bani: Meshulamu, Maluki, Adaya, Yashubu, Sheali na Yeremothi.
ומבני בני--משלם מלוך ועדיה ישוב ושאל ירמות (ורמות)
30 Kutoka wazao wa Pahath-Moabu: Adna, Kelali, Benaya, Maaseya, Matania, Bezaleli, Binui na Manase.
ומבני פחת מואב עדנא וכלל בניה מעשיה מתניה בצלאל ובנוי ומנשה
31 Kutoka wazao wa Harimu: Eliezeri, Ishiya, Malkiya, Shemaya, Shimeoni,
ובני חרם--אליעזר ישיה מלכיה שמעיה שמעון
32 Benyamini, Maluki, na Shemaria.
בנימן מלוך שמריה
33 Kutoka wazao wa Hashumu: Matenai, Matata, Zabadi, Elifeleti, Yeremai, Manase na Shimei.
מבני חשם--מתני מתתה זבד אליפלט ירמי מנשה שמעי
34 Kutoka wazao wa Bani: Maadai, Amramu, Ueli,
מבני בני מעדי עמרם ואואל
35 Benaya, Bedeya, Keluhi,
בניה בדיה כלוהי (כלוהו)
36 Vania, Meremothi, Eliashibu,
וניה מרמות אלישיב
37 Matania, Matenai na Yaasu.
מתניה מתני ויעשו (ויעשי)
38 Kutoka wazao wa Binui: Shimei,
ובני ובנוי שמעי
39 Shelemia, Nathani, Adaya,
ושלמיה ונתן ועדיה
40 Maknadebai, Shashai, Sharai,
מכנדבי ששי שרי
41 Azareli, Shelemia, Shemaria,
עזראל ושלמיהו שמריה
42 Shalumu, Amaria na Yosefu.
שלום אמריה יוסף
43 Kutoka wazao wa Nebo: Yeieli, Matithia, Zabadi, Zebina, Yadai, Yoeli na Benaya.
מבני נבו--יעיאל מתתיה זבד זבינא ידו (ידי) ויואל בניה
44 Hawa wote walikuwa wameoa wanawake wa kigeni, na baadhi yao walikuwa wamezaa nao watoto.
כל אלה נשאי (נשאו) נשים נכריות ויש מהם נשים וישימו בנים

< Ezra 10 >