< Ezekieli 8 >
1 Katika siku ya tano ya mwezi wa sita mwaka wa sita, baada ya kupelekwa uhamishoni nilipokuwa nimeketi katika nyumba yangu na wazee wa Yuda walikuwa wameketi mbele yangu, mkono wa Bwana Mwenyezi ulikuja juu yangu.
Hivyo ikawa kuhusu katika mwaka wa sita na mwezi wa sita, katika siku ya tano ya mwezi, nilipokuwa nimeketi kwenye nyumba yangu na wazee wa Yuda waliketi mbele yangu, kwamba mkono wa Bwana Yahwe ukanijaza juu yangu huko.
2 Nikatazama, nikaona umbo mfano wa mwanadamu. Kutokana na kile kilichoonekana kuwa kiuno chake kuelekea chini alifanana na moto. Kuanzia kwenye kiuno kuelekea juu sura yake kama chuma kingʼaavyo kikiwa ndani ya moto.
Hivyo nikaona, na tazama, kulikuwa na mfano kama mwonekano wa mwanadamu. Kutoka kwenye mwonekano wake wa nyonga kwenda chini kulikuwa na moto. Na kutoka kwenye nyonga kwenda juu kulikuwa na mwonekano wa kitu kinachong'aa, kama mng'ao wa chuma.
3 Akanyoosha kitu kilichoonekana kama mkono, akaniinua kwa kushika nywele za kichwa changu. Roho akaniinua juu kati ya nchi na mbingu nikiwa katika maono ya Mungu akanichukua mpaka Yerusalemu, kwenye ingilio la lango la upande wa kaskazini ya ukumbi wa ndani, mahali iliposimama ile sanamu ichocheayo wivu.
Kisha akanyoosha kutoka kwenye mkono na kunichukua kwa nywele za kichwa changu; Roho akaniacha juu kati ya dunia na mbingu, na katika maono kutoka kwa Mungu, akaniletea hata Yerusalemu, kwenye mlango wa kuingia ndani ya lango la kaskazini, ambako sanamu ile iletayo wivu mkubwa ilipokuwa imesiamama.
4 Hapo mbele yangu palikuwa na utukufu wa Mungu wa Israeli, kama utukufu ule niliouona katika maono kule ua wa ndani.
Kisha tazama, utukufu wa Mungu wa Israeli ulikuwa huko, kulingana na ono nililokuwa nimeliona kwenye uwanda.
5 Kisha akaniambia, “Mwanadamu, tazama kuelekea kaskazini.” Hivyo nikatazama na kwenye ingilio upande wa kaskazini wa lango la madhabahu, nikaona sanamu hii ya wivu.
Kisha akanambia, “Mwanadamu, inua juu macho yako kwenda upande wa kaskazini.” Hivyo nikainua macho yangu kuelekea kaskazini, na kwenye lango la kaskazini kulekea kwenye madhabahu, huko kwenye lango la kuingilia, kulikuwa na sanamu ya wivu.
6 Ndipo akaniambia, “Mwanadamu, je, unaona yale wanayofanya, haya mambo ya machukizo kabisa nyumba ya Israeli wanayotenda hapa, ambayo yatanifanya niende mbali na mahali pangu patakatifu? Lakini utaona vitu ambavyo vinachukiza zaidi hata kuliko hivi.”
Hivyo akanambia, “Mwanadamu, unaona wanayoyafanya? Haya ni machukizo makubwa ambayo nyumba ya Israeli wanayoyafanya hapa kunifanya niende mbali kutoka patakatifu pangu. Lakini utageuka na kuona machukizo makubwa zaidi.”
7 Kisha akanileta mpaka ingilio la ukumbi. Nikatazama, nami nikaona tundu ukutani.
Kisha akanileta hata kwenye mlango wa uzio, na nikatazama, kulikuwa na shimo kwenye ukuta.”
8 Akaniambia, “Mwanadamu, sasa toboa kwenye ukuta huu.” Ndipo nikatoboa ule ukuta, nikaona hapo pana mlango.
Akanambia, “Mwanadamu, chimba kwenye huu ukuta.” Basi nikachimba kwenye huo ukuta, na kulikuwa na mlango.
9 Naye akaniambia, “Ingia ndani, ukaone maovu na machukizo wanayofanya humu.”
Kisha akanambia, “Nenda na ukaone machukizo ya uovu ambayo wanayoyafanya hapa.”
10 Hivyo nikaingia ndani na kutazama, nikaona kuta zote zimechorwa kila aina ya vitu vitambaavyo na ya wanyama wachukizao wa kila aina na sanamu zote za nyumba ya Israeli.
Basi nilipokuwa nikienda ndani na nikaona, na tazama! Kulikuwa na kila umbo la vitu vikitembea polepole na mnyama achukizaye sana! Kila sanamu wa nyumba ya Israeli ilikuwa imechongwa kwenye ukuta pande zote.
11 Mbele yao walisimama wazee sabini wa nyumba ya Israeli, naye Yaazania mwana wa Shafani alikuwa amesimama miongoni mwao. Kila mmoja alikuwa na chetezo mkononi na moshi wa harufu nzuri ya uvumba ulikuwa unapanda juu.
Wazee sabini wa wa nyumba ya Israeli walikuwa huko, na Yaazania mwana wa Shafani alikuwa amesimama katikati yao. Walikuwa wamesimama mbele ya picha, na kila mtu alikuwa na chetezo kwenye mkono wake ili kwamba harufu ya ubani ingeweza kupanda juu.
12 Akaniambia, “Mwanadamu, umeona wanayoyafanya wazee wa nyumba ya Israeli gizani, kila mmoja kwenye sehemu yake mwenyewe ya kufanyia ibada za sanamu yake? Wao husema, ‘Bwana hatuoni, Bwana ameiacha nchi.’”
Akanambia, “mwanadamu, unaona kile ambacho wazee wa nyumba ya Israeli wanachokifanya kwenye giza? Kila mmoja hufanya hivi kwenye chumba cha sanamu yake, kwa kuwa husema, 'Yahwe hatuone! Yahwe ameitelekeza hii nchi.”'
13 Akasema tena, “Bado utaona machukizo wanayofanya ambayo ni makubwa kuliko haya.”
Kisha akanambia, “Geuka tena na tazama machukizo makubwa ambayo wanayoyafanya.”
14 Ndipo akanileta mpaka ingilio la lango la kaskazini la nyumba ya Bwana, nami nikaona wanawake wameketi hapo, wakimwombolezea Tamuzi.
Tena akanileta kwenye lango la kuingia la nyumba ya Yahwe lililokuwa upande waa kaskazini, na tazama! Wanawake walikuwa wameketi huko wakimlilia Tamuzi.
15 Akaniambia, “Unaliona hili, mwanadamu? Utaona vitu ambavyo ni machukizo kuliko hili.”
Hivyo akanambia, “Umeiona hii, mwanadamu? Geuka tena na uone machukizo makubwana zaidi kuliko hayo.”
16 Ndipo akanileta mpaka kwenye ukumbi wa ndani wa nyumba ya Bwana, nako huko katika ingilio la Hekalu, kati ya baraza na madhabahu, walikuwepo wanaume wapatao ishirini na watano. Wakiwa wamelipa kisogo Hekalu la Bwana na kuelekeza nyuso zao upande wa mashariki, wakilisujudia jua huko mashariki.
Akanileta hata kwenye uzio wa ndani wa nyumba ya Yahwe, na tazama! huko kwenye lango la kuingia kwenye madhabahu, kulikuwa na takribani watu ishirini na tano waliokuwa wamelipa mgongo hekalu la Yahwe na nyuso zao kuelekea mashariki, na walikuwa wakiabudu jua.
17 Akaniambia, “Je, umeona hili mwanadamu? Je, ni jambo dogo sana kwa nyumba ya Yuda kufanya machukizo wanayoyafanya hapa? Je, ni lazima pia waijaze nchi dhuluma na kuendelea siku zote kunikasirisha? Watazame wanavyonibania pua kana kwamba ninanuka!
Akanambia, “Unaona hii, mwanadamu? Je ni kitu kidigo kwa ajili ya nyumba ya Yuda kufanya haya machukizo wanayoyafanya? Kwa kuwa wameijaza nchi kwa uovu na wamerudi tena ili kuniletea hasira, kuweka tawi kwenye pua zao.
18 Kwa hiyo nitashughulika nao kwa hasira, sitawaonea huruma wala kuwaachilia. Wajapopiga makelele masikioni mwangu, sitawasikiliza.”
Hivyo nitatenda miongoni mwao pia; jicho langu halitakuwa na huruma, sitaacha kuwaharibu. hata watalia kwenye masikio yangu kwa sauti kubwa, sitawasikia.”