< Ezekieli 6 >

1 Neno la Bwana likanijia kusema,
Neno la Yahwe likanijia, likisema,
2 “Mwanadamu, elekeza uso wako kukabili milima ya Israeli, utabiri dhidi yake
“Mwana wa adamu, weka uso wako dhidi ya milima ya Israeli na uwatabirie.
3 na useme: ‘Ee milima ya Israeli, sikia neno la Bwana Mwenyezi. Hili ndilo Bwana Mwenyezi aliambiayo milima na vilima, magenge na mabonde: Ninakaribia kuleta upanga dhidi yenu, nami nitapaharibu mahali penu pote pa juu pa kuabudia miungu.
Sema, 'Milima ya Israeli, silikilizeni neno la Bwana Yahwe! Bwana Yahwe asema hivi kwenye milima kwenye vilele, kwenye vijito na kwenye mabonde: Tazama! Naleta upanga dhidi yenu, na nitapaharibu pahali penu pa juu.
4 Madhabahu yenu yatabomolewa na madhabahu yenu ya kufukizia uvumba yatavunjavunjwa, nami nitawachinja watu wenu mbele ya sanamu zenu.
Kisha madhabahu zenu zitakuwa ukiwa na nguzo zenu zitaharibiwa, na nitatupa chini wafu wenu mbele ya sanamu zao.
5 Nitazilaza maiti za Waisraeli mbele ya sanamu zao, nami nitatawanya mifupa yenu kuzunguka madhabahu yenu.
Nitalaza miili iliyokufa kwa watu wa Israeli mbele ya sanamu zao, na kuitawanya mifupa yenu kuzizunguka madhabahu zenu.
6 Popote mnapoishi, miji hiyo itafanywa ukiwa na mahali pa juu pa kuabudia miungu patabomolewa, ili madhabahu yenu ifanywe ukiwa na kuharibiwa, sanamu zenu zitavunjavunjwa na kuharibiwa, madhabahu yenu ya kufukizia uvumba yatabomolewa na kila mlichokifanya kitakatiliwa mbali.
Kila mahali utaishi, miji itaharibiwa na mahali pa juu kuangamia, hivyo basi madhabahu zenu zitaharibiwa na kufanywa ukiwa. Kisha zitavunjwa na kupotea, nguzo zenu zitaangushwa chini na kazi zenu zitafutwa mbali.
7 Watu wenu watachinjwa katikati yenu, nanyi mtatambua Mimi ndimi Bwana.
Waliokufa wataanguka chini kati yenu nanyi mtajua kwamba mimi ni Yahwe.
8 “‘Lakini nitawabakiza hai baadhi yenu, kwa kuwa baadhi yenu watanusurika kuuawa watakapokuwa wametawanyika katika nchi na mataifa.
Lakini nitahifadhi mabaki kwenu, na kutakuwa na wale watakao toroka upanga miongoni mwa mataifa,
9 Ndipo katika mataifa ambamo watakuwa wamechukuliwa mateka, wale ambao watanusurika watanikumbuka, jinsi ambavyo nimehuzunishwa na mioyo yao ya uzinzi, ambayo imegeukia mbali nami na macho yao ambayo yametamani sanamu zao. Watajichukia wenyewe kwa ajili ya uovu walioutenda na kwa ajili ya desturi zao za kuchukiza.
Kisha wale watakao toroka watanikumbuka miongoni mwa mataifa amabapo watakapochukuliwa mateka, ndivyo nitakavoyowaponda mioyo yao ya kikahaba ambayo imeniacha, na kwa macho yao ya kikahaba kufuata sanamu zao. Kisha wataonyesha chuki kwenye nyuso zao kwa udhaifu walioufanya kwa machukizo yao yote.
10 Nao watajua kuwa Mimi ndimi Bwana, sikuwaonya bure kuwa nitaleta maafa hayo yote juu yao.
Hivyo watajua kwamba mimi ni Yahwe. Kulikuwa na sababu kwamba nimesema nitaleta huu uovu kwao.
11 “‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Piga makofi, kanyaga chini kwa mguu na upige kelele, “Ole!” kwa sababu ya maovu yote na machukizo yote yanayofanywa na nyumba ya Israeli, kwa kuwa wataanguka kwa upanga, njaa na tauni.
Bwana Yahwe asema hivi: Piga makofi na kanyaga kwa mguu wako! Sema! 'Ole!' kwa sababu ya uovu wote wa chukizo wa nyumba ya Israeli! Wataanguka kwa upanga, njaa, na tauni.
12 Yeye aliye mbali sana atakufa kwa tauni, naye aliye karibu atauawa kwa upanga, naye yule atakayenusurika na kubaki atakufa kwa njaa. Hivyo ndivyo nitakavyotimiza ghadhabu yangu dhidi yao.
Yule aliye mbali sana atakufa kwa tauni, na yule aliyekaribu ataanguka kwa upanga. Wale watakaobaki na kuishi watakufa kwa upanga. Kwa njia hii ndivyo nitakavyo kamilisha madhabahu yangu dhidi yao.
13 Nao watajua kwamba Mimi ndimi Bwana, wakati maiti za watu wao zitakapokuwa zimelala katikati ya sanamu zao kuzunguka madhabahu yao, juu ya kila kilima kilichoinuka na juu ya vilele vyote vya milima, chini ya kila mti uliotanda na kila mwaloni wenye majani, yaani, sehemu walizofukizia uvumba kwa sanamu zao zote.
Kisha mtajua kwamba mimi ni Yahwe, wakati waliokufa watakapolala kati ya sanamu zao, kuzizunguka madhabahu, kwa kila mlima mrefu-juu ya vilele vya mlima, na chini ya mti wenye majani mabichi na mwalo mnene-sehemu wanapochomea ubani kwa sanamu zao zote.
14 Nami nitanyoosha mkono wangu dhidi yao na kuifanya nchi yao ukiwa, kuanzia jangwani hadi Dibla, kila mahali wanapoishi. Ndipo watakapojua ya kwamba Mimi ndimi Bwana.’”
Nitapiga kwa mkono wangu na kuifanya nchi ukiwa na isiyofaa, kutoka jangwa hata Dibla, kupita sehemu zote wanapoishi. Kisha watajua kwamba mimi ni Yahwe.”

< Ezekieli 6 >