< Ezekieli 46 >
1 “‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Lango la ukumbi wa ndani linaloelekea upande wa mashariki litakuwa linafungwa kwa siku sita za juma, ila siku ya Sabato na siku ya Mwezi Mwandamo litafunguliwa.
Bwana Yahwe asema hivi: Lango la uzio wa ndani, linaloelekea mashariki, litafungwa kwa mda wa siku sita za kazi, lakini katika siku za Sabato litakuwa wazi, na katika siku ya mwezi mpya litafunguliwa.
2 Mkuu anayetawala ataingia kupitia baraza ya njia ya lango la ukumbi na kusimama karibu na nguzo ya lango. Makuhani watatoa sadaka za mkuu anayetawala za kuteketezwa na sadaka za amani. Mkuu anayetawala atasujudu kwenye kizingiti cha njia ya lango, kisha atatoka nje, lakini lango halitafungwa mpaka jioni.
Mwana wa mfalme ataingia kwa kutumia lango la njia ya nyuma ya varanda upande wa nje, na atasimama mbele ya muhimili wa mwimo wa lango la ndani wakati makuhani wakiwa wakitengeza sadaka ya kuteketezwa na sadaka ya amani. Kisha ataabudu kwenye kizingiti cha lango la ndani na kutoka nje, lakini lango halitakuwa linafungwa hadi jioni.
3 Siku za Sabato na za Mwezi mwandamo watu wote wa nchi wataabudu mbele za Bwana penye lile ingilio la ile njia.
Watu wa nchi pia wataabudu mbele ya Yahwe kwenye hili lango la kuingilia katika siku ya Sabato na siku mpya za mwezi.
4 Sadaka ya kuteketezwa aletazo mkuu anayetawala kwa Bwana siku ya Sabato itakuwa ni wana-kondoo sita na kondoo dume mmoja, wote wasiwe na dosari.
Sadaka ya kuteketezwa ambayo mwana wa mfalme aitoayo kwa Yahwe katika siku ya Sabato itakuwa wanakondoo sita wasiokuwa na dosari na kondoo dume asiyekuwa na dosari.
5 Sadaka ya nafaka inayotolewa pamoja na huyo kondoo dume itakuwa efa moja na sadaka ya nafaka inayotolewa na hao wana-kondoo itakuwa kiasi apendacho mtu pamoja na hini ya mafuta kwa kila efa.
Sadaka ya unga pamoja na kondoo dume itakuwa efa moja, na sadaka ya unga pamoja na wanakondoo kiasi awezacho kutoa, na hini moja ya mafuta pamoja na kila efa ya unga.
6 Siku ya mwezi mwandamo atatoa fahali mchanga, wana-kondoo sita na kondoo dume, wote wasiwe na dosari.
Katika siku ya mwezi mpya atatoa ng'ombe mchanga asiyekuwa na dosari kutoka kuchungwa, wanakondoo sita, na kondoo asyekuwa na dosari.
7 Atatoa kuwa sadaka ya nafaka efa moja pamoja na fahali mmoja, efa moja na kondoo dume mmoja na pamoja na wana-kondoo kama atakavyo kutoa, pamoja na hini ya mafuta kwa kila efa.
Atatengeneza sadaka ya unga ya efa moja kwa ajili ya ng'ombe na efa moja kwa ajili ya kondoo, na kwa kiasi awezacho kukitoa kwa ajili ya wanakondoo, na hini ya mafuta kwa kila efa ya unga.
8 Wakati mkuu anayetawala aingiapo, atapitia kwenye baraza ya njia ya lango, naye atatoka nje kwa njia hiyo hiyo.
Wakati mwana wa mfalme atakapokuwa anaingia kwa njia ya lango lenye varanda, ataondoka kwa njia hiyo hiyo.
9 “‘Wakati watu wa nchi wanapokuja mbele za Bwana katika sikukuu zilizoamriwa, yeyote aingiaye kwa lango la kaskazini kuabudu atatoka nje kwa lango la kusini na yeyote aingiaye kwa lango la kusini atatoka nje kwa lango la kaskazini. Hakuna mtu yeyote atakayerudi kwa kupitia lango lile aliloingilia, lakini kila mmoja atatoka nje kwa lango linalokabili lile aliloingilia.
Lakini wakati watu wa nchi watakakuja kwa Yahwe katika sikukuu zilizoteuliwa, kila mmoja kuingia kupitia kwenye lango la kaskazini kuabudu ataondoka kupitia lango la kusini; na kila atakayeingillia kupitia lango la kusini atatoka kupitia lango la kaskazini. Hakuna atakayerudia kwa lile lango aliloingilia, kwa kuwa atatoka nje moja kwa moja.
10 Mkuu anayetawala atakuwa miongoni mwao, akiingia nao ndani wanapoingia, naye atatoka nao nje wanapotoka.
Mwana wa mfalme atakuwa kati yao; watakapoingia, ataingia ndani, na watakapoondoka, atatoka nao.
11 “‘Kwenye sikukuu na kwenye sikukuu zilizoamriwa, sadaka ya nafaka itakuwa efa moja pamoja na fahali mmoja, efa moja pamoja na kondoo dume mmoja, pamoja na idadi ya wana-kondoo kama mtu apendavyo kutoa, pamoja na hini ya mafuta kwa kila efa.
Kwenye sikukuu hizo, sadaka ya unga itakuwa efa moja ya unga kwa ng'ombe mmoja na efa moja kwa kondoo dume, na chochote atakacho kitoa pamoja na wanakondoo, na hini moja ya mafuta kwa kila efa.
12 Mkuu anayetawala anapotoa sadaka ya hiari kwa Bwana, ikiwa ni sadaka ya kuteketezwa au sadaka ya amani, lango linaloelekea mashariki litafunguliwa kwa ajili yake. Atatoa sadaka yake ya kuteketezwa au sadaka yake ya amani kama afanyavyo katika siku ya Sabato. Kisha atatoka nje, naye akiisha kutoka nje, lango litafungwa.
Wakati mwana wa mfalme atakapotoa sadaka atakayojisikia kutoa, labda sadaka ya kuteketezwa au sadaka ya amani kwa Yahwe, lango la kuelekea mashariki litafunguliwa kwa ajili yake. Atatoa sadaka yake ya kuteketezwa au sadaka ya amani kama afanyavyo siku ya Sabato. Kisha atatoka nje, na baada ya kutoka lango litafungwa.
13 “‘Kila siku utamtoa mwana-kondoo wa mwaka mmoja asiyekuwa na dosari kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa kwa Bwana, utaitoa kila siku asubuhi.
Kwa kuongeza, utatoa mwanakondoo asiyekuwa na dosari mwenye umri wa mwaka mmoja kama sadaka ya kuteketezwa kwa Yahwe kila siku; utafanya hivi kila asubuhi.
14 Pia kila siku asubuhi pamoja na hiyo sadaka utatoa sadaka ya nafaka, ikiwa na sehemu ya sita ya efa pamoja na theluthi moja ya hini ya mafuta ya kuchanganya na ule unga. Utoaji wa sadaka hii ya nafaka kwa Bwana ni amri ya daima.
Utatoa sadaka ya unga pamoja nayo kila asubuhi, efa sita na sehemu ya tatu ya hini ya mafuta kuchanganya na sadaka ya unga kwa ajili ya Yahwe, kulingana na sheria ilivyo.
15 Kwa hiyo mwana-kondoo na sadaka ya nafaka na mafuta vitatolewa kila siku asubuhi kwa ajili ya sadaka ya daima ya kuteketezwa.
Watandaa mwanakondoo, sadaka ya kuteketezwa, na mafuta kila asubuhi, sadaka ya kuteketezwa ya kudumu.
16 “‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Ikiwa mkuu atawalaye atatoa zawadi kutoka kwenye urithi wake na kumpa mmoja wa wanawe, hiyo zawadi itakuwa pia kwa wazao wake, itakuwa mali yao kwa urithi.
Bwana Yahwe asema hivi: Kama mwana wa mfalme akitoa zawadi kwa mmoja wa watoto wake, imekuwa urithi wake. Itakuwa mali ya mtoto wake, imekuwa urithi.
17 Hata hivyo, kama atatoa zawadi kutoka urithi wake na kumpa mmoja wa watumishi wake, mtumishi anaweza kuiweka mpaka mwaka wa uhuru, kisha itarudishwa kwa mkuu anayetawala. Urithi wake ni wa wanawe peke yao, ni mali yao.
Lakini kama akimpatia zawadi kutoka urithi wake kwa mmoja wa watumishi wake, kisha itakuwa ya huyo mtumishi mpaka mwaka wa uhuru, na kisha itarudi kwa mwana wa mfalme. Urithi wake yamkini ukawa kwa ajili ya watoto wake.
18 Mkuu anayetawala hana ruhusa kuchukua urithi wowote wa watu na kuwaondoa kwenye mali zao. Mkuu atawalaye atawapa wanawe urithi wao, kutoka kwenye mali zake mwenyewe, ili kwamba pasiwe na mtu wangu yeyote atakayetengwa na urithi wake.’”
Mwana wa mfalme hatawaondolea urithi wa watu kutoka kwenye mali zao wenyewe; ataandaa kwa ajili ya watoto wake mali ili kwamba watu wangu wasitawanyike, kila mtu kutoka mali kwenye yake mwenyewe.”
19 Kisha mtu yule akanileta kwa kupitia kwenye ingilio lililokuwa kando ya lango mpaka kwenye vyumba vitakatifu vinavyoelekea kaskazini, ambavyo ni vya makuhani, naye akanionyesha mahali fulani upande wa mwisho wa magharibi.
Kisha yule mtu akaniletea kwenye lango la kutokea hata kwenye vyumba vitakatifu kwa ajili ya makuhani, vilivyokuwa vimeelekea kaskazini na tazama! Kulikuwa na sehemu mbele magharibi.
20 Akaniambia, “Mahali hapa ndipo makuhani watakapotokosea sadaka ya hatia na sadaka ya dhambi na kuoka sadaka ya nafaka, kuepuka kuzileta katika ukumbi wa nje na kushirikisha utakatifu kwa watu.”
Akanambia, “Hii ndio sehemu ambayo makuhani watakapo chemshia sadaka ya hatia na sadaka ya dhambi na walipookea sadaka ya unga. Wasilete sadaka nje ya uzio, kwa kuwa watu watatakaswa.”
21 Baada ya hapo akanileta kwenye ukumbi wa nje na kunizungusha kwenye pembe zake nne, nami nikaona katika kila pembe ya huo ukumbi kulikuwa na ukumbi mwingine.
Kisha akanileta kwenye uzio wa nje akaniongoza kuzunguka pembe nne za uzio, nikaona kwamba katika kila pembe ya uzio kulikuwa na uwanja.
22 Katika pembe nne za huo ukumbi wa nje kulikuwa na kumbi nyingine, zenye urefu wa dhiraa arobaini na upana wake dhiraa thelathini, ambapo hizo kumbi kwenye hizo pembe nne zilikuwa na vipimo vilivyo sawa.
Katika hizo pembe nne za nje ya uzio kulikuwa na nzio nne ndogo, dhiraa arobaini urefu na thelathini upana. Ukubwa ule ule kwa nzio zote nne.
23 Mzunguko wa ndani wa hizo kumbi nne ulikuwa na ukingo wa jiwe, zikiwa na sehemu zilizojengwa kwa ajili ya moto kuzunguka chini ya huo ukingo.
Kulikuwa na safu zilizokuwa zimetengenezwa kwa mawe kuzizunguka zote nne, na meko ya kupikia ilikuwa chini ya safu ya jiwe.
24 Akaniambia, “Hizi ndizo sehemu za kupikia ambazo wale wanaohudumu kwenye Hekalu watatokosea dhabihu za watu.”
Yule mtu akanambia, “Hizi ndizo sehemu ambazo watumishi watachemshia dhabihu za watu.”