< Ezekieli 44 >
1 Ndipo yule mtu akanirudisha mpaka kwenye lango la nje la mahali Patakatifu, lile linaloelekea upande wa mashariki, nalo lilikuwa limefungwa.
Kisha yule mtu akanirudisha hata lango la nje la patakatifu linaloelekea mashariki; lilikuwa limefungwa kwa kukazwa.
2 Bwana akaniambia, “Lango hili litabaki limefungwa. Haliruhusiwi kufunguliwa, wala hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kuingilia kwenye lango hili. Litabaki limefungwa kwa sababu Bwana, Mungu wa Israeli, ameingia kwa kupitia lango hili.
Yahwe akanambia, “Hili lango litakuwa limefungwa; halitafunguliwa. Hakuna mtu atakaye pitia hapo, kwa kuwa Yahwe, Mungu wa Israeli ameingia kwa hilo, hivyo lilikuwa limefungwa kwa kukazwa.
3 Yeye aliye mkuu peke yake ndiye anayeweza kukaa penye njia ya hilo lango na kula chakula mbele za Bwana. Itampasa aingie kwa njia hiyo ya lango la ukumbini na kutokea njia iyo hiyo.”
Mtawala wa Israeli atakaa katika hilo kula chakula mbele ya Yahwe. Ataingia kwa njia ya varanda na kutoka kwa njia hiyo hiyo.”
4 Kisha yule mtu akanileta kwa njia ya lango la kaskazini mpaka mbele ya Hekalu. Nikatazama nami nikauona utukufu wa Bwana ukilijaza Hekalu la Bwana, nami nikaanguka kifudifudi.
Kisha akaniletea kwa njia ya lango la kaskazini linaloelekea kwenye nyumba. Hivyo nikaona na kutazama, utukufu wa Yahwe umejaa kwenye nyumba ya Yahwe, nikaanguka kifudifudi.
5 Bwana akaniambia, “Mwanadamu, angalia kwa uangalifu, usikilize kwa bidii na uzingatie kila kitu ninachokuambia kuhusu masharti yote yanayohusu Hekalu la Bwana. Uwe mwangalifu kuhusu wale wanaoruhusiwa hekaluni na wale wasioruhusiwa kuingia mahali patakatifu.
Kisha Yahwe akanambia, “Mwanadamu, andaa moyo wako na tazama kwa macho yako na sikiliza kwa masikio yako kwa yote yale nikuambiayo, kwa amri zote za nyumba ya Yahwe na maagizo yote. Fikiri kuhusu malango ya nyumba na na matokeo ya malango.
6 Iambie nyumba ya kuasi ya Israeli, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Matendo yenu ya machukizo yatosha, ee nyumba ya Israeli!
Kisha waambie wale walioasi, nyumba ya Israeli, 'Bwana Yahwe asema hivi: Acheni matendo yenu maovu kwenu, nyumba ya Israeli-
7 Zaidi ya matendo yenu yote ya machukizo, mmewaleta wageni wasiotahiriwa mioyo na miili katika patakatifu pangu, mkilinajisi Hekalu langu, huku mkinitolea chakula, mafuta ya wanyama na damu, nanyi mmevunja Agano langu.
ambayo mmewaleta wageni pamoja na wasiotahiriwa mioyo na wasiotahiriwa mwili kuwa katika patakatifu pangu, kuikufuru nyumba yangu, wakati mlipokuwa mnanitolea chakula, mafuta na damu-mmevunja agano langu kwa matendo yenu maovu.
8 Badala ya kutimiza wajibu wenu kuhusiana na vitu vyangu vitakatifu, mmeweka watu wengine kuwa viongozi katika patakatifu pangu.
Hamkumaliza kazi zenu zinazohusiana na vitu vitakatifu, lakini mmewateua wengine kuchukua kazi zenu, na mmewatuma kupaangalia mahali patakatifu pangu.
9 Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Hakuna mgeni asiyetahiriwa moyo na mwilini anayeruhusiwa kuingia patakatifu pangu, wala hata wageni wanaoishi miongoni mwa Waisraeli.
Bwana Yahe asema hivi: hakuna mgeni, ambaye hajatahiriwa kwenye moyo wake na mwili, kutoka yeyote wa hao waishio miongoni mwa watu wa Israeli, awezaye kuingia patakatifu pangu.
10 “‘Walawi walioniacha wakati Waisraeli walipopotoka wakatoka kwangu na kutangatanga kwa kufuata sanamu zao, watachukua adhabu ya dhambi zao.
Kisha Walawi wakaenda mbali nami-wakapotea mbali nami, kwenda kwenye sanamu zao-lakini watalipa kwa ajili ya dhambi yao.
11 Wanaweza wakatumika katika mahali patakatifu pangu, wakiwa na uangalizi wa malango ya Hekalu, nao watachinja sadaka za kuteketezwa na dhabihu kwa ajili ya watu na kusimama mbele ya watu ili kuwahudumia.
Wao ni watumishi katika patakatifu pangu, waangalizi wa malango ya nyumba na kutumika kwenye nyumba na kuchinja sadaka za kuteketezwa na dhabihu za watu, na watasimama mbele za watu na kuwatumikia.
12 Lakini kwa sababu waliwatumikia watu mbele ya sanamu zao na kuifanya nyumba ya Israeli ianguke kwenye dhambi, kwa hiyo nimeapa kwa mkono ulioinuliwa kwamba ni lazima wachukue matokeo ya dhambi yao, asema Bwana Mwenyezi.
Lakini kwa sababu wamefanya dhabihu mbele ya sanamu zao, wamekuwa kikwazo kwa dhambi ya nyumba ya Israeli. Kwa hiyo nitainua mkono wangu kuapa kiapo dhidi yao-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-watabeba adhabu yao.
13 Hawaruhusiwi kukaribia ili kunitumikia kama makuhani wala kukaribia chochote changu kilicho kitakatifu au sadaka iliyo takatifu kupita zote, bali watachukua aibu ya matendo yao ya kuchukiza.
Hawatakuja karibu nami kufanya kama makuhani au kukaribiakila vitu vyangu vitakatifu, vitu vitakatifu sana. Badala yake, watabeba lawama zao na hatia zao kwa ajili ya matendo yao ya karaha waliyoyafanya.
14 Lakini nitawaweka katika uangalizi wa Hekalu na kazi zote zile zinazotakiwa kufanyika ndani yake.
Lakini nitawaweka kama watunzaji wa kazi katika nyumba, kwa kazi zote na kila kitu kitakachofanyika ndani yake.
15 “‘Lakini makuhani, ambao ni Walawi na wazao wa Sadoki, ambao walitimiza wajibu wao kwa uaminifu katika patakatifu pangu wakati Waisraeli walipopotoka, watakaribia ili kutumika mbele zangu. Itawapasa wasimame mbele zangu ili kutoa dhabihu za mafuta ya wanyama na damu, asema Bwana Mwenyezi.
Kisha makuhani walawi, hao wana wa Zadoki ambao waliokamilisha kazi ya patakatifu pangu wakati wana wa Israeli walipotea mbali nami-watakuja karibu nami kuniambudu. Watasimama mbele yangu kunitolea mafuta na damu-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.
16 Wao peke yao ndio wenye ruhusa ya kuingia mahali patakatifu pangu. Wao peke yao ndio watakaokaribia meza yangu ili kuhudumu mbele zangu na kufanya utumishi wangu.
Watakuja hata patakatifu pangu; wataikaribia meza yangu kuniabudu na kukamilisha kazi zao kwangu.
17 “‘Watakapoingia kwenye malango ya ukumbi wa ndani, watavaa nguo za kitani safi, hawaruhusiwi kamwe kuvaa mavazi ya sufu wakati wanapokuwa wakihudumu kwenye malango ya ukumbi wa ndani wala ndani ya Hekalu.
Hivyo itakuwa kwamba watakapokuja kwenye malango ya ua wa ndani, watatakiwa kuvaa mavazi ya kitani, kwa kuwa hawatakuja na sufu ndani ya lango la ua wa ndani na nyumba yake.
18 Watavaa vilemba vya kitani safi vichwani mwao na nguo za ndani za kitani safi viunoni mwao. Hawatavaa chochote kitakachowafanya kutoa jasho.
Kutakuwa na vilemba juu ya vichwa vyao na kitani ndani ya viuno vyao. Ndani wasivae nguo ambayo itawafanya watoke jasho.
19 Watakapotoka ili kuingia katika ukumbi wa nje mahali watu walipo, watavua nguo walizokuwa wakihudumu nazo na wataziacha katika vyumba vitakatifu nao watavaa nguo nyingine, ili kwamba wasije wakaambukiza watu utakatifu kwa njia ya mavazi yao.
Wakati watakapotoka nje ya ua wa nje, hata kwenye ua wa ndani ili kwenda kwa watu, watavua nguo zao walizokuwa wamezivaa kisha wakatumika; watazivua na kuziweka chini katika chumba kitakatifu, hivyo wasiwafanye wengine watakatifu kwa kugusana na nguo zao maalumu.
20 “‘Hawatanyoa nywele za vichwa vyao wala kuziacha ziwe ndefu, bali watazipunguza.
Hawatanyoa vichwa vyao wala kuruhusu nywele zao kuwa ndefu, watapunguza nywele za vichwa vyao.
21 Kuhani yeyote asinywe mvinyo aingiapo katika ukumbi wa ndani.
Hakuna kuhani atakaye ruhusiwa kunywa mvinyo wakati atakapoingia kwenye uwa wa ndani,
22 Wasioe wanawake wajane wala walioachika, inawapasa kuoa wanawake bikira wenye heshima wa Israeli au wajane wa makuhani.
hakuna kuchukua mjane au mwanamke aliyetalikiwa kama mke kwa ajili yake, lakini mwali kutoka safu ya nyumba ya Israeli au mjane aliyekuwa ameolewa na kuhani aliyepita.
23 Watawafundisha watu wangu tofauti kati ya vitu vitakatifu na vitu vya kawaida na kuwaonyesha jinsi ya kupambanua kati ya vitu najisi na vitu safi.
Kwa kuwa watawafundisha watu wangu tofauti kati ya utakatifu na kukufuru; watawafanya kujua uchafu kutoka usafi.
24 “‘Katika magombano yoyote, makuhani watatumika kama mahakimu na kuamua hilo jambo kufuatana na sheria zangu. Watazishika sheria zangu na maagizo yangu katika sikukuu zangu zote zilizoamriwa, nao watatakasa Sabato zangu.
Katika kubishana watasimama kwenye hukumu pamoja na amri yangu; watakuwa waadilifu. Watashika sheria yangu na amri zangu katika sikukuu, na watasherekea siku yangu ya Sabato.
25 “‘Kuhani asijitie unajisi kwa kukaribia maiti, lakini, kama mtu aliyekufa alikuwa baba yake au mama yake, mwana au binti yake, ndugu yake au dada ambaye hajaolewa, basi aweza kujitia unajisi kwa hao.
Hawataenda kwa mtu aliyekufa ili wasiwe najisi, vinginevyo awe ni baba au mama yao, mwana wa kiume au binti, kaka au dada ambaye hajawahi kulala na mtu; vinginevyo, watakuwa najisi.
26 Baada ya kujitakasa, atakaa hali hiyo kwa muda wa siku saba.
Baada ya kuhani kuwa najisi, watahesabu mda wa siku saba kwa ajili yake.
27 Siku atakapoingia katika ukumbi wa ndani wa mahali patakatifu ili kuhudumu, atatoa sadaka ya dhambi kwa ajili yake mwenyewe, asema Bwana Mwenyezi.
Katika siku atakayoingia mahali patakatifu, ndani kwenye uzio kutumika katika mahali patakatifu, ataleta sadaka ya dhambi kwa ajili yake mwenyewe-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.
28 “‘Mimi nitakuwa ndio urithi pekee walio nao makuhani katika Israeli. Msiwape wao milki, mimi nitakuwa milki yao.
Hapa patakuwa urithi wao: Mimi ndiyo urithi wao, na usiwapatie mali katika Israeli; nitakuwa mali yao!
29 Wao watakula sadaka za nafaka, sadaka za dhambi na sadaka za hatia na kila kitu kitakachotolewa kwa Bwana katika Israeli kitakuwa chao.
Watakula chakula cha sadaka, sadaka za dhambi, sadaka za hatia, na kila kitakachotolewa kwa ajili ya Yahwe katika Israeli, vitakuwa vyao.
30 Yote yaliyo bora ya malimbuko ya vitu vyote na matoleo yenu maalum vitakuwa vya makuhani. Inawapasa kuwapa malimbuko ya kwanza ya unga wenu ili kwamba baraka ipate kuwa katika nyumba zenu.
Malimbuko ya kwanza ya vitu na kila sadaka, kila kitu kitokanacho na sadaka zenu vitakuwa mali ya makuhani, mtatoa sadaka ya chakula kizuri kwa makuhani ili kwamba baraka iweze kukaa katika nyumba zenu.
31 Makuhani hawaruhusiwi kula chochote, ikiwa ni ndege au mnyama, aliyekutwa akiwa amekufa au aliyeraruliwa na wanyama pori.
Makuhani hawatakula mzoga au mnyama aliyeraruliwa, iwe ni ndege au mnyama.