< Ezekieli 43 >
1 Kisha yule mtu akanileta kwenye lango linaloelekea upande wa mashariki,
Yule mtu kisha akanileta hata kwenye lango lililokuwa linaelekea mashariki.
2 nami nikaona utukufu wa Mungu wa Israeli ukija kutoka upande wa mashariki. Sauti yake ilikuwa kama ya ngurumo ya maji yaendayo kasi, nayo nchi ikangʼaa kwa utukufu wake.
Tazama! Utukufu wa Mungu wa Israeli ukaja kutoka mashariki; sauti yake ilikuwa kama sauti ya maji mengi, na nchi iling'aa kwa utukufu wake.
3 Maono niliyoyaona yalikuwa kama maono yale niliyokuwa nimeyaona wakati Mungu alipokuja kuangamiza mji na kama maono niliyokuwa nimeyaona kando ya Mto wa Kebari, nami nikaanguka kifudifudi.
Yalikuwa yanalingana na sura ya ono nililolona, kulingana na ono nililokuwa nimeliona wakati alipokuja kuuteketeza mji, na maono yalikuwa kama maono ambayo niliyokuwa nimeyaona Keberi Kanali nikaanguka kifudi fudi.
4 Utukufu wa Bwana ukaingia hekaluni kwa kupitia lango linaloelekea upande wa mashariki.
Hivyo utukufu wa Yahwe ukaja kwenye nyumba ya karibu na njia ya lango lililokuwa wazi kwa upande wa magharibi.
5 Kisha Roho akanichukua na kunileta katika ule ua wa ndani, nao utukufu wa Bwana ulilijaza Hekalu.
Kisha Roho akanichukua na kunileta kwenye ua wa ndanni. Tazama! Utukufu wa Yahwe ulikuwa umeijaza nyumba.
6 Wakati yule mtu akiwa amesimama kando yangu, nilisikia mtu mmoja akisema nami kutoka ndani ya Hekalu.
Mtu alisimama karibu na mimi, na nikamsikia mtu mwingine akizungumza na mimi kutoka kwenye nyumba.
7 Akasema, “Mwanadamu, hapa ni mahali pa kiti changu cha enzi na mahali pa kuweka nyayo za miguu yangu. Hapa ndipo nitakapoishi miongoni mwa Waisraeli milele. Kamwe nyumba ya Israeli hawatalinajisi tena Jina langu takatifu, yaani, wao wala wafalme wao, kwa ukahaba wao na kwa sanamu zao zisizokuwa na uhai za wafalme wao katika mahali pao pa juu pa kuabudia miungu.
Akanambia, “Mwanadamu, hapa ndipo mahali pangu pa enzi na mahali kwa ajili ya ya miguu yangu, ambapo nitaishi kati ya watu wa Israeli milele. Nyumba ya Israeli haitalikufuru tena jina langu takatifu-wao au wafalme wao katika mahali patakatifu pao.
8 Walipoweka kizingiti chao karibu na kizingiti changu na miimo yao ya milango karibu na miimo yangu, pakiwa na ukuta tu kati yangu na wao, walilinajisi Jina langu takatifu kwa matendo yao ya machukizo. Kwa sababu hiyo niliwaangamiza kwa hasira yangu.
Hawatalikufuru tena jina langu takatifu kwa kuweka kizingiti chao karibu na kizingiti changu, na nguzo yao ya lango karibu na nguzo yangu ya lango, bila kitu lakini ukuta kati yangu na wao. Wamelikufuru jina langu kwa matendo yao machafu, hivyo nimewala kwa hasira yangu.
9 Basi sasa na waweke mbali nami ukahaba wao na sanamu za wafalme wao zisizo na uhai, nami nitakaa miongoni mwao milele.
Sasa waache waondoe udanganyifu wao na maiti za wafalme wao kutoka kwangu, na nitaishi katikati yao milele.
10 “Mwanadamu, elezea hilo Hekalu kwa watu wa Israeli, ili wapate kuona aibu kwa ajili ya dhambi zao. Wao na wapime hicho kielelezo.
Mwanadamu, wewe mwenyewe utaiambia nyumba ya Israeli kuhusu nyumba hii hivyo watajiskia aibu ya uovu wao. Wanaweza kutafakari kuhusu haya maelezo.
11 Wakishaona aibu kwa ajili ya yale yote waliyotenda, wafahamishe kielelezo cha hilo Hekalu, yaani mpangilio wake, maingilio yake ya kutoka na kuingia, kielelezo chake chote, na masharti yake yote na sheria zake zote. Yaandike haya mbele yao ili wapate kuwa waaminifu kwa hicho kielelezo chake na kufuata masharti yake yote.
Kwa kuwa wameaibika kwa yote waliyoyafanya, kisha waonyeshe mchoro wa nyumba, maelezo yake, matokeo yake, maingio yake, na mchoro wake, sheria zake zote na kanuni. Kisha andika hivi chini mbele ya macho yao ili waweze kutunza michoro yote na kanuni zake zote, hivyo kama wazitiivo.
12 “Hii ndiyo sheria ya Hekalu: Eneo lote linalozunguka Hekalu juu ya mlima litakuwa takatifu kuliko yote. Hii ndiyo sheria ya Hekalu.
Hii ndiyo sheria kwa ajili ya nyumba: Kutoka kwenye kilele cha mlima hata mpaka wote unaoizunguka, patakuwa patakatifu sana. Tazama! Hii ndiyo sheria kwa ajili ya nyumba.
13 “Hivi ndivyo vipimo vya madhabahu kwa dhiraa ndefu, yaani, dhiraa moja na nyanda nne: Tako lake liwe na kina cha hiyo dhiraa moja na upana wa hiyo dhiraa moja, ikiwa na ukingo wa shibiri moja kuizunguka pembeni. Hiki kitakuwa ndicho kimo cha madhabahu:
Hivi vitakuwa vipimo vya madhabahu katika dhiraa-hiyo dhiraa kuwa dhiraa ya kawaida na urefu wa kiganja. Hivyo mfereji ulio uzunguka madhabahu utakuwa dhiraa moja chini, na upana wake pia utakuwa dhiraa moja. Mpaka wa karibu uizungukayo machinjio shubiri moja. Hii itakuwa kitako cha madhabahu.
14 Kimo cha msingi kuanzia usawa wa ardhi mpaka kwenye mfereji sehemu ya chini kimo chake ni dhiraa mbili na upana wake ni dhiraa moja na kuanzia kwenye ukingo mdogo hadi kwenye ukingo mpana kimo chake ni dhiraa nne na upana wake ni dhiraa moja.
Usawa wa kutoka kwenye mferji hadi kwenye machinijo ya chini ya madhabahu itakuwa dhiraa mbili, na hiyo machinjio yenyewe itakuwa dhiraa moja upana. Kisha kutoka machinjio madogo hadi kwenye machinjio makubwa ya madhabahu, itakuwa dhiraa nne, na machinjio makubwa yatakuwa dhraa moja upana.
15 Pale pawashwapo moto madhabahuni kimo chake kitakuwa dhiraa nne, na pembe nne zinazoelekeza juu kutoka pale pawashwapo moto.
Meko juu ya madhabahu kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa ni dhiraa nne juu, na kuna pembe nne zilizoelekea juu kwenye meku.
16 Pale pawashwapo moto pa madhabahu ni mraba, urefu wake ni dhiraa kumi na mbili na upana wa dhiraa kumi na mbili.
Meku ina dhiraa kumi na moja urefu na dhiraa kumi na mbili upana, za mraba.
17 Pia sehemu ya juu ni mraba, urefu wake dhiraa kumi na nne na upana wa dhiraa kumi na nne, ikiwa na ukingo wa nusu dhiraa na mfereji kuizunguka madhabahu. Ngazi za kupandia madhabahuni zitaelekea upande wa mashariki.”
Mpaka wake ni dhiraa kumi na nne urefu na dhiraa kumi na nne upana pande zake zote nne, na ukingo wake ni nusu dhiraa upana. Mfereji ni dhiraa moja upana kuzuka kote pamoja na ngazi zielekeazo mashariki.”
18 Kisha akaniambia, “Mwanadamu, hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Haya ndiyo yatakayokuwa masharti ya kutoa dhabihu za kuteketezwa na kunyunyiza damu juu ya madhabahu itakapokuwa imejengwa.
Kisha akanambia, “Mwanadamu, Bwana Yahwe asema hivi: Hizi ndizo sheria kwa ajili ya madhabahu katika siku watakayoitengeza, kwa ajili kutoa sadaka ya kuteketezwa kwenye hiyo, na kwa jili ya kunyunyiza damu juu yake.
19 Utatoa fahali mchanga kuwa sadaka ya dhambi kwa makuhani, ambao ni Walawi, wa jamaa ya Sadoki, ndio watakaonikaribia kuhudumu mbele zangu, asema Bwana Mwenyezi.
Utatoa ng'ombe kutoka kwenye kundi kama sadaka ya dhambi kwa ajili ya Walawi makuhani ambao ni uzao wa Zadoki, wale wajao karibu nami kunitumikia-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.
20 Itakupasa kuchukua baadhi ya hiyo damu ya mnyama huyo na kuiweka juu ya hizo pembe nne za madhabahu na juu ya ncha zake nne za sehemu ya juu kuzunguka ukingo wote, ili kuitakasa madhabahu na kufanya upatanisho kwa ajili yake.
Kisha utachukua baadhi ya damu yake na kuiweka juu pembe nne za madhabahu na pande nne za machinjio na kuuzunguka ukingo; utaitakasa na kufanya upatanisho kwa ajili yake.
21 Itakupasa kumchukua huyo fahali mchanga kwa ajili ya sadaka ya dhambi na kumteketeza mahali palipoagizwa katika eneo la Hekalu nje ya mahali Patakatifu.
Kisha chukua ng'ombe kama sadaka ya dhambi na iteketezwe katika eneneo lililotengwa la nje ya patakatifu.
22 “Siku ya pili yake utamtoa beberu asiye na dosari kwa ajili ya sadaka ya dhambi, nayo madhabahu itatakaswa kama ilivyotakaswa kwa yule fahali.
Kisha katika siku ya pili utatoa mbuzi dume asiyekuwa na dosari kutoka kundini kama sadaka ya dhambi; makuhani wataisafisha madhabahu kama walivyoisafisha kwa ng'ombe.
23 Utakapokuwa umemaliza kazi ya kuitakasa, utamtoa fahali mchanga pamoja na kondoo dume toka kwenye kundi, wote wawe hawana dosari.
Utakapomaliza kusafisha, toa ng'ombe asiyekuwa na dosari kutoka kwenye mifugo na kondoo dume asiyekuwa na dosari kutoka kundini.
24 Utawatoa mbele za Bwana, nao makuhani watanyunyizia chumvi juu yao na kuwatoa kuwa sadaka ya kuteketezwa kwa Bwana.
Watoe mbele ya Yahwe; makuhani watanyunyiza chumvi juu yao na kuwainua juu kama sadaka ya kutekezwa kwa Yahwe.
25 “Kwa siku saba itakupasa kutoa beberu kila siku kwa ajili ya sadaka ya dhambi, pia itakupasa kutoa fahali mchanga na kondoo dume kutoka zizini, wote wawe hawana dosari.
Utaandaa mbuzi dume kama sadaka ya dhambi kila siku kwa mda wa siku saba, na makuhani pia wataandaa ng'ombe asiye na dosari kutoka kwenye kundi na kondoo dume kutoka kwenye kundi.
26 Kwa siku saba itawapasa kufanya upatanisho kwa ajili ya madhabahu na kuitakasa na hivyo ndivyo watakavyoiweka wakfu.
Wataipatanisha madhabahu kwa siku saba na kuitakasa, wataitakasa kwa njia hii.
27 Mwishoni mwa hizi siku saba, kuanzia siku ya nane na kuendelea, itawapasa makuhani kutoa sadaka zenu za kuteketezwa na sadaka za amani juu ya madhabahu. Kisha nitawakubali ninyi, asema Bwana Mwenyezi.”
Watamaliza hizi siku saba, na katika siku ya nane na kuendelea itakuwa kwamba makuhani wataandaa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani kwenye madhabahu, ndipo nitakapowakubali-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.”