< Ezekieli 41 >

1 Kisha yule mtu akanileta katika sehemu ya nje ya patakatifu, naye akaipima miimo; upana wake ulikuwa dhiraa sita kila upande.
Kisha yule mtu akanileta mahali patakatifu pa hekalu na mihimili-dhiraa sita upana pande zote.
2 Ingilio lilikuwa la upana wa dhiraa kumi na kuta zilizojitokeza kila upande zilikuwa na upana wa dhiraa tano. Pia akapima sehemu ya nje ya patakatifu, nayo ilikuwa na urefu wa dhiraa arobaini na upana wa dhiraa ishirini.
Upana wa maingilio ulikuwa dhiraa kumi; ukuta kila upande dhiraa tano urefu kila upande. Kisha yule mtu akapima ukubwa wa mahali patakatifu-dhiraa arobaini upana urefu na dhiraa ishirini upana.
3 Kisha akaingia sehemu takatifu ndani ya Hekalu na kupima miimo ya ingilio, kila mmoja ulikuwa na upana wa dhiraa mbili. Ingilio lilikuwa na upana wa dhiraa sita, na kuta zilizotokeza kila upande zilikuwa na upana wa dhiraa saba.
Kisha yule mtu akaenda hata mahali patakatifu sana na kuipima miimili ya matokeo-dhiraa mbili-kuta pande zote zilikuwa dhiraa saba upana.
4 Naye akapima urefu wa sehemu takatifu ndani, nao ulikuwa dhiraa ishirini, na upana wake ulikuwa dhiraa ishirini hadi mwisho wa sehemu ya nje ya sehemu takatifu. Akaniambia, “Hapa ndipo Patakatifu pa Patakatifu.”
Kisha akapima urefu wa vyumba-dhiraa ishirini. Upana wake-dhiraa ishirini hata mbele kwenye ukumbi wa hekalu. Kisha akanambia, “Hapa ndipo mahali patakatifu sana.”
5 Kisha akapima ukuta wa Hekalu, nao ulikuwa na unene wa dhiraa sita, na kila chumba cha pembeni kuzunguka Hekalu kilikuwa na upana wa dhiraa nne.
Kisha yule akapima kuta za nyumba-zilikuwa dhiraa sita unene. Upana wa kila upande wa chumba kuzunguka nyumba dhiraa nne upana.
6 Vyumba vya pembeni vilikuwa na ghorofa tatu, kimoja juu ya kingine, kila ghorofa ilikuwa na vyumba thelathini. Kulikuwa na boriti katika ukuta wote wa Hekalu ili kuimarisha vyumba vya pembeni, kwa hiyo boriti hizo hazikushikamanishwa kwenye ukuta wa Hekalu.
Kulikuwa na pande tatu za vyumba, chumba kimoja juu ya kingine, vyumba thelathini, kulikuwa na kibao kitokezacho ukutani kuzunguka ukuta wa nyumba, kusaidia pande zote za vyumba, kwa kuwa hapakuwa na msaada uliokuwa umewekwa kwenye ukuta wa nyumba.
7 Vyumba vya pembeni vilivyozunguka Hekalu vilizidi kupanuka kulingana na sakafu zilivyokwenda juu. Ujenzi uliozunguka Hekalu ulijengwa kukwea juu, kwa hiyo vyumba vilipanuka kwa kadiri ya kila kimoja kilivyokwenda juu. Ngazi za kupandia zilianzia sakafu ya chini hadi sakafu ya juu kabisa kwa kupitia sakafu ya kati.
Hivyo mbavu za nyumba zilipanuka na kuzunguka kwenda juu, kwa kuwa nyumba ilizunguka kwenda juu, na ngazi kuelekea juu hata sehemu ya juu, kupitia sehemu ya katikati.
8 Nikaona pia kuwa Hekalu lilikuwa na kitako kilichoinuliwa pande zote, huu ulikuwa ndio msingi wa vile vyumba vya pembeni ambao ulikuwa na urefu wa ule ufito mmoja wa kupimia, yaani, dhiraa ndefu sita.
Kisha nikaona sehemu iliyoinuka kuzunguka nyumba, msingi kwa ajili ya pande za vyumba; ikapimwa fimbo nzima urefu-dhiraa sita.
9 Ukuta wa nje wa vyumba vya pembeni ulikuwa na unene wa dhiraa tano. Eneo la wazi katikati ya vyumba vya pembeni vya Hekalu
Upana wa ukuta wa vyumba vya pembeni kwa upande wa nje ulikuwa dhiraa tano. Kulikuwa na sehemu ya wazi kwa upande wa nje wa hivi vyumba katika patakatifu.
10 na vyumba vya makuhani lilikuwa na upana wa dhiraa ishirini kuzunguka Hekalu pande zote.
Kwa upande mwingine wa hii sehemu ya wazi kulikuwa na vyumba vya makuhani upande wa nje; hii sehemu ilikuwa na dhiraa ishirini upana kupazunguka patakatifu.
11 Kulikuwa na maingilio kwenye vyumba vya pembeni kutokea eneo lililo wazi, moja upande wa kaskazini na lingine upande wa kusini, nao msingi uliounganisha lile eneo la wazi ulikuwa na upana wa dhiraa tano ukilizunguka lote.
Kulikuwa na milango kwenye vyumba vya pembeni kutoka sehemu ya wazi nyingine-njia ya mlango moja uliokuwa upande wa kaskazini, na mwingine upande wa kusini. Upana wa hili eneo la wazi ulikuwa na dhiraa tano kupazunguka.
12 Jengo lililoelekeana na ua wa Hekalu upande wa magharibi lilikuwa na upana wa dhiraa sabini. Ukuta wa jengo hilo ulikuwa na unene wa dhiraa tano, kulizunguka lote, urefu ulikuwa wa dhiraa tisini.
Lile jengo lililokuwa limeelekea kwenye ua upande wa magaribi dhiraa sabini upana. Ukuta wake ulipimwa dhiraa tano pande zote, na ilikuwa dhiraa tisini urefu.
13 Kisha akapima Hekalu, lilikuwa na urefu wa dhiraa mia moja na ua wa Hekalu na jengo pamoja na kuta zake vilikuwa na urefu wa dhiraa mia moja pia.
Kisha yule mtu akapapima patakatifu-dhiraa mia moja urefu. jengo lililokuwa limetengeka, kuta zake, na kwenye ua pia palipimwa dhiraa mia moja urefu.
14 Upana wa ua wa Hekalu upande wa mashariki, pamoja na upande wa mbele wa Hekalu ulikuwa dhiraa mia moja.
Upana wa mbele kwenye ua mbele ya patakatifu pia kulikuwa dhiraa mia moja.
15 Kisha akapima urefu wa jengo linaloelekeana na ua upande wa nyuma wa Hekalu, pamoja na vyumba vyake kila upande, ilikuwa dhiraa mia moja. Sehemu takatifu ya nje, sehemu takatifu ya ndani, pamoja na baraza inayoelekeana na ukumbi,
Kisha yule mtu akapima urefu wa jengo karibu na patakatifu, kwa upande wake wa magharibi, na juu ya baraza pande zote-dhiraa mia moja. Mahali patakatifu na varanda,
16 pamoja na vizingiti, madirisha membamba na vyumba vyote vitatu, kila kimoja pamoja na kizingiti vilifunikwa kwa mbao. Sakafu, ukuta mpaka kwenye madirisha na madirisha yenyewe vilifunikwa kwa mbao.
kuta za ndani na madirisha, pamoja na madirisha madogo, na baraza za pande zote kwenye pande tatu, zilikuwa zimefungwa kwa mbao.
17 Katika nafasi iliyokuwa juu ya upande wa nje wa ingilio la sehemu takatifu ya ndani, na katika kuta zilizozunguka sehemu takatifu ya ndani na sehemu takatifu ya nje, kwa nafasi zilizo sawa,
Juu ya lango la kuingilia hata patakatifu pa ndani na kuwekwa karibu na kuta kulikuwa na pazia lililokuwa limepimwa.
18 kulinakshiwa makerubi na miti ya mitende. Miti ya mitende ilikuwa kati ya kerubi na kerubi. Kila kerubi alikuwa na nyuso mbili:
Palikuwa pamepambwa na makerubi mitende; pamoja na mitende kati ya kerubi na kerubi, na kila kerubi lilikuwa na nyuso mbili:
19 upande mmoja uso wa mwanadamu kuelekea mti wa mtende na upande mwingine uso wa simba ukielekea mti mwingine wa mtende. Ilinakshiwa kuzunguka Hekalu lote.
uso wa mtu aliyekuwa ameelekea mtende mmoja, na uso wa mwana simba ulitazama kuelekea mtende kwa upande mwingine. Vilifunikwa kuzunguka malango ya kuingia yote ya nyumba.
20 Kuanzia sakafu mpaka eneo lililo juu ya ingilio, palinakshiwa makerubi na miti ya mitende pamoja na kwenye ukuta wa nje wa patakatifu.
Kutoka chini hata juu kwenye njia ya mlango, makerubi na mtende vilifunikwa na ukuta wa nje ya nyumba.
21 Mahali patakatifu pa nje palikuwa na miimo ya mlango uliokuwa mraba na ule uliokuwa katika Patakatifu Pa Patakatifu ulikuwa unafanana na huo mwingine.
Mihimili ya lango la mahali patakatifu lilikuwa mraba. Umbo lao lilikuwa kama umbo la
22 Kulikuwa na madhabahu ya mbao kimo chake dhiraa tatu na ilikuwa dhiraa mbili mraba pande zote, tako lake na pande zake zilikuwa za mbao. Yule mtu akaniambia, “Hii ni meza ambayo iko mbele za Bwana.”
kwanza madhabahu ya mbao mbele ya mahali patakatifu, ambapo kulikuwa na dhiraa tatu kwenda juu na dhiraa urefu kwa kila upande. Pembe zake mihimili, kitako, na kiunzi kilitengenezwa kwa mbao. Kisha yule mtu akanambia, “Hii ni meza ambayo itakuwa kwa ajili ya Yahwe.”
23 Mahali patakatifu pa nje na Patakatifu Pa Patakatifu zilikuwa na milango miwili.
Kulikuwa na milango miwili kwa ajili ya mahali patakatifu na mahali patakatifu sana.
24 Kila mlango ulikuwa na vipande viwili, vipande viwili vilivyoshikwa na bawaba vyenye kufunguka kwa kila mlango.
Hii milango ilikuwa na bawaba mbili kila mlango paneli, paneli mbili kwa ajili ya mlango mmoja na paneli mbili kwa ajili ya mwingine.
25 Juu ya hiyo milango ya Patakatifu palinakshiwa makerubi na miti ya mitende kama yale yaliyonakshiwa kwenye kuta, na kulikuwa na ubao ulioningʼinia mbele ya baraza kwa nje.
Ilifunikwa-juu ya milango ya mahali patakatifu ambapo makerubi na mti wa mtende kama kuta ilipambwa, kulikuwa na paa ya mbao juu ya varanda kwa mbele.
26 Katika kuta za pembeni za ukumbi kulikuwa na madirisha membamba yaliyonakshiwa miti ya mitende kila upande. Vyumba vya pembeni vya Hekalu pia vilikuwa vimefunikwa kwa mbao.
Kulikuwa na madidsha madogo miti ya mitende kwenye varanda pande zote. Hivyo vilikuwa vyumba vya pembeni ya nyumba, na pia ilizielekea dari.

< Ezekieli 41 >