< Ezekieli 40 >

1 Katika mwaka wa ishirini na tano wa uhamisho wetu, mwanzoni mwa huo mwaka, siku ya kumi ya mwezi, katika mwaka wa kumi na nne baada ya kuanguka kwa mji, siku hiyo hiyo mkono wa Bwana ulikuwa juu yangu, naye akanipeleka huko.
Katika mwaka wa ishirini na tano wa kuhamishwa kwetu mwanzoni mwa mwaka siku ya kumi ya mwezi, katika mwaka wa kumi na nne baada ya mji kuchukuliwa-katika siku hiyo hiyo, mkono wa Yahwe ulikuwa juu yangu na alinichukua huko.
2 Nikiwa katika maono ya Mungu alinichukua mpaka nchi ya Israeli, naye akaniweka kwenye mlima mrefu sana, ambako upande wa kusini kulikuwepo baadhi ya majengo ambayo yalionekana kama mji.
Katika maono ya Mungu akanileta hata nchi ya Israeli. Akanileta kupumzika juu ya kila mlima mrefu sana; upande wa kusini kulikuwa na monekano kana kwamba majengo ya mji.
3 Akanipeleka huko, nami nikamwona mtu ambaye kuonekana kwake kulikuwa kama kuonekana kwa shaba. Alikuwa amesimama kwenye lango akiwa na kamba ya kitani na ufito wa kupimia mkononi mwake.
Kisha akanileta huko. Tazama, kulikuwa na mtu! Mwonekano wake ulikuwa kama mwonekano wa shaba. Alikuwa na uzi wa kitani na mwanzi wa kupimia mkononi mwake, na alisimama katika lango la mji.
4 Mtu huyo akaniambia, “Mwanadamu, angalia kwa macho yako na usikie kwa masikio yako nawe uzingatie kitu nitakachokuonyesha, kwa kuwa ndiyo sababu umeletwa hapa. Iambie nyumba ya Israeli kila kitu utakachoona.”
Huyo mtu akanambia, “Mwanadamu, tazama kwa macho yako na sikiliza kwa masikio yako, na elekeza moyo wako juu ya yote ninayokufunulia, kwa kuwa ulinileta hapa ili niweze kukufunulia haya wewe. Toa taarifa ya kila kitu utakachokiona kwa nyumba ya Israeli.
5 Nikaona ukuta uliozunguka eneo lote la Hekalu. Ule ufito wa kupimia uliokuwa mkononi mwa yule mtu ulikuwa na urefu wa dhiraa ndefu sita, yaani, dhiraa ndefu ni sawa na dhiraa na nyanda nne, akapima ule ukuta. Ukuta huo ulikuwa na unene wa dhiraa ndefu sita na kimo cha dhiraa ndefu sita.
Kulikuwa ukuta uliokuwa umezunguka eneo la hekalu. Urefu wa kipimo cha mwanzi katika mkono wa mtu ulikuwa dhiraa sita urefu, kila urefu wa dhiraa ulikuwa dhiraa moja na kipimo cha kiganja cha mkono urefu. Aliupima ukuta; ulikuwa kipimo cha mwanzi mmoja na ufito mmoja urefu.
6 Kisha akaenda kwenye lango linaloelekea mashariki. Akapanda ngazi zake akapima kizingiti cha lango, nacho kilikuwa na kina cha huo ufito.
Kisha akaenda hata kwenye lango la hekalu lililokuwa limeelekea mashariki. Akapanda ngazi na kuipima kizingiti cha lango-mwanzi mmoja upana.
7 Vyumba vya kupumzikia vya walinzi vilikuwa na urefu wa huo ufito mmoja na upana wa huo ufito, kuta zilizogawa vyumba hivyo vya mapumziko zilikuwa na unene wa dhiraa tano. Nacho kizingiti cha lango lililokuwa karibu na ukumbi unaoelekea hekaluni ulikuwa na kina cha huo ufito.
Vyumba vya ulinzi vilikuwa kila mwanzi mmoja urefu na mwanzi mmoja upana; kulikuwa na dhiraa tano katika kila vyumba viwili, na kizingiti cha lango la hekalu karibu na tawa la hekalu kilikuwa mwanzi mmoja urefu.
8 Kisha akapima baraza ya njia ya lango,
Akapima tawa la lango; ulikuwa mwanzi mmoja urefu.
9 ambayo ilikuwa na kina cha dhiraa nane na miimo yake ilikuwa na unene wa dhiraa mbili. Baraza ya lango ilielekea Hekalu.
Akapima tawa la lango. Ilikuwa mwanzi mmoja kwenda chini. Mihimili ilikuwa dhiraa mbili upana. Hili lilikuwa tawa la lango kuelekea hekalu.
10 Ndani ya lango la mashariki kulikuwepo vyumba vitatu vya kupumzikia kila upande, vyote vitatu vilikuwa na vipimo vilivyo sawa, nazo nyuso za kuta zilizotenganisha kila upande zilikuwa na vipimo vilivyo sawa.
Kulikuwa na vyumba vitatu vya ulinzi pande zote za lango la mashariki, na yote yalikuwa na kipimo kile kile, na kuta zilizokuwa zimezigawanya zilikuwa na kipimo kile kile.
11 Kisha akapima upana wa ingilio la lango, ilikuwa dhiraa kumi na urefu wake ulikuwa dhiraa kumi na tatu.
Kisha yule mtu akapima upana wa njia ya lango la kuingia-dhiraa kumi; na akapima urefu wa njia ya lango la kuingia-dhiraa kumi na tatu.
12 Mbele ya kila chumba cha kupumzikia kulikuwepo ukuta uliokuwa na kimo cha dhiraa moja kwenda juu, navyo hivyo vyumba vilikuwa dhiraa sita mraba.
Akaupima ukuta uliokuwa mpaka mbele ya vyumba-dhiraa moja urefu. Vyumba vilipimwa dhiraa sita kila upande.
13 Kisha akapima njia ya lango kuanzia juu ya ukuta wa nyuma wa chumba kimoja cha kupumzikia hadi juu ya ukuta wa nyuma wa chumba upande wa pili; kukawa na nafasi ya dhiraa ishirini na tano kuanzia lango la ukuta mmoja hadi lango la ukuta uliokuwa upande mwingine.
Kisha akapima lango la njia kutoka kwenye paa ya chumba kimoja kuelekea chumba kingine-dhiraa ishirini na tano, kutoka lango la kuingia chumba cha kwanza kuelekea kile cha pili.
14 Akapima pia ukumbi, urefu wa dhiraa ishirini na lango linalofuatia hiyo nguzo kila upande wa huo ukumbi.
Kisha akapima ukuta uliokuwa umeenda kati ya vyumba vya ulinzi-dhiraa sitini urefu; alipima kwa mbali na tawa la lango.
15 Umbali kuanzia ingilio la njia ya lango hadi mwisho kabisa wa baraza yake ulikuwa dhiraa hamsini.
Lango la kuingia kutoka lango la mbele kuelekea lango jingine la tawa la mwisho lilikuwa dhiraa hamsini.
16 Kulikuwa na vidirisha kwenye hivyo vyumba vya walinzi na nguzo za hivyo vyumba zilikuwa kwenye mzunguko wa hilo lango, vivyo hivyo kulikuwa na madirisha yaliyozunguka kuelekeana na ua na juu ya kila nguzo kulikuwa na mapambo ya miti ya mitende.
Kulikuwa na madirisha yaliyokuwa yamefungwa kuelekea vyumba na kuelekea nguzo zake kati ya malango kuzunguka kote; na vivyo hivyo kwa mabaraza. Kulikuwa na madirisha pande zote za ndani, na kila mhimili ulikuwa umepambwa kwa mitende.
17 Kisha akanileta katika ukumbi wa nje. Huko nikaona vyumba vingine pamoja na njia iliyokuwa imejengwa kuzunguka ukumbi wote, kulikuwa na vyumba thelathini vimepangana kando ya hiyo njia.
Kisha huyo mtu akanileta hata ua wa nje mwa hekalu. Tazama, kulikuwa na vyumba, na kulikuwa na kibamba katika ua, pamoja na vyumba thelathini baada ya kibamba.
18 Njia hii iliyojengwa iliambaa na lango, ikiwa na urefu sawa na lango, hii ilikuwa ni njia ya chini.
Kibamba kilienda juu hata upande wa malango, na upana wake ulikuwa sawsawa na urefu wa malango. Hiki kilikuwa kibamba cha chini.
19 Kisha akapima umbali kutoka ndani ya lango la chini mpaka nje ya ukumbi wa ndani, nao ulikuwa dhiraa mia moja upande wa mashariki na dhiraa mia moja upande wa kaskazini.
Kisha huyo mtu akapima umbali kutoka mebele ya lango la chini hata mbele ya lango la ndani; ilikuwa dhiraa mia moja upande wa mashariki, na sawasawa na upande wa kaskazini.
20 Kisha akapima urefu na upana wa lango linaloelekea kaskazini, kukabili ukumbi wa nje.
Kisha akapima urefu na upana wa lango lililokuwa upande wa kaskazini mwa ua wa nje.
21 Vyumba vyake vilikuwa vitatu kila upande, kuta zilizogawanya vyumba na baraza ilikuwa na vipimo sawa na zile kuta za lango la kwanza. Zilikuwa na urefu wa dhiraa hamsini na upana wa dhiraa ishirini na tano.
Kulikuwa na vyumba vitatu pande zote za lango, na lango na matawa yake yalipimwa sawa na lango kubwa-dhiraa hamsini upana wote na dhiraa ishirini na tano upana.
22 Madirisha yake, baraza yake na nakshi yake ya miti ya mitende vilikuwa na vipimo sawasawa na vile vya lango linaloelekea mashariki. Kulikuwa na ngazi saba za kupandia huko, pamoja na baraza yake mkabala nazo.
Madirisha yake, tawa, vyumba, na mitende yake vilikabiliana na lango ambalo linaloelekea mashariki. Ngazi saba kuupandia juu hata kwenye tawa lake.
23 Kulikuwa na lango kwenye ukumbi wa ndani lililoelekea lile lango la kaskazini, kama vile ilivyokuwa ule upande wa mashariki. Akapima kutoka lango moja hadi lile lililo mkabala nalo, lilikuwa dhiraa mia moja.
Kulikuwa na lango kwenye ua wa ndani mbele kuelekea mashariki; huyo mtu alipima kutoka lango moja hadi lango jingine-dhiraa mia moja umbali.
24 Ndipo akaniongoza mpaka upande wa kusini, nami nikaona lango linaloelekea kusini. Akaipima miimo yake na baraza yake, navyo vilikuwa na vipimo sawa kama hivyo vingine.
Kisha huyo mtu akanileta hata kwenye lango la kuingia la kusini, na kuta zake na tawa vilipimwa sawa kama malango mengine ya nje.
25 Lango na baraza yake vilikuwa na madirisha membamba pande zote, kama madirisha ya huko kwingine. Ilikuwa na urefu wa dhiraa hamsini na upana wake dhiraa ishirini na tano.
Kulikuwa na madirisha yaliyofungwa katika lango la njia na tawa lake kama lile lango. Lango la kusini na tawa lake vilipimwa dhiraa hamsini urefu na dhiraa ishirini na tano upana.
26 Kulikuwa na ngazi saba za kupandia huko, pamoja na baraza yake mkabala nazo. Ilikuwa na nakshi za miti ya mitende kwenye kuta zilizogawanya vyumba kila upande.
Kulikuwa na ngazi saba hadi kwenye lango na matawa yake, na kulikuwa na mitende iliyochongoka juu ya kuta pande zote.
27 Ukumbi wa ndani pia ulikuwa na lango lililoelekea kusini. Naye akapima kutoka lango hili mpaka kwenye lango la nje upande wa kusini; ilikuwa dhiraa mia moja.
Kulikuwa na lango la ua wa ndani upande wa kusini, na yule mtu akapima kutoka hilo lango hata lango la kuingia upande wa kusini-dhiraa mia moja umbali.
28 Kisha akanileta mpaka ukumbi wa ndani kwa kupitia lango la kusini, naye akapima lango la kusini, ambalo lilikuwa na vipimo sawa na yale mengine.
Kishi huyo mtu akanileta hata ua wa ndani karibu na lango lake la kusini, ambalo lilikuwa na vipimo vile vile kama malango mengine.
29 Vyumba vyake, kuta zilizogawanya vyumba na ukumbi wake zilikuwa na vipimo sawasawa na zile nyingine. Hilo lango na baraza yake vilikuwa na madirisha pande zote. Navyo vilikuwa na urefu wa dhiraa hamsini na upana wa dhiraa ishirini na tano.
Vyumba vyake, kuta, na matao vilipimwa sawa kama malango mengine; kulikuwa na madirisha kuzunguka matao yote. Lango la ndani na matao yake yalipimwa dhiraa hamsini urefu na dhiraa ishirini na tano upana.
30 (Baraza za malango zilizozunguka ukumbi wa ndani zilikuwa na upana wa dhiraa ishirini na tano na kina cha dhiraa tano.)
Pia kulikuwa na matao pande zote za kuta za ndani; haya yalikuwa dhiraa ishirini na tano urefu na dhiraa tano upana.
31 Baraza yake ilielekeana na ukumbi wa nje, miimo yake ilinakshiwa miti ya mitende, kulikuwa na ngazi nane za kupandia huko.
Hili tawa lilielekea ua wa nje pamoja na mitende iliyochongwa juu ya kuta zake na ngazi nane kuupandia.
32 Kisha akanileta mpaka kwenye ukumbi wa ndani ulioko upande wa mashariki, naye akalipima lango hilo, lilikuwa na vipimo vilivyo sawasawa na yale mengine.
Kisha yule mtu akanileta hata kwenye ua wa ndani karibu na njia ya kaskazini na kulipima lango, ambalo lilikuwa na vipimo sawa kama malango mengine.
33 Vyumba vyake, kuta zake na baraza yake vilikuwa na vipimo vilivyo sawa na vile vingine. Lile lango pamoja na baraza yake vilikuwa na madirisha pande zote. Urefu wake ulikuwa dhiraa hamsini na upana wake dhiraa ishirini na tano.
Vyumba vyake, kuta, na matawa yalikuwa na kipima sawa kama cha malango, na kulikuwa na madirisha pande zote. Laango la ndani na matawa yake yalikuwa dhiraa hamsini urefu na dhiraa ishirini na tano upana.
34 Baraza yake ilielekea ukumbi wa nje, miimo yake ilinakshiwa miti ya mitende pande zote. Kulikuwa na ngazi nane za kupandia huko.
Matawa yake yalielekea nje ya ua; ilikuwa na mitende pande zote za hiyo na ngazi nane za kuupandia.
35 Kisha akanileta mpaka kwenye lango la kaskazini na kulipima. Lilikuwa na vipimo sawa na yale mengine,
Kisha huyo mtu akanileta hata lango la kaskazini na kulipima; likapimwa vivyo hivyo kama malango mengine.
36 kama vile ilivyokuwa kwa vyumba, kuta zake na baraza yake, tena kulikuwa na madirisha pande zote. Ilikuwa na urefu wa dhiraa hamsini na upana wake dhiraa ishirini na tano.
Vyumba vyake, kuta, na ukumbi vilipimwa sawa na malango mengine, na kulikuwa na madirisha pande zote. Njia ya lango na matao yake yalipimwa dhiraa hamsini urefu na upana dhiraa ishirini na tano.
37 Baraza yake ilielekeana na ukumbi wa nje, miimo yake ilinakshiwa miti ya mitende pande zote, kulikuwa na ngazi nane za kupandia huko.
Tatawa lake lilielekea ua wa nje; ilikuwa na mitende pande zote za huo na ngazi nane kuupandia.
38 Kulikuwa na chumba na mlango karibu na baraza katika kila njia ya ndani ya lango ambamo sadaka za kuteketezwa zilioshwa.
Kulikuwa na chumba pamoja na mlango karibu na kila lango la ndani. Hapa ndipo ambako walipooshea sadaka za kutekezwa.
39 Kwenye baraza ya lile lango kulikuwepo meza mbili kila upande, ambako sadaka za kuteketezwa, sadaka za dhambi na sadaka za hatia zilichinjiwa.
Kulikuwa na meza mbili kila upande wa kila ukumbi, ambako sadaka ya kuteketezwa ilipochinjiwa, na pia sadaka ya dhambi na sadaka ya hatia.
40 Karibu na ukuta wa nje wa baraza ya lile lango karibu na ngazi kwenye ingilio kuelekea kaskazini kulikuwa na meza mbili, nako upande mwingine wa ngazi kulikuwepo na meza mbili.
Karibu na ukuta wa ua, kuelekea juu kwenye lango kuelekea kaskazini, kulikuwa na meza mbili. Pia kwa upande mwingine kulikuwa na meza mbili kwenye lango la ukumbi.
41 Kwa hiyo kulikuwa na meza nne upande mmoja wa lango na nyingine nne upande mwingine, zote zilikuwa meza nane, ambapo dhabihu zilichinjiwa.
Kulikuwa na meza nne pande zote karibu na lango; wakachinja wanyama juu ya meza nane.
42 Pia kulikuwa na meza nne za mawe yaliyochongwa kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa, kila meza ilikuwa na urefu wa dhiraa moja na nusu, upana wake dhiraa moja na nusu na kimo cha dhiraa moja. Juu ya meza hizo viliwekwa vyombo vya kuchinjia sadaka za kuteketezwa na dhabihu nyingine mbalimbali.
Kulikuwa na meza nne za mawe yaliyochongwa kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, dhiraa moja na nusu urefu, dhiraa moja na nusu upana, na kimo dhiraa moja. Juu yake waliweka vyombo pamoja ambavyo walivichinjia sadaka za kuteketezwa kwa ajili ya sadaka.
43 Kulikuwa na kulabu, urefu wake nyanda nne, zilikuwa zimeshikizwa ukutani pande zote. Meza zilikuwa kwa ajili ya nyama za sadaka.
Kulabu mbili ujazo wa kiganja urefu uliokuwa umeunganishwa katika ua pande zote, na nyama ya matoleo ilikuwa imewekwa juu ya meza.
44 Nje ya lango la ndani, kwenye ukumbi wa ndani, kulikuwa na vyumba viwili, kimoja upande wa lango la kaskazini nacho kilielekea kusini, kingine upande wa lango la kusini nacho kilielekea kaskazini.
Karibu na lango la ndani, katika ua wa ndani, kulikuwa na vyumba vya waimbaji. Moja ya hivi vyumba kilikuwa upande wa kaskazini, na kingine kusini.
45 Akaniambia, “Chumba kinachoelekea upande wa kusini ni kwa ajili ya makuhani ambao wana usimamizi wa hekaluni,
Kisha yule mtu akanambia, “Hiki chumba kinachoelekea kusini ni kwa ajili ya makuhani walio zamu katika hekalu.
46 nacho chumba kinachoelekea upande wa kaskazini ni kwa ajili ya makuhani wenye usimamizi wa madhabahuni. Hawa ni wana wa Sadoki, ambao ndio Walawi pekee wanaoweza kumkaribia Bwana ili kuhudumu mbele zake.”
Chumba kilichoelekea kaskazini kilikuwa kwa ajili ya makuhani waliokuwa zamu kwenye madhabahu. Hawa ni wana wa Sadoki ambaye huja humkaribia Yahwe kumtumikia; ambao ni miongoni mwa wana wa Lawi.”
47 Ndipo alipopima ukumbi: nao ulikuwa mraba wa dhiraa mia moja urefu na upana. Madhabahu yalikuwa mbele ya Hekalu.
Kisha akaupima ule ua-dhiraa mia moja urefu na dhiraa mia moja upana mraba, pamoja na madhabahu mbele ya nyumba.
48 Akanileta mpaka kwenye baraza ya Hekalu naye akaipima miimo ya hiyo baraza, nayo ilikuwa na upana wa dhiraa tatu kila upande. Upana wa ingilio ulikuwa dhiraa kumi na nne na kuta zake zilikuwa na upana wa dhiraa tatu kila upande.
Kisha yule mtu akanileta hata kwenye varanda ya nyumba na kupima mwimo wa milango yake-ilikuwa dhiraa tano unene upande huu. Njia ya kuingilia yenyewe ilikuwa dhiraa kumi na nne, na kuta pande zote za huo zilikuwa dhraa tatu upana.
49 Baraza ilikuwa na dhiraa ishirini kwenda juu na dhiraa kumi na mbili kuanzia mbele hadi nyuma. Kulikuwa na ngazi kumi za kupandia huko, pia kulikuwa na nguzo kwa kila upande wa miimo.
Urefu wa ukumbi ulikuwa dhiraa ishirini, na upana wake ulikuwa dhiraa kumi na moja. Kulikuwa na ngazi zilizokuwa zimepanda juu na nguzo zilizokuwa zimesimama pande zote za huo.

< Ezekieli 40 >