< Ezekieli 38 >

1 Neno la Bwana likanijia kusema:
ויהי דבר יהוה אלי לאמר׃
2 “Mwanadamu, kaza uso wako dhidi ya Gogu, katika nchi ya Magogu, mkuu wa Roshi, Mesheki na Tubali, tabiri dhidi yake
בן אדם שים פניך אל גוג ארץ המגוג נשיא ראש משך ותבל והנבא עליו׃
3 na useme: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Ee Gogu, mimi ni kinyume nawe, mtawala mkuu wa Roshi, Mesheki na Tubali.
ואמרת כה אמר אדני יהוה הנני אליך גוג נשיא ראש משך ותבל׃
4 Nitakugeuza kuelekea ulikotoka na kukutia ndoana kwenye mataya yako na kukutoa nje wewe pamoja na jeshi lako lote, yaani, farasi wako, wapanda farasi wako waliojiandaa tayari kwa vita, pamoja na kundi kubwa la wajeuri wakiwa na ngao na vigao, wote wakipunga panga zao.
ושובבתיך ונתתי חחים בלחייך והוצאתי אותך ואת כל חילך סוסים ופרשים לבשי מכלול כלם קהל רב צנה ומגן תפשי חרבות כלם׃
5 Uajemi, Kushi na Putu watakuwa pamoja nao, wote wakiwa na ngao na kofia za chuma,
פרס כוש ופוט אתם כלם מגן וכובע׃
6 pia Gomeri pamoja na vikosi vyake vyote, na Beth-Togarma kutoka kaskazini ya mbali pamoja na vikosi vyake vyote, mataifa mengi wakiwa pamoja nawe.
גמר וכל אגפיה בית תוגרמה ירכתי צפון ואת כל אגפיו עמים רבים אתך׃
7 “‘Jiandae, uwe tayari, wewe na makundi yako yote ya wajeuri yaliyokusanyika pamoja nawe, nawe waamrishe.
הכן והכן לך אתה וכל קהלך הנקהלים עליך והיית להם למשמר׃
8 Baada ya siku nyingi utaitwa vitani. Katika miaka ijayo, utaivamia nchi ile ambayo imepona kutoka vita, ambayo watu wake walikusanywa kutoka mataifa mengi kuja katika milima ya Israeli, ambayo kwa muda mrefu ilikuwa imeachwa ukiwa. Wameletwa kutoka mataifa na sasa wote wanaishi katika hali ya salama.
מימים רבים תפקד באחרית השנים תבוא אל ארץ משובבת מחרב מקבצת מעמים רבים על הרי ישראל אשר היו לחרבה תמיד והיא מעמים הוצאה וישבו לבטח כלם׃
9 Wewe na vikosi vyako vyote na mataifa mengi yaliyo pamoja nawe mtapanda juu, mtawazoa kama tufani na kuifunika nchi kama wingu.
ועלית כשאה תבוא כענן לכסות הארץ תהיה אתה וכל אגפיך ועמים רבים אותך׃
10 “‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Katika siku ile mawazo yataingia moyoni mwako nawe utapanga mipango mibaya.
כה אמר אדני יהוה והיה ביום ההוא יעלו דברים על לבבך וחשבת מחשבת רעה׃
11 Utasema, “Nitapigana vita na nchi ambayo vijiji vyake havina maboma. Nitawashambulia watu wanaoishi kwa amani na wasiotarajia vita: wote wanaishi bila maboma na bila malango na makomeo.
ואמרת אעלה על ארץ פרזות אבוא השקטים ישבי לבטח כלם ישבים באין חומה ובריח ודלתים אין להם׃
12 Nitateka mateka na kuchukua nyara mali za wale waliorudi kuishi katika mahame na wale watu waliokusanywa kutoka kwa mataifa, ambao sasa wana mifugo na mali nyingi, wanaoishi katikati ya nchi.”
לשלל שלל ולבז בז להשיב ידך על חרבות נושבת ואל עם מאסף מגוים עשה מקנה וקנין ישבי על טבור הארץ׃
13 Sheba na Dedani pamoja na wafanyabiashara wa Tarshishi na vijiji vyake vyote watakuambia, “Je, umekuja kuteka mateka? Je, umekusanya makundi yako ya wajeuri ili kuchukua nyara mali, kutwaa fedha na dhahabu, kutunyangʼanya mifugo na mali na kuteka nyara nyingi zaidi?”’
שבא ודדן וסחרי תרשיש וכל כפריה יאמרו לך הלשלל שלל אתה בא הלבז בז הקהלת קהלך לשאת כסף וזהב לקחת מקנה וקנין לשלל שלל גדול׃
14 “Kwa hiyo, mwanadamu, tabiri na umwambie Gogu: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Katika siku ile, watu wangu Israeli watakapokuwa wanaishi salama, Je, wewe mwenyewe hutalijua hilo?
לכן הנבא בן אדם ואמרת לגוג כה אמר אדני יהוה הלוא ביום ההוא בשבת עמי ישראל לבטח תדע׃
15 Utakuja kutoka kwako huko kaskazini ya mbali, ukiwa pamoja na mataifa mengi, wote wakiwa wamepanda farasi, kundi kubwa, jeshi kuu.
ובאת ממקומך מירכתי צפון אתה ועמים רבים אתך רכבי סוסים כלם קהל גדול וחיל רב׃
16 Utakuja dhidi ya watu wangu Israeli kama wingu lifunikavyo nchi. Siku zijazo, ee Gogu, nitakuleta wewe dhidi ya nchi yangu, ili kwamba mataifa wapate kunijua Mimi nitakapojionyesha mtakatifu kwa kukupitia wewe mbele ya macho yao.
ועלית על עמי ישראל כענן לכסות הארץ באחרית הימים תהיה והבאותיך על ארצי למען דעת הגוים אתי בהקדשי בך לעיניהם גוג׃
17 “‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Je, wewe si yule niliyenena juu yako katika siku za zamani kwa kupitia kwa watumishi wangu manabii wa Israeli? Wakati ule walitabiri kwa miaka mingi kwamba ningekuleta upigane nao.
כה אמר אדני יהוה האתה הוא אשר דברתי בימים קדמונים ביד עבדי נביאי ישראל הנבאים בימים ההם שנים להביא אתך עליהם׃
18 Hili ndilo litakalotokea katika siku ile: Gogu atakaposhambulia nchi ya Israeli, hasira yangu kali itaamka, asema Bwana Mwenyezi.
והיה ביום ההוא ביום בוא גוג על אדמת ישראל נאם אדני יהוה תעלה חמתי באפי׃
19 Katika wivu wangu na ghadhabu yangu kali ninasema kuwa wakati ule patakuwepo tetemeko kuu katika nchi ya Israeli.
ובקנאתי באש עברתי דברתי אם לא ביום ההוא יהיה רעש גדול על אדמת ישראל׃
20 Samaki wa baharini, ndege wa angani, wanyama wa kondeni, kila kiumbe kitambaacho ardhini, na watu wote walio juu ya uso wa nchi watatetemeka mbele zangu. Milima itapinduka, majabali yatapasuka na kila ukuta utaanguka chini.
ורעשו מפני דגי הים ועוף השמים וחית השדה וכל הרמש הרמש על האדמה וכל האדם אשר על פני האדמה ונהרסו ההרים ונפלו המדרגות וכל חומה לארץ תפול׃
21 Nitaita upanga vita dhidi ya Gogu juu ya milima yangu yote, asema Bwana Mwenyezi. Upanga wa kila mtu utakuwa dhidi ya ndugu yake.
וקראתי עליו לכל הרי חרב נאם אדני יהוה חרב איש באחיו תהיה׃
22 Nitatekeleza hukumu juu yake kwa tauni na kwa umwagaji wa damu. Nitaifanya mvua ya mafuriko kunyesha, mvua ya mawe na moto wa kiberiti juu yake na juu ya vikosi vyake na juu ya mataifa mengi walio pamoja naye.
ונשפטתי אתו בדבר ובדם וגשם שוטף ואבני אלגביש אש וגפרית אמטיר עליו ועל אגפיו ועל עמים רבים אשר אתו׃
23 Nami hivyo ndivyo nitakavyoonyesha ukuu wangu na utakatifu wangu, nami nitajijulisha mbele ya macho ya mataifa mengi. Ndipo watakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana.’
והתגדלתי והתקדשתי ונודעתי לעיני גוים רבים וידעו כי אני יהוה׃

< Ezekieli 38 >