< Ezekieli 34 >

1 Neno la Bwana likanijia kusema:
Kisha neno la Yahwe likanijia, kusema,
2 “Mwanadamu, tabiri juu ya wachungaji wa Israeli, tabiri na uwaambie: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Ole wa wachungaji wa Israeli ambao hujitunza wenyewe tu! Je, haiwapasi wachungaji kutunza kundi la kondoo?
“Mwanadamu, tabiri dhidi ya wachungaji wa Israeli. Toa unabii na waambie, 'Bwana Yahwe asema hivi kwa wachungaji: Ole kwa wachungaji wa Israeli wanaojilisha wenyewe. Je! wachungaji hawapaswi kulilinda kundi?
3 Mnakula mafuta ya wanyama, mnavaa mavazi ya sufu na kuchinja kondoo walionona, lakini hamlitunzi kundi.
Mnakula mafungu yaliyonona na mnavaa sufu. Mnawachinja walionona. Hamkuwalisha siku zote.
4 Hamkuwatia nguvu walio dhaifu wala hamkuwaganga wenye maradhi wala kuwafunga waliojeruhiwa. Hamkuwarudisha waliotangatanga wala kuwatafuta wale waliopotea. Badala yake mmewatawala kwa ukali na kwa ukatili.
Hamkuwatia nguvu wagonjwa, wala hamkuwaponya wenye maradhi. Hamkuwafungua wale waliovunjika, hamkuwarudisha waliofukuzwa au kuwatafuta waliopotea. Badala yake, mmetawala juu yao kwa nguvu na vurugu.
5 Hivyo walitawanyika kwa sababu hapakuwepo mchungaji, nao walipotawanyika, wakawa chakula cha wanyama wa mwitu wote.
Kisha walikuwa wametawanyika bila mchungaji, na wakawa chakula kwa wanyama wote waishio katika mashamba, walipokuwa wametawanyika.
6 Kondoo wangu walitawanyika, wakatangatanga kwenye milima yote na kwenye kila kilima kirefu. Kondoo wangu walitawanyika juu ya uso wa dunia yote bila kuwa na yeyote wa kuwaulizia wala wa kuwatafuta.
Kundi langu limetawanyika juu ya milima yote na juu ya kilima kirefu, na limetawanyika juu ya uso wote wa dunia. Wala hakuna anayewatafua.
7 “‘Kwa hiyo, ninyi wachungaji, lisikieni neno la Bwana:
Kwa hiyo, wachungaji, sikilizeni neno la Yahwe:
8 Kwa hakika kama niishivyo, asema Bwana Mwenyezi, kwa sababu kondoo zangu wamekosa mchungaji na hivyo wametekwa nyara na kuwa chakula cha wanyama wote wa mwituni na kwa sababu wachungaji wangu, hawakuwatafuta kondoo zangu, bali wachungaji wamejitunza wenyewe, nao hawakuwalisha kondoo zangu,
Kama niishivyo-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-kwa sababu kundi langu limekuwa mateka na chakula kwa ajili ya wanyama katika mashamba, kwa sababu hapakuwa na mchungaji yeyote, lakini wachungaji walijilisha wenyewe na hawakulisha kundi langu.
9 kwa hiyo enyi wachungaji, sikieni neno la Bwana:
Kwa hiyo, wachungaji, lisikilizeni neno la Yahwe:
10 Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Mimi ni kinyume na wachungaji nami nitawadai kondoo zangu mikononi mwao. Nitawafukuza kutoka kwenye kuchunga kundi langu, ili wachungaji wasiendelee kujitunza wenyewe. Nitaokoa kondoo zangu kutoka kwenye vinywa vyao, nao kondoo hawatakuwa tena chakula chao.
Bwana Yahwe asema hivi: Tazama! Niko juu ya wachungaji, na nitalitaka kundi langu kutoka mkononi mwake. Kisha nitawaachisha kutoka kulichunga kundi; wala wachungaji hawatajilisha wenyewe tena kwa kuwa nitaliondoa kundi langu kutoka midomoni mwao, ili kwamba kundi langu lisiwe chakula kwa ajili yao tena.
11 “‘Kwa kuwa hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Mimi mwenyewe nitawaulizia kondoo wangu na kuwatafuta.
Kwa kuwa Bwana Yahwe asema hivi: Tazama! mimi mwenyewe nitawatafuta kondoo wangu na kuwaulizia,
12 Kama vile mchungaji atafutavyo kundi lake lililotawanyika wakati akiwa pamoja nalo, hivyo ndivyo nitakavyowatafuta kondoo wangu. Nitawaokoa kutoka mahali pote walipokuwa wametawanyikia katika siku ya mawingu na giza nene.
kama mchungaji atafutaye kundi lake juu ya siku hiyo yupo ndani ya kundi lake lililotawanyika. Hivyo nitalitafuta kundi langu, na nitalichunga kutoka sehemu lilipokuwa limetawanyika siku ya mawingu na giza.
13 Nitawatoa katika mataifa na kuwakusanya kutoka nchi mbalimbali, nami nitawaleta katika nchi yao wenyewe. Nitawalisha kwenye milima ya Israeli, katika mabonde na mahali pote panapokalika katika nchi.
Kisha nitalileta kutoka miongoni mwa watu; nitalikusanya kutoka nchi mbali mbali na kulileta kwenye nchi yao. Nitaliweka kwenye malisho juu ya pande za milima ya Israeli, karibu na vijito, na katika kila makazi katika nchi.
14 Nitawachunga kwenye malisho mazuri na miinuko ya mlima wa Israeli patakuwa mahali pao pa malisho. Huko watajipumzisha kwa amani katika nchi ya malisho mazuri, nao watajilisha huko katika malisho tele katika milima ya Israeli.
Nitawaweka kwenye malisho mema; juu ya milima ya Israeli itakuwa sehemu za malisho yao. Watalala chini huko katika sehemu nzuri kwa ajili ya malisho, katika malisho mengi, na watalisha juu ya milima ya Israeli.
15 Mimi mwenyewe nitawachunga kondoo zangu na kuwafanya wapumzike, asema Bwana Mwenyezi.
Mimi mwenyewe nitachunga kondoo wangu, na mimi mwenyewe nitawalaza chini-hivi ndivyo Bwana Yahwe
16 Nitawaulizia kondoo waliopotea na kuwaleta waliotangatanga. Nitawafunga waliojeruhiwa na kuwatia nguvu walio dhaifu lakini wale waliojikinai na wenye nguvu nitawaangamiza. Nitalichunga kundi kwa haki.
asemavyo-Nitawatafuta waliopotea nitawarudisha waliofukuzwa. Nitawafunga waliovunjika na kuwaponya kondoo waliougua lakini wanene na wenye nguvu nitawaharibu. Nitawalisha kwa haki.
17 “‘Kwa habari yenu, enyi kundi langu, hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Nitahukumu kati ya kondoo na kondoo, kati ya kondoo dume na mbuzi.
Hivyo sasa ninyi, kundi langu-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-tazama, nitakuwa hakimu kati ya kondoo na kondoo na kati ya kondoo dume na mbuzi dume.
18 Je, haiwatoshi ninyi kujilisha kwenye malisho mazuri? Je, ni lazima ninyi kuyakanyaga pia malisho yenu yaliyobaki kwa miguu yenu? Je, haiwatoshi ninyi kunywa maji safi? Je, ni lazima kuyachafua maji mengine kwa miguu yenu?
Je! haitoshi kulisha juu ya malisho mazuri, ambayo mtayakanyaga chini kwa miguu yenu kile kilichobakia kwenye malisho; na kunywa kutoka maji masafi, ambayo hakuna budi kuikanyaga mito kwa miguu yenu?
19 Je, ni lazima kundi langu wajilishe kwa yale mliyoyakanyaga na kunywa maji mliyoyachafua kwa miguu yenu?
Kondoo zangu zitakula kile mlichokanyagwa kwa miguu yenu, na kunywa maji yale mliyoyakanyaga kwa miguu yenu?
20 “‘Kwa hiyo, hili ndilo Bwana Mwenyezi awaambialo: Tazama, mimi mwenyewe nitahukumu kati ya kondoo wanono na waliokonda.
Kwa hiyo Bwana Yahwe anawaambia hivi; Tazama! Mimi mwenyewe nitahukumu kati ya wanene na waliokonda,
21 Kwa sababu mmewapiga kikumbo na kuwapiga kwa pembe zenu kondoo wote walio dhaifu mpaka wakawafukuza,
Kwa kuwa mmewasukuma kwa ubavu wenu na mabega, na kuwapiga kwa pembe wadhaifu wote kwa pembe zenu hadi mtakapowatawanya mbali kutoka kwenye nchi.
22 nitaliokoa kundi langu na hawatatekwa nyara tena. Nitahukumu kati ya kondoo na kondoo.
Nitaliokoa kundi langu na hawatakuwa mateka tena, na nitahukumu kati ya kondoo mmoja na mwingine!
23 Nitaweka juu yao mchungaji mmoja, mtumishi wangu Daudi, naye atawachunga, atawachunga na kuwa mchungaji wao.
Nitaweka juu yao mchungaji mmoja, mtumishi wangu Daudi. Atawachunga, atawalisha, na atakuwa mchungaji wao.
24 Mimi Bwana nitakuwa Mungu wao, naye mtumishi wangu Daudi atakuwa mkuu miongoni mwao. Mimi Bwana nimenena.
Kwa kuwa mimi, Yahwe, nitakuwa Mungu wao, na mtumishi wangu Daudi atakuwa mkuu kati yao-mimi, Yahwe, nimesema hivi.
25 “‘Nitafanya nao Agano la amani na kuwaondoa wanyama wa mwitu kutoka nchi yao ili kondoo wangu waweze kupumzika nyikani na msituni kwa salama.
Kisha nitafanya agano la amani pamoja nao na kuwaondoa wanyama waovu kutoka kwenye nchi, ili kwamba waishi salama katika jangwa na walale salama katika misitu.
26 Nitawabariki wao pamoja na maeneo yanayozunguka kilima changu. Nitawanyeshea mvua kwa majira yake, kutakuwepo mvua za baraka.
Pia nitaleta baraka juu yao na juu ya maeneo yazungukao kilima changu, kwa kuwa nitaleta manyunyu kwa wakati wake. Haya yatakuwa manyunyu ya baraka.
27 Miti ya shambani itatoa matunda yake na ardhi itatoa mazao yake, watu watakaa salama katika nchi yao. Watajua kuwa Mimi ndimi Bwana, nitakapovunja vifungo vya nira zao na kuwaokoa kutoka mikono ya wale waliowafanya watumwa.
Kisha miti ya shambani itazaa matunda yake, na dunia itashindwa kuzaa matunda yake. Kondoo wangu watakuwa salama katika nchi yao; kisha watajua ya kwamba mimi ni Yahwe, wakati nitakazipovunja fito za kongwa zao, na wakati nitakapowalinda kutoka kwenye mkono wa wale walio watumikisha.
28 Hawatatekwa tena nyara na mataifa, wala wanyama pori hawatawala tena. Wataishi kwa salama, wala hakuna yeyote atakayewatia hofu.
Hawatakuwa mateka tena kwa mataifa, na wanyama pori juu ya dunia hawatawameza tena. Kwa kuwa wataishi salama na wala hakuna mtu atakayewatia hofu.
29 Nitawapa nchi yenye sifa kutokana na mazao yake, hawatapatwa na njaa katika nchi tena wala hawatadharauliwa na mataifa.
Kwa kuwa nitatengeneza sehemu ya kulimia nzuri kwa ajili yao hivyo hawataangamia kwa njaa katika nchi, na mataifa hayataleta matukano juu ya yao.
30 Ndipo watakapojua kuwa Mimi, Bwana, Mungu wao, niko pamoja nao, na kwamba wao, nyumba ya Israeli, ni watu wangu, asema Bwana Mwenyezi.
Kisha watajua kwamba mimi, Yahwe Mungu wao, niko pamoja nao. Ni watu wangu, nyumba ya Israeli-hivi ndivyo Bwana Mungu asemavyo.
31 Ninyi ni kondoo wangu, kondoo wa malisho yangu, ninyi ni watu wangu, nami ni Mungu wenu, asema Bwana Mwenyezi.’”
Kwa kuwa ninyi ni kondoo wangu, kundi la malisho yangu, na watu wangu, na mimi ni Mungu wenu-hivi ndivyo Bwana Mungu asemavyo.”

< Ezekieli 34 >