< Ezekieli 32 >

1 Katika mwaka wa kumi na mbili, mwezi wa kumi na mbili, siku ya kwanza ya mwezi, neno la Bwana likanijia, kusema:
Kisha ikawa katika mwezi wa kumi na mbili wa mwaka wa kumi na mbili, siku ya kwanza ya mwezi, lile neno la Yahwe likanijia, kusema,
2 “Mwanadamu, fanya maombolezo kwa ajili ya Farao mfalme wa Misri na umwambie: “‘Wewe ni kama simba miongoni mwa mataifa, wewe ni kama joka kubwa baharini, unayevuruga maji kwa miguu yako na kuchafua vijito.
“Mwanadamu, inua maombolezo kuhusu Farao mfalme wa Misri; mwambie, 'Wewe ni kama simba mdogo juu ya mataifa, lakini kama jitu la kutisha, unatoka kwenye maji, unayachafua maji kwa miguu yako na kuyachafua maji yao.
3 “‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: “‘Nikiwa pamoja na wingi mkubwa wa watu nitautupa wavu wangu juu yako, nao watakukokota katika wavu wangu.
Bwana Yahwe asema hivi: Basi nitautandaza wavu wangu juu yako katika kusanyiko la watu wengi, na watawainua juu katika wavu wangu.
4 Nitakutupa nchi kavu na kukuvurumisha uwanjani. Nitawafanya ndege wote wa angani watue juu yako na wanyama wote wa nchi watajishibisha nyama yako.
Nitakuacha katika nchi. Nitakutupa kwenye shamba na kufanya ndege wote wa angani watue juu yako; njaa ya wanyama wote waishio juu ya nchi watashibishwa na wewe.
5 Nitatawanya nyama yako juu ya milima na kujaza mabonde kwa mabaki yako.
Kwa kuwa nitaiweka nyama yako juu ya milima, na nitayajaza mabonde kwa funza wako waliokufa.
6 Nitailowanisha nchi kwa damu yako inayotiririka njia yote hadi milimani, nayo mabonde yatajazwa na nyama yako.
Kisha nitamwaga damu yako juu ya milima, na vitanda vya kijito vitajazwa kwa damu yako.
7 Nitakapokuzimisha, nitafunika mbingu na kuzitia nyota zake giza; nitalifunika jua kwa wingu, nao mwezi hautatoa nuru yake.
Kisha wakati nitakapokuzimisha, nitazifunika mbingu na kuzitia giza nyota zake; nitalifunika jua kwa mawingu, na mwezi hautatoa nuru yake usiku.
8 Mianga yote itoayo nuru angani nitaitia giza juu yako; nitaleta giza juu ya nchi yako, asema Bwana Mwenyezi.
Mianga ya mbinguni nitaiweka giza juu yako, na nitaweka giza juu ya nchi-hivi ndivyo asemavyo Bwana Yahwe.
9 Nitaifadhaisha mioyo ya mataifa mengi nitakapokuangamiza miongoni mwa mataifa, nikikuleta uhamishoni miongoni mwa nchi ambazo haujapata kuzijua.
Hivyo nitaitisha mioyo ya watu wengi katika nchi ambao huwajui, wakati nitakapoleta kuhusu uvunjifu miongoni mwa mataifa, miongoni mwa nchi ambazo hukuzijua.
10 Nitayafanya mataifa mengi wakustaajabie, wafalme wao watatetemeka kwa hofu kwa ajili yako nitakapotikisa upanga wangu mbele yao. Siku ya anguko lako kila mmoja wao atatetemeka kila dakika kwa ajili ya maisha yake.
Nitawashangaza watu wengi kuhusiana na wewe; wafalme wao watatetemeka kwa hofu kuhusiana na wewe nitakapoutikisa upanga wangu mbele yao. Kila wakati kila mmoja atatetemeka kwa sababu yako, katika siku ya kuanguka kwako.
11 “‘Kwa kuwa hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: “‘Upanga wa mfalme wa Babeli utakuja dhidi yako.
Kwa kuwa Bwana Yahwe asema hivi: Upanga wa mfalme wa Babeli utakuja juu yako.
12 Nitafanya makundi yako ya wajeuri kuanguka kwa panga za watu mashujaa, taifa katili kuliko mataifa yote. Watakivunjavunja kiburi cha Misri, nayo makundi yake yote ya wajeuri yatashindwa.
Nitawafanya watu wako kuanguka kwa panga za mashujaa-kila shujaa ni tishio la mataifa. Hawa mashujaa watateketeza kiburi cha Misri na kuangamiza watu wake wote.
13 Nitaangamiza mifugo yake yote wanaojilisha kando ya maji mengi, hayatavurugwa tena kwa mguu wa mwanadamu wala kwato za mnyama hazitayachafua tena.
Kwa kuwa nitaiharibu mifugo yote kutoka karibu na maji mengi; na mguu wa mtu hautayatibua tena, wala kwato za wanyama hazitayatibua.
14 Kisha nitafanya maji yake yatulie na kufanya vijito vyake vitiririke kama mafuta, asema Bwana Mwenyezi.
Kisha nitayafanya maji yao kuwa matulivu na kufanya mito yao kukimbia kama mafuta-hivi ndivyo asemavyo Bwana Yahwe.
15 Nitakapoifanya Misri kuwa ukiwa na kuiondolea nchi kila kitu kilichomo ndani yake, nitakapowapiga wote waishio humo, ndipo watakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana.’
Wakati nitakapoifanya nchi ya Misri sehemu iliyojitenga, wakati nchi iliyopungukiwa na vitu viijazavyo, wakati nitakapo washambulia wakaao ndani yake, watajua yakwamba mimi ni Yahwe.
16 “Hili ndilo ombolezo watakalomwimbia. Binti za mataifa wataliimba, kwa kuwa Misri na makundi yake yote ya wajeuri wataliimba, asema Bwana Mwenyezi.”
Kutakuwa na maombolezo; binti za mataifa wataomboleza juu yake; wataomboleza juu ya Misri, juu ya watu wake wote wataomboleza-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.”'
17 Katika mwaka wa kumi na mbili, mwezi wa kwanza, siku ya kumi na tano ya mwezi, neno la Bwana likanijia kusema:
Kisha ikawa katika mwaka wa kumi na mbili, siku ya kumi na tano ya mwezi, lile neno la Yahwe likanijia, kusema,
18 “Mwanadamu, omboleza kwa ajili ya makundi ya wajeuri wa Misri na uwatupe kuzimu yeye na binti za mataifa yenye nguvu, waende huko pamoja nao washukao shimoni. (questioned)
“Mwanadamu, omboleza kwa ajili watu wa misri na walete chini-yeye na binti za mataifa mashuhuri-hata chini ya dunia pamoja na wale walioshuka chini kwenye shimo.
19 Je, ninyi mnamzidi nani kwa uzuri? Shukeni chini! Nanyi mkalazwe pamoja na hao wasiotahiriwa!
'Je! wewe ni mzuri zaidi kuliko mtu mwingine yeyote? Nenda chini na lala chini pamoja na wasiotahiriwa.'
20 Wataanguka miongoni mwa wale waliouawa kwa upanga. Upanga umefutwa, mwache aburutwe mbali pamoja na hao wajeuri wake wote.
Wataanguka miongoni mwao waliokuwa wameuawa kwa upanga. Upanga ulikuwa umewekwa! Alikuwa amepatiwa upanga; watamkamata na watu wake.
21 Kutoka kuzimu viongozi hodari watanena kuhusu Misri pamoja na wale walioungana nao, ‘Wameshuka chini, nao wamelala kimya pamoja na hao wasiotahiriwa, pamoja na wale waliouawa kwa upanga.’ (Sheol h7585)
Hodari wa wapiganaji katika Sheoli atasema kuhusu Misri na rafiki zake, 'Wameshuka chini hapa! Watalala pamoja na wasiotahiriwa, pamoja na wale waliokuwa wameuawa kwa upanga.' (Sheol h7585)
22 “Ashuru yuko huko pamoja na jeshi lake lote, amezungukwa na makaburi ya watu wake wote waliouawa, wale wote walioanguka kwa upanga.
Ashuru yupo huko pamoja na kusanyiko lake. Makaburi yake yamemzunguka; wote waliuawa kwa upanga.
23 Makaburi yao yako kwenye kina cha chini cha shimo na jeshi lake limelala kulizunguka kaburi lake. Wote waliokuwa wameeneza hofu kuu katika nchi ya walio hai wameuawa, wameanguka kwa upanga.
Wale ambao makaburi yao yamewekwa katika maficho ya mashimo yaliyo huko, pamoja na kusanyiko lake. Makaburi yake yakiwazunguka wote waliokuwa wameuawa, walioanguka kwa upanga, wale walioleta hofu juu ya nchi ya walio hai.
24 “Elamu yuko huko, pamoja na makundi yake yote ya wajeuri wakiwa wamelizunguka kaburi lake. Wote wameuawa, wameanguka kwa upanga. Wote waliokuwa wameeneza hofu katika nchi ya walio hai walishuka kuzimu bila kutahiriwa. Wanaichukua aibu yao pamoja na wale washukao shimoni. (questioned)
Elamu yupo huko pamoja na watu wake wote. Makaburi yake yamemzunguka; wote walikuwa wameuawa. Wale walioawa kwa upanga, walioshuka chini wasiotahiriwa hata sehemu ya chini kabisa ya dunia, waliowatia hofu juu ya nchi ya walio hai na wale waliobeba aibu yao wenyewe, pamoja na wale washukao chini kwenye shimo.
25 Kitanda kimetandikwa kwa ajili yake miongoni mwa waliouawa, pamoja na makundi yake yote ya wajeuri wakiwa wamelizunguka kaburi lake. Wote ni watu wasiotahiriwa, wameuawa kwa upanga. Kwa sababu vitisho vyao vilienea katika nchi ya walio hai, wameichukua aibu yao pamoja na wale washukao shimoni, nao wamewekwa miongoni mwa waliouawa.
Wamemuwekea kitanda kwa ajili ya Elamu na watu wake wote kati ya wachinjaji; kaburi lake limemzunguka. Wote hawajatahiriwa, kukatwa vipande kwa upanga, kwa sababu waliwaleta mashujaa wao juu ya nchi ya walio hai. Hivyo wamechukua aibu yao wenyewe, pamoja na wale washukao kwenye shimo miongoni mwa wote waliouawa, wale washukao kwenda shimoni. Elamu yu miongoni mwa wale waliokuwa wameuawa.
26 “Mesheki na Tubali wako humo, pamoja na makundi yao ya wajeuri wakiwa wameyazunguka makaburi yao. Wote hawakutahiriwa, wameuawa kwa upanga kwa sababu walieneza vitisho vyao katika nchi ya walio hai.
Mesheki, Tubali, na watu wake wote wako huko! Makaburi yao yamewazunguka. Wote hawajatahiriwa, wameuawa kwa upanga, kwa sababu walileta utiisho wao juu ya nchi ya walio hai.
27 Je, hawakulala na mashujaa wengine wasiotahiriwa waliouawa, ambao wameshuka kaburini wakiwa na silaha zao za vita, ambao panga zao ziliwekwa chini ya vichwa vyao na uovu wao juu ya mifupa yao? Adhabu kwa ajili ya dhambi zao ilikuwa juu ya mifupa yao, ingawa vitisho vya mashujaa hawa vilikuwa vimeenea hadi kwenye nchi ya walio hai. (Sheol h7585)
Wasilale pamoja mashujaa walioanguka wa wasiotahiriwa walioshuka chini kwa Sheoli pamoja na silaha zao zote za vita, na pamoja na panga zao zote walizoziweka chini ya vichwa vyao na maovu yao juu ya mifupa yao. Kwa kuwa walikuwa tishio kwa mashujaa katika nchi ya walio hai. (Sheol h7585)
28 “Wewe pia, ee Farao, utavunjwa nawe utalala miongoni mwa wasiotahiriwa, pamoja na wale waliouawa kwa upanga.
Basi wewe, Misri, utavunjika kati yao wasiotahiriwa! Utalala karibu nao waliokuwa wamekatwa vipande vipande kwa upanga.
29 “Edomu yuko humo, wafalme wake wote na wakuu wake wote, ambao ijapokuwa wana nguvu, wamelazwa pamoja na wale waliouawa kwa upanga. Wamelala pamoja na wasiotahiriwa, pamoja na wale washukao shimoni.
Edomu yuko huko na wafalme na viongozi wake wote. Walikuwa wamehifadhiwa katika uwezo wao pamoja na wale walioawa kwa upanga. Pamoja na wasiotahiriwa wamelala, pamoja na wale walioshuka kwenye shimo.
30 “Wakuu wote wa kaskazini na Wasidoni wote wako huko, wameshuka chini pamoja na waliouawa kwa aibu ijapokuwa kuna vitisho vilivyosababishwa na nguvu zao. Wamelala bila kutahiriwa pamoja na wale waliouawa kwa upanga na kuchukua aibu yao pamoja na wale washukao chini shimoni.
Wakuu wa kaskazini wako huko-wote na Wasidoni wote walioshuka chini pamoja na hao waliokuwa wamekatwa vipande vipande. Walikuwa na nguvu na kuwafanya wengine kuogopa, lakini sasa wako huko kwa aibu, wasiotahiriwa pamoja na wale waliokatwa vipande vipande kwa upanga. Wamebeba aibu yao wenyewe, pamoja nao waendao kwenye shimo.
31 “Farao, yeye pamoja na jeshi lake lote, atakapowaona atafarijiwa kwa ajili ya makundi yake yote ya wajeuri, wale waliouawa kwa upanga, asema Bwana Mwenyezi.
Farao ataona na kupata faraja kuhusu kundi lake waliokatwa vipande vipande kwa upanga -Farao na jeshi lake lote-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.
32 Ingawa nilimfanya Farao aeneze vitisho vyake katika nchi ya walio hai, Farao pamoja na makundi yake yote ya wajeuri watalazwa miongoni mwa wasiotahiriwa, pamoja na wale waliouawa kwa upanga, asema Bwana Mwenyezi.”
Natamuweka kama utiisho wangu katika nchi ya walio hai, lakini atakuwa amelazwa chini katikati yao wasiotahiriwa, miongoni mwa wale walio katwa vipande kwa upanga, Farao na makundi yake yote-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.

< Ezekieli 32 >