< Ezekieli 31 >
1 Katika mwaka wa kumi na moja, mwezi wa tatu, siku ya kwanza, neno la Bwana likanijia, kusema:
Kisha ikawa katika mwaka wa kumi na moja, katika mwezi wa tatu, siku ya kwanza ya mwezi, lile neno la Yahwe likanijia, kusema,
2 “Mwanadamu, mwambie Farao mfalme wa Misri na makundi yake ya wajeuri: “‘Je, ni nani awezaye kulinganishwa na wewe katika fahari.
“Mwanadamu, mwambie Farao, mfalme wa Misri, na watu wake wanaomzunguka, 'Katika ukuu wako, je! wewe ni kama nani?
3 Angalia Ashuru, wakati fulani ilikuwa mwerezi huko Lebanoni, ukiwa na matawi mazuri ukitia msitu kivuli; ulikuwa mrefu sana, kilele chake kilipita majani ya miti yote.
Tazama! Ashuru ilikuwa mwerezi katika Lebanoni pamoja na matawi mazuri, yakitoa kivuli kwenye msitu, na mirefu katika kimo, na matawi yalitengeneza kilele cha mti wake.
4 Maji mengi yaliustawisha, chemchemi zenye maji mengi ziliufanya urefuke; vijito vyake vilitiririka pale ulipoota pande zote na kupeleka mifereji yake kwenye miti yote ya shambani.
Maji mengi yaliufanya kuwa mrefu; maji ya chini yaliufanya kuwa mkuba. Mito ilitiririka sehemu zake zote, kwa kuwa mifereji yake ilitoa kuelekea kwenye miti yote katika shamba.
5 Hivyo ukarefuka kupita miti yote ya shambani; vitawi vyake viliongezeka na matawi yake yakawa marefu, yakitanda kwa sababu ya wingi wa maji.
Kimo chake kikubwa kilikuwa zaidi kuliko miti mingine yote katika shamba, na matawi yake yakawa mengi; matawi yake yalikuwa marefu kwa sababu ya maji mengi yalipokuwa yakikua.
6 Ndege wote wa angani wakaweka viota kwenye vitawi vyake, wanyama wote wa shambani wakazaana chini ya matawi yake, mataifa makubwa yote yaliishi chini ya kivuli chake.
Kila ndege wa mbinguni alitengeza kiota kwenye matawi yake, wakati kila kiumbe hai cha shamba kilizaa mtoto chini ya tawi. Mataifa mengi yote yaliishi chini ya kivuli chake.
7 Ulikuwa na fahari katika uzuri, ukiwa na matawi yaliyotanda, kwa kuwa mizizi yake ilikwenda chini mpaka kwenye maji mengi.
Kwa kuwa ulikuwa uzuri katika ukuu wake na kimo cha matawi yake, kwa kuwa mizizi yake ilikuwa katika maji mengi.
8 Mierezi katika bustani ya Mungu haikuweza kushindana nao, wala misunobari haikuweza kulingana na vitawi vyake, wala miaramoni haikulinganishwa na matawi yake, wala hakukuwa na mti katika bustani ya Mungu wa kulinganisha na uzuri wake.
Mierezi katika bustani ya Mungu haikuweza kuwa sawa nayo. Hakuna miongoni mwa miti ya mivinje iliyofanana matawi yake, na miti ya miamori haikuweza kuwa sawa na majani yake. Hapakuwa na mti mwingine katika bustani ya Mungu ulikuwa kama huo katika uzuri wake.
9 Niliufanya kuwa mzuri ukiwa na matawi mengi, ulionewa wivu na miti yote ya Edeni katika bustani ya Mungu.
Nimeufanya kuwa mzuri pamoja na matawi yake mengi na miti yote ya Edeni iliyokuwa katika bustani ya Mungu ilimwonea wivu.
10 “‘Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Kwa sababu ulikuwa mrefu sana, kilele chake kikiwa juu ya majani manene ya miti na kwa sababu ulikuwa na kiburi cha urefu wake,
Kwa hiyo Bwana Yahwe asema hivi: Kwa sababu ilikuwa mirefu kwa kina, na imekiweka kilele chake kati ya matawi yake, moyo wake umeinua kwa sababu ya urefu wake.
11 niliutia mikononi mwa mtawala wa mataifa, ili yeye aushughulikie sawasawa na uovu wake. Nikaukatilia mbali,
Nimeuweka kwenye mikono ya yeye mwenye uweza wa mataifa, kuishughulikia kulingana na yale maovu anayostahili. Nimeufukuza.
12 nayo mataifa mageni yaliyo makatili sana yaliukata huo mti na kuuacha. Matawi yake yalianguka juu ya milima na kwenye mabonde yote, vitawi vyake vikavunjika na kusambaa katika makorongo yote ya nchi. Mataifa yote ya duniani yakaondoka kutoka kwenye kivuli chake na kuuacha.
Wageni waliokuwa wakiogofya wa mataifa yote wameikatilia mbali kuiacha ife. Matawi yake yameanguka kwenye milima na mabonde yote, na matawi yake yameanguka katika mito yote ya nchi. Kisha mataifa yote juu ya nchi wakatoka nje kutoka chini ya kivuli na kwenda zao wakamwacha.
13 Ndege wote wa angani wakakaa kwenye ule mti ulioanguka na wanyama pori wote wakakaa katikati ya vitawi vyake.
Ndege wa agani watapumzika kwenye shina la mti ulioanguka, na kila mnyama wa shambani atakuja kwenye matawi yake.
14 Kamwe hakutakuwa na miti mingine kando ya hayo maji itakayorefuka zaidi ya huo, vilele vyake vikiwa juu ya majani yote ya miti. Hakuna miti mingine, hata kama imekunywa maji vizuri namna gani, itakayofikia urefu huo. Yote mwisho wake ni kifo, na kuingia ardhini, kama vile ilivyo kwa wanadamu, pamoja na wale waendao shimoni.
Hii litokea ili kwamba pasiwe na miti mingine itakayopandwa karibu na maji yatang'oa majani yake hata kwenye kina cha miti mirefu, na kwamba hakuna miti mingine itakayomea karibu na maji itakayofikia kwenye hicho kina. Wote wametolewa kufa, chini ya nchi, miongoni mwa watoto wa binadamu, pamoja na wale washukao chini.
15 “‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Katika siku ile mwerezi uliposhushwa chini kaburini nilizifunika chemchemi zenye maji mengi kwa maombolezo: Nilivizuia vijito vyake na wingi wa maji yake nikauzuia. Kwa sababu yake niliivika Lebanoni huzuni, nayo miti yote ya shambani ikanyauka. (Sheol )
Bwana Yahwe asema hivi: Katika siku wakati mkangazi uliposhuka chini nilileta maombolezo kwenye dunia. Niliyafunika maji ya chini juu yake, nikayarudisha maji ya bahari. Nilizuia maji makuu, nikaleta maombolezo hata Lebanoni kwa ajili yake. Hivyo miti yote ya shambani ikaomboleza kwa sababu yake. (Sheol )
16 Niliyafanya mataifa yatetemeke kwa kishindo cha kuanguka kwake wakati nilipoushusha chini kaburini pamoja na wale washukao shimoni. Ndipo miti yote ya Edeni, miti iliyo bora kuliko yote na iliyo mizuri sana ya Lebanoni, miti yote ile iliyokunywa maji vizuri, ilifarijika hapa duniani. (Sheol )
Nimeleta tetemeko kwa mataifa wa sauti ya kuanguka kwake, wakati nitakapomtupa chini mpaka kuzimu pamoja na wale walioenda chini kwenye shimo. Hivyo niliitia moyo miti ya Edeni yote katika pande zote za nchi. Hii ilikuwa imechaguliwa na miti iliyokuwa bora ya Lenanoni; miti iliyokunywa maji. (Sheol )
17 Wale walioishi katika kivuli chake, wale walioungana naye miongoni mwa mataifa, nao pia walikuwa wamezikwa pamoja naye, wakiungana na wale waliouawa kwa upanga. (Sheol )
Kwa kuwa walikwenda chini pia pamoja nayo hata kuzimu, kwa wale waliokuwa wameuawa kwa upanga. Kulikuwa na jeshi lake imara, yale mataifa yalikuwa yakiishi kati kivuli chake. (Sheol )
18 “‘Ni miti ipi ya Edeni inayoweza kulinganishwa nawe kwa fahari na utukufu? Hata hivyo, wewe pia, utashushwa chini pamoja na miti ya Edeni mpaka kuzimu, utalala miongoni mwa wasiotahiriwa, pamoja na wale waliouawa kwa upanga. “‘Huyu ni Farao pamoja na makundi yake yote ya wajeuri, asema Bwana Mwenyezi.’” ()
Umefanana na nani hivi katika utukufu na ukuu kati ya mti wa Edeni? Kwa kuwa utashushwa chini pamoja na miti ya Edeni hata pande zote nne za dunia miongoni mwa wasiotahiriwa; utaishi pamoja na watu wake wote-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavy.”